Wenye "madingi" wakali tukutane hapa

bado yupo hai kweli maana hafai hata kidogo
ni kati ya watu wa maana sana kwangu asee alifariki 96...kwetu mpaka leo hamna t.v kuna santuri na shelfu la vitabu..alikua mtu wa haki sana sema adhabu zake si za nchi hii...kadri siku zinavyoenda huwa natamani sana kuwa kama yeye but siwezi..ila kaka yangu hakuwahi kumpenda mpaka na sidhan kama hata anamkumbukaga
 
hahahahahhaha mada nzima chupi na sio dingi tena hahahahah
 
Ni ukweli usiopingika Wazee wa zama zile wengi wao walikuwa wakali hatari,walikuwa hawataki mchezo na wakiwepo full heshima yaani mpaka raha;na kipindi hicho vijana weng walikuwa na sifa ya ukorofi acha hawa wa siku hizi;Mzee akiwepo Nyumbani ni kimya na wala hakuna kutangatanga,kuropoka au kulala lala ovyo bila kazi,na masister walikuwa hawabebi mimba wakiwa Nyumbani maana mziki wake wanaujua ila Wazee wa siku hizi jina tu,madada wanazaa ovyo ovyo na vijana nao wapo huru kufanya watakayo,kiufupi mambo yamebadilika kwa sasa,Wazee wa miaka ile walikuwa Wakoloni kwwl
 
Khaaa huyu alikuwa zaidi ya mkali
 
Hapa huwezi kusema baba yako ni mkali
 
mkuu ilikuwa wapi hyoo???

umenikumbusha kitambo sana

mie nakumbuka enzi hizo kuna siku sikuenda madrasa mda wa jioni asee mdingi kurudi si akapata taarifa kwamba dogo sijaenda madrasa dooooohhhh..

nlikaa nje tangu saa tatu usiku mpaka mda usiofahamika mpaka kuna jirani yetu akanionea huruma akanichukua nikaenda kulala kwake mpaka asubuhi ...

mzee alikuwa hataki mchezo kabisa aseee
 
Dah Mzee mbabe sana
 
Daaah,maisha haya!!
Mkuu umenikumbusha maisha yangu ya utotoni.

Kwa asilimia kubwa mzee alikuwa huko job mwanza, lakini kila weekend alikuwa anarudi home.

Huyu mzee alikuwa mkali na mbabe haswaa!!

Kwanza tulikuwa tumenunuliwa saa za mkononi,inatakiwa saa kumi na mbili jioni uwe umesharudi home,ukichelewa hata dakika moja utakula kichapo kikali sana.

Kaka yetu mkubwa kwa sasa ni marehemu,alichelewa kurudi home,mzee akazama kitaani kumtafuta mwenyewe,aliporudi nae akajifungia nae ndani,brother alikula kichapo heavy mpaka akachanganyikiwa, mzee akawa anamuuliza nimekukuta wapi?Bro,anajibu nimesahau uliponikutia!!

Mungu amjaalie umri mrefu sana,kwa sasa ana miaka 70 lakini hadi wajukuu wakizingua wanachezea kichapo.


Mimi mwenyewe siwezi kumjibu nikiwa karibu,akiwa anakuuliza ukikaa kimya ni kichapo unadharau,halafu ukimjibu unapigwa vibao kwa sababu ni kiburi kumjibu.

Sio mzungumzaji sana lakini ukiongea nae akikwambi,unyamaze imetosha!!unapaswa kunyamaza,ukiendelea kuongea una hamu ya kukandwa
 
Hahahaa kama nawaona mlivyokuwa mnatamani kurudisha siku nyuma weekend isifike
 
We jamaa unaongelea kuchapwa na waya za umeme??....me nlichapwa na hizo waya, mipira ya maji mzee akaona hii bado nunda...basi akatafuta kipande cha waya unaoshikilia nguzo za simu (steel wire).....daahh ilikua shughuli, nlipigwa tatu tu ila ziligonga hadi mifupa!!!
 
Hahahah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…