Wenye magari pitieni hapa kuepuka kupigwa vituo vya mafuta

Umepigwa mkuu hii mbinu inaitwaga "unga unga" amekujazia ya 9,000 maksudi hayo uliyoongezewa ya elf saba umejaziwa hewa kwasababu haku reset machine, UMEPIGWA!!!

Siku nyingine nenda na kamera ya ushahidi akikufanyia tena wakujazie Lita 50 lasivyo tishia juisambaza video
Hahhahhaha weeee mimi bila machine kusoma sifuri za kutosha sikubali
 
Alivyoanza kujaza hayo ya elfu tisa machine ilikuwa inasoma 0.000 lakini he alivyomaliza kujaza hayo ya elfu Tisa Ali reset upya mashine ili akuongezee yaliyobaki ya elfu sita??? Hadi umewekewa hayo mafuta ya elfu saba badala ya elfu sita amini usiamini kuna mchezo ulichezwa
 
Hahahaha Mpwa, she was trying to teach an old Dog new tricks! Mzee kitu lazima isome masifuri! Hakuna sifuri tunaanza upya au tunaahirisha gemu
 
nevertheless an old dog can still be fooled by old tricks🙂🙂, vp lakini si ulichukua risiti mbili ile ya elfu 9 na ya elfu 6, au uliziacha
 
Ukiwa na jenereta nyumbani utaenda na madumu wanayotaka ambayo hadi Leo sijui yapoje,
Basically, EWURA wamezuia watu kununua mafuta kwenye vidumu bila ya kutoa mwongozo wenye generators wananunuaje mafuta?
 
foto28493.jpg

Mafuta ni kitu muhimu kwenye gari, Ni mara kwa mara tunayajaza haya mafuta lakini tukumbuke pia unaweza kupigwa mchana kweupe.

Hakikisha kabla hujajaza mafuta ile pump ya kujazia imerudishwa kikamilifu kwenye mashine, Pump inaporudishwa lazima mashine isome 0.00, ila endapo pump ikategeshwa ionekane kwamba imerudishwa haitasome 0.00 hapo utakuwa umepigwa.

Hakikisha kwamba ukiweka mafuta basi kiasi kamili kiwekwe bila kuunga unga, mfano ukiwaambia wakuwekee mafuta ya elf 10 wasiweke ya elfu mbili alafu kwenye mashine waongezee ya elfu nane bila kurudisha pump ili isome 0.0, kitachotokea ni kwamba watakuingizia ya elfu mbili tu hayo ya elfu 8 hayatoki itatoka hewa tu.

Mwenzako wa mbele anapojaziwa sisitiza sana pump ipachikwe kwenye mashine ili isome 0;00 usiruhusu mwenzako wa mbele ajaziwe na wewe ujaziwe mafuta bila pump kurudishwa kwenye mashine ili ianze upya.

Hakikisha unaangalia kwenye kioo wameingiza pump kwenye gari yako, ukiwa mzembe wanaweza wanaweza kujijazia kwenye vigaloni.

Omba risiti na uhakikishe ni ya pump waliyokujazia na muda uendane na ulipojaza, nakumbuka niliwahi kupewa risiti ya saa tatu asubuhi wakati nimejaza jioni.

Muhimu: Kwa hizi njia anayeiba sio sheli ni mtu. Usipumbazwe na sheli fulani kusifiwa.

zamani watu wakihisi wanapigwa walikua wanaenda na vidumu vyeupe vile vinavyoonesha ujazo ila Tangu mwaka 2009 EWURA ilipopiga marufuku unaweza kukataliwa kujaziwa, ukitaka kujaziwa uende kirafiki usiende kwa nia ya kuhisi wanakuibiaga.

View attachment 1324474
Kama naenda kuweka kwenye kajenereta kangu nyumbani naweka wapi petrol? Au itabidi nikibebe Hadi petrol station?
 
Tusahihishe kidogo hapa sheli ni kampuni ya mafuta kama ilivyo BP, Total na vingine isomeke wanafanya vizuri ukifanananisha na vituo vingine vya Mafuta.Tulizoea kuita Shel nafikiri ni kampuni ya mwanzo kabisa kua na vituo vya mafuta
Kabisa mKuu, Puma na total wako vizuri... Ukiweka mafuta mshale unaona kabisa unapanda [emoji23] tofaut na sheli nyingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tusahihishe kidogo hapa sheli ni kampuni ya mafuta kama ilivyo BP, Total na vingine isomeke wanafanya vizuri ukifanananisha na vituo vingine vya Mafuta.Tulizoea kuita Shel nafikiri ni kampuni ya mwanzo kabisa kua na vituo vya mafuta

Sent using Jamii Forums mobile app
Hizo habari si kwamba hatuzijui mkuu... Tunazijua ila ndio tumezoea kuita sheli na najua umeelewa...
 
Nadhani ifikie mahali BAKITA na TUKI wafanye usanifishaji wa neno SHEL (sheli) ili liingizwe kwenye kamusi ya Kiswahili na liwe na maana ya kituo chochote cha kujazia mafuta.

....coz bongo tumeshazoea kila kituo cha mafuta tunakiita Sheli
Hizo habari si kwamba hatuzijui mkuu... Tunazijua ila ndio tumezoea kuita sheli na najua umeelewa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni kwa staili hii basi nilishapigwa, niliweka mafuta lakini mpaka naondoka kituoni pale mpaka nafika nyumbani mshale haukusogea hata nukta, nikasema tu nimeibiwa ila sikujua nimeibiwaje maana kiwango cha mafuta kinachoingia cha hiyo pesa nakijua. Nilitamani kesho yake nipite niwaambie lakini sikuwa na ushahidi madhubuti wa hili.
Asante kwa elimu hii.
 
foto28493.jpg

Mafuta ni kitu muhimu kwenye gari, Ni mara kwa mara tunayajaza haya mafuta lakini tukumbuke pia unaweza kupigwa mchana kweupe.

Hakikisha kabla hujajaza mafuta ile pump ya kujazia imerudishwa kikamilifu kwenye mashine, Pump inaporudishwa lazima mashine isome 0.00, ila endapo pump ikategeshwa ionekane kwamba imerudishwa haitasome 0.00 hapo utakuwa umepigwa.

Hakikisha kwamba ukiweka mafuta basi kiasi kamili kiwekwe bila kuunga unga, mfano ukiwaambia wakuwekee mafuta ya elf 10 wasiweke ya elfu mbili alafu kwenye mashine waongezee ya elfu nane bila kurudisha pump ili isome 0.0, kitachotokea ni kwamba watakuingizia ya elfu mbili tu hayo ya elfu 8 hayatoki itatoka hewa tu.

Mwenzako wa mbele anapojaziwa sisitiza sana pump ipachikwe kwenye mashine ili isome 0;00 usiruhusu mwenzako wa mbele ajaziwe na wewe ujaziwe mafuta bila pump kurudishwa kwenye mashine ili ianze upya.

Hakikisha unaangalia kwenye kioo wameingiza pump kwenye gari yako, ukiwa mzembe wanaweza wanaweza kujijazia kwenye vigaloni.

Omba risiti na uhakikishe ni ya pump waliyokujazia na muda uendane na ulipojaza, nakumbuka niliwahi kupewa risiti ya saa tatu asubuhi wakati nimejaza jioni.

Muhimu: Kwa hizi njia anayeiba sio sheli ni mtu. Usipumbazwe na sheli fulani kusifiwa.

zamani watu wakihisi wanapigwa walikua wanaenda na vidumu vyeupe vile vinavyoonesha ujazo ila Tangu mwaka 2009 EWURA ilipopiga marufuku unaweza kukataliwa kujaziwa, ukitaka kujaziwa uende kirafiki usiende kwa nia ya kuhisi wanakuibiaga.

View attachment 1324474
vipi risiti za TRA, Tunazo pewa!
 
Back
Top Bottom