Singida ndio home
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 3,188
- 3,370
Mafuta ni kitu muhimu kwenye gari, Ni mara kwa mara tunayajaza haya mafuta lakini tukumbuke pia unaweza kupigwa mchana kweupe.
Hakikisha kabla hujajaza mafuta ile pump ya kujazia imerudishwa kikamilifu kwenye mashine, Pump inaporudishwa lazima mashine isome 0.00, ila endapo pump ikategeshwa ionekane kwamba imerudishwa haitasome 0.00 hapo utakuwa umepigwa.
Hakikisha kwamba ukiweka mafuta basi kiasi kamili kiwekwe bila kuunga unga, mfano ukiwaambia wakuwekee mafuta ya elf 10 wasiweke ya elfu mbili alafu kwenye mashine waongezee ya elfu nane bila kurudisha pump ili isome 0.0, kitachotokea ni kwamba watakuingizia ya elfu mbili tu hayo ya elfu 8 hayatoki itatoka hewa tu.
Mwenzako wa mbele anapojaziwa sisitiza sana pump ipachikwe kwenye mashine ili isome 0;00 usiruhusu mwenzako wa mbele ajaziwe na wewe ujaziwe mafuta bila pump kurudishwa kwenye mashine ili ianze upya.
Hakikisha unaangalia kwenye kioo wameingiza pump kwenye gari yako, ukiwa mzembe wanaweza wanaweza kujijazia kwenye vigaloni.
Omba risiti na uhakikishe ni ya pump waliyokujazia na muda uendane na ulipojaza, nakumbuka niliwahi kupewa risiti ya saa tatu asubuhi wakati nimejaza jioni.
Muhimu: Kwa hizi njia anayeiba sio sheli ni mtu. Usipumbazwe na sheli fulani kusifiwa.
zamani watu wakihisi wanapigwa walikua wanaenda na vidumu vyeupe vile vinavyoonesha ujazo ila Tangu mwaka 2009 EWURA ilipopiga marufuku unaweza kukataliwa kujaziwa, ukitaka kujaziwa uende kirafiki usiende kwa nia ya kuhisi wanakuibiaga.