Wenye magari pitieni hapa kuepuka kupigwa vituo vya mafuta

Wenye magari pitieni hapa kuepuka kupigwa vituo vya mafuta

Du haya,yangu macho mie,ila wawe na huruma hawajui mtu anaenda wapi na kakadiria mafuta yake we unayapunguza anapaki gari porini anavamiwa na majambazi,hakika hiyo laana itakula ukoo wenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vilikatazwa na nani? Ukiwa na generator nyumbani unanunuaje mafuta?
Mkuu una muda gani tangu uanze kwenda sheli😳😳?? Tangu 2009 MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA), ilipiga marufuku, ukienda kwa gia za kupaki gari karibu na sheli na kushuka na kigaloni chako wana kila sababu ya kukukatalia
 
Na kituo cha mafuta ambacho wanatabia ya wizi, ukienda na kidumu wanakuangalia vibaya....

Na ukinunua mafuta ya kidumu let's say 10000 yanafanya mizunguko mingi kuliko kununua ya 10000 direct kwenye tank ya gari..

Tanzania shida tupu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu una muda gani tangu uanze kwenda sheli😳😳?? Tangu 2009 MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA), ilipiga marufuku, ukienda kwa gia za kupaki gari karibu na sheli na kushuka na kigaloni chako wana kila sababu ya kukukatalia
Jana tu nimetoka "sheli" lakini hujajibu swali langu la pili.
 
Hivi kwanini unaitwa Sheli? Maana Sheli ni kampuni kama Total au Meru.

Ni sawa na useme Total ndio Meru bora[emoji2]

Sent using Jamii Forums mobile app
Sababu ni rahisi tu ndugu yangu. Hii ni kampuni ya kuuza mafuta iliyotamalaki sana katika nchi hii hapo siku za nyuma. Kumbuka kabla ya ubinafsishaji, kampuni binafsi za mafuta zilikuwa chache sana. Hivyo kutokana na ukubwa wake na kusambaa nchini, vituo vyake vikajipatia brand name ya shell. Tangia hapo ikaonekana kuwa kumbe kituo chochote cha kuuzia mafuta ni shell. Kibiashara tunasema kama ni kupromote kampuni tu, basi lengo lilifikiwa na kuzidi.
 
Sidhani kama wa Dar wanafanya wizi wa kiboya hivyo. Ila juzi kituo kimoja hapo Dar kwenu Kuna Binti alitaka kunipiga kijinga sana, nilimwambia mafuta elfu 15, na nikampatia pesa kabisa, akaweka elfu Tisa! Nikamuuliza mbona unaweka 9,000?? Akasema hakusikia vizuri akajifanya kuangalia mkononi nimempa bei gani, akakuta 15,000! Basi akaweka tena mafuta ya 7,000 ili kufidia, nikamwambia umenizidishia buku akakataa tena, tukapiga hesabu nikamuongezea buku yake nikaondoka zangu

Umepigwa mkuu hii mbinu inaitwaga "unga unga" amekujazia ya 9,000 maksudi hayo uliyoongezewa ya elf saba umejaziwa hewa kwasababu haku reset machine, UMEPIGWA!!!

Siku nyingine nenda na kamera ya ushahidi akikufanyia tena wakujazie Lita 50 lasivyo tishia juisambaza video
 
Back
Top Bottom