Nimelelewa na Baba mdogo ila mtata kinoma,kuna siku alisafiri huku nyuma mi nkaacha kwenda chuo(madrasa),mama akiniambia niende chuo namwambia 'kausha' basi siku aliorudi akaambiwa taarifa zangu,mzee akaniita akiwa na gunia la bakora,akaniambia nivue nguo zote,baada ya kusaula alinipa kichapo ambacho siwez sahau,baada ya kunichapa sana akawa ananizungusha mtaani mm mbele yeye nyuma huku akiniteremshia mvua ya bakora tena akawa ananiambia niwe naimba hv,mm cna akili,mm mwehu,mm kichaa nisiependa chuo,basi alinikimbisha mchaka mchaka wa bakora mtaa mzima,nilvyoona hali mbaya na yeye hana dalili za kuniacha nkakimbilia msikitini maana ilikua mida km ya saa 2 hv usiku,mzee nkajitosa msikitini mzima mzima nliwakuta na wanakimu kwa ajili ya kuaza swala,hapo ndo ikawa ponea yangu maana wazee wa msikiti walimuona anisamehe japo alikua mgumu kunisamehe lkn mwisho akakubali kunisamehe,yy alitaka aendelee na lile zoezi usiku kucha,basi asubuhi yake nkaamka nkiwa na vidonda vya haja,alafu mtaan ikawa gumzo kila nnapopita nachekwa tena hadi na madem zangu,alafu pale mwanzo alipokua ananiamuru nivue nguo ile chupi nkawa cjaiweka chini,maana nlipovua chupi tu kichapo kikaanza kwa hiyo nkakosa nafasi ya kuiweka chini,hivyo mda wote wa mchaka mchaka wa mateso ile chupi nlikua nayo mkononi,(tena kipindi nakimbizwa na fimbo kulikua na kundi la watoto walikua wameunga ule mchakamchaka huku wakishangilia mm nnavyoadhirika) sasa baada ya kuingia msikitini wale mashekhe wakanitoa nje ili waongee na mdingi ili anisamehe,sasa mdingi alivyofika tu akanichapa bakora ya mkono tena ule mkono nlioishika ile chupi,kutokana na mshituko ile chupi ikaniluka na ckujua imelukia wapi kwa wakat huo,kumbe ile chupi ilirukia juu ya paa la msikiti,asubuhi yake watu(hasa watoto wenzangu) wakaiona juu ya bati basi ikawa stori tena kila nkipita nachekwa na kukejeliwa juu ya kile kichapo na chupi yangu kuwa juu ya paa la msikiti,ile chupi ilifanya tukio langu lisisahaulike haraka halafu ikanishangaza ilikua haianguki hata mvua iminyesha kias gani,ilikaa zaidi ya mwezi mmoja pale juu hadi ilipodondoka ndo nkaanza kua na amani maana watu wakaanza kusahau kile kipondo changu,hadi leo nmebaki na makovu km kumbukumbu ya lile tukio,USIOMBE YAKUKUTE