Mshua alinichapaga viboko mbele ya demu wangu alikuja kusuka.
Dingi amekuja mchana kula chakula akakuta hakuna maji hata ya kunawa mikono, kubabake alinichapa sticki hizo.
Demu wangu alikua nje anasukwa na dada yangu, dingi ananichapia sebuleni.
Kwa kuwa nilikua sitaki demu wangu ajue kama nachapwa, nikawa najikaza sipigi kelele.
Dingi akajua viboko havini umizi, akaanza kunipiga na mavibao, kubabake nilivimbaga mikononi.
Mara Paaaap nikatoka na mindoo kwenda kuchota maji, mialama ya viboko kwenye matako, mgongoni, mikononi.
2001 hiyo Kiloleni Tabora