Wenye "madingi" wakali tukutane hapa

Kwa nini alikuwa mkali?
 
Nakumbuka nilikuwa napenda sana kutengeneza manati.sasa kama mnavyojua manati yanatakiwa yawe na like kingozi cha kushikia jiwe,na lazima kiwe kilaini.sasa bwana huku na huku nikatafuta ngozi bila mafanikio.akili ikanituma nikakate kiatu cha baba anachokipenda kuliko vyote.kilichotokea alivyorudi huwa ctak kukumbuka maana alinipa kichapo kiwango cha lami.
 
Mzee wangu alikua mtata ila hamzidi kaka yake ambae ni baba mkubwa aisee kwanza nililijua jina halisi la baba mkubwa nikiwa umri umeenda ila nilijua jina la baba mkali alikua akija kusalimia home yeye ndo anakua kama baba mwenye nyumba anapiga mkwala mpk mdgo wake aisee kile kchwa balaa watoto wake walikuwa mamenyooka kama nguo ya kamanda siro kwake kulikua na taratibu ambazo kamwe hazivunjwi aisee apumzike kwa amani
 
Mkuu Raphael wa Ureno, nimecheka sana, najua ushapoa sasa hakuna haja ya pole.

Kibishi tu sasa hivi nikimtazama huwa naona kama Bro wangu hana noma, Mara ya Mwisho ananipiga ilikuwa niko Darasa la nne, alikuwa yupo safarini ila asubuhi aliniita chumbani akanipa majukumu ya kufanya, Nimeamka tu nikaenda kusakata kabumbu nikijidai Maradona hadi saa 12 jioni ndipo Maradona anarudi nyumbani akamkuta baba yake kafika hakuna kazi yeyote iliyotendeka.

Kipigo cha Kufa Mbwa kikamhusu Maradona, Kilichoniokoa niliona nikiendelea kulia na kupiga kelele nitakufa kwa ngumi na makofi ya Baba yake Maradona basi Nikajidai nimezima anapiga sitikisiki wala kugeuka kapiga kama dakika 1 kashituka, akajua Maradona Kafariki, alikuwa na buti moja chini limeandikwa Base akanikanyaga nalo duh maumivu yale yalimtoa chini Maradona akasepa mwendo wa Kimondo kuelekea kusikojulikana.

Tangu Siku hiyo hakunipiga tena.
 
Nimelelewa na Baba mdogo ila mtata kinoma,kuna siku alisafiri huku nyuma mi nkaacha kwenda chuo(madrasa),mama akiniambia niende chuo namwambia 'kausha' basi siku aliorudi akaambiwa taarifa zangu,mzee akaniita akiwa na gunia la bakora,akaniambia nivue nguo zote,baada ya kusaula alinipa kichapo ambacho siwez sahau,baada ya kunichapa sana akawa ananizungusha mtaani mm mbele yeye nyuma huku akiniteremshia mvua ya bakora tena akawa ananiambia niwe naimba hv,mm cna akili,mm mwehu,mm kichaa nisiependa chuo,basi alinikimbisha mchaka mchaka wa bakora mtaa mzima,nilvyoona hali mbaya na yeye hana dalili za kuniacha nkakimbilia msikitini maana ilikua mida km ya saa 2 hv usiku,mzee nkajitosa msikitini mzima mzima nliwakuta na wanakimu kwa ajili ya kuaza swala,hapo ndo ikawa ponea yangu maana wazee wa msikiti walimuona anisamehe japo alikua mgumu kunisamehe lkn mwisho akakubali kunisamehe,yy alitaka aendelee na lile zoezi usiku kucha,basi asubuhi yake nkaamka nkiwa na vidonda vya haja,alafu mtaan ikawa gumzo kila nnapopita nachekwa tena hadi na madem zangu,alafu pale mwanzo alipokua ananiamuru nivue nguo ile chupi nkawa cjaiweka chini,maana nlipovua chupi tu kichapo kikaanza kwa hiyo nkakosa nafasi ya kuiweka chini,hivyo mda wote wa mchaka mchaka wa mateso ile chupi nlikua nayo mkononi,(tena kipindi nakimbizwa na fimbo kulikua na kundi la watoto walikua wameunga ule mchakamchaka huku wakishangilia mm nnavyoadhirika) sasa baada ya kuingia msikitini wale mashekhe wakanitoa nje ili waongee na mdingi ili anisamehe,sasa mdingi alivyofika tu akanichapa bakora ya mkono tena ule mkono nlioishika ile chupi,kutokana na mshituko ile chupi ikaniluka na ckujua imelukia wapi kwa wakat huo,kumbe ile chupi ilirukia juu ya paa la msikiti,asubuhi yake watu(hasa watoto wenzangu) wakaiona juu ya bati basi ikawa stori tena kila nkipita nachekwa na kukejeliwa juu ya kile kichapo na chupi yangu kuwa juu ya paa la msikiti,ile chupi ilifanya tukio langu lisisahaulike haraka halafu ikanishangaza ilikua haianguki hata mvua iminyesha kias gani,ilikaa zaidi ya mwezi mmoja pale juu hadi ilipodondoka ndo nkaanza kua na amani maana watu wakaanza kusahau kile kipondo changu,hadi leo nmebaki na makovu km kumbukumbu ya lile tukio,USIOMBE YAKUKUTE
 
Mzee wako alikuwa msala... Mm kuna jirani yangu alikuwa ni mtata sana, alikuwa anadaka madogo anawafungia kwenye mfuko ile ya kamba za katani anawapandishia darini la jikoni halafu anatafuta kuni zinazo toa moshi mwingi anawafukiza wakiwa huko darini hahaha
 
Mzee kwel alikuwa hatari"kimbia ukiwa mbali sema tayari"
 
Malizia mkuu hamna tatizo just fun
 
Yaaani Nimecheka mpka nimejamba.
 
bado yupo hai kweli maana hafai hata kidogo
 
hahahahaha izo taratibu sasa ivi zinavunjwa tu
 
hahahahaha hafai kwa jamii huyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…