Wenye majengo walipe wenyewe kodi ya jengo

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
21,741
Reaction score
26,735
Matajiri wajanja wametusukumizia kodi za majengo yao wanayowapangisha wageni tuzilipe sisi ambao hata bei ya tofali hatuijui.

Wajanja hawa kama wangekuwa na nia nzuri na sisi masikini wangeweka bima ya afya (NHIF) tuilipe kwenye mfumo wa LUKU, hii ingetuwezesha tusio na uwezo wa kulipa kwa mkupuo tuwe na bima.

Rais Samia wajanja wamekuzidi kete kwa hili, ondoa kodi ya jengo masikini kuwalipia matajiri weka masikini kujilipia Bima ya Afya kwa mfumo wa LUKU.
 
Aise awamu hii mpaka nauli zimepanda. Nimeshangaa juzi nalipia dstv eti nako kuna ada ya kufanya muamala.

Nikabaki nashangaa sijui tumefikaje huku
 
Mfumo wa malipo ya Kodi ya majengo bado uko vilevile sema imepanda mpka 12000 nenda ofisi za TRA zilizo karibu nawe. Marekebisho ya kodi hiyo bado hayajafanyika kwenye system ili kuweza kulipa kwa hiyo LUKU.
 
Inawezekana bado haujauelewa,nlinunua LUKU nikakatwa japo sina jengo! Wameipa jina la TRAN FEE! ABRACADABRA.
 
Mfumo wa malipo ya Kodi ya majengo bado uko vilevile sema imepanda mpka 12000 nenda ofisi za TRA zilizo karibu nawe. Marekebisho ya kodi hiyo bado hayajafanyika kwenye system ili kuweza kulipa kwa hiyo LUKU.
Unaanza rasmi kesho tarehe 20/8/2021.
 
Matajiri wajanja wametusukumizia kodi za majengo yao wanayowapangisha wageni tuzilipe sisi ambao hata bei ya tofali hatuijui.

Wajanja hawa kama wangekuwa na nia nzuri na sisi masikini wangeweka bima ya afya (NHIF) tuilipe kwenye mfumo wa LUKU, hii ingetuwezesha tusio na uwezo wa kulipa kwa mkupuo tuwe na bima.

Rais Samia wajanja wamekuzidi kete kwa hili, ondoa kodi ya jengo masikini kuwalipia matajiri weka masikini kujilipia Bima ya Afya kwa mfumo wa LUKU.
Ninahisi serikali inataka kufilisika.
 
Hilo wazo la bima ni zuri sana. Ila
Kwako ewe mnyonge, Ukiwa umepanga hilo jengo ni lako kwa muda huo uliopanga. Lilipie kodi tu.🤣
 
Matajiri wajanja wametusukumizia kodi za majengo yao wanayowapangisha wageni tuzilipe sisi ambao hata bei ya tofali hatuijui.

Wajanja hawa kama wangekuwa na nia nzuri na sisi masikini wangeweka bima ya afya (NHIF) tuilipe kwenye mfumo wa LUKU, hii ingetuwezesha tusio na uwezo wa kulipa kwa mkupuo tuwe na bima.

Rais Samia wajanja wamekuzidi kete kwa hili, ondoa kodi ya jengo masikini kuwalipia matajiri weka masikini kujilipia Bima ya Afya kwa mfumo wa LUKU.
Serikali ya ajabu sana hii na haina mwisho mzuri hata kama wakitumia dola na mamlaka ya kikatiba waliyo nayo, Mungu hadhihakiwi
 
Taarifa kwa umma

IMG_20210819_164726.jpg
 
Matajiri wajanja wametusukumizia kodi za majengo yao wanayowapangisha wageni tuzilipe sisi ambao hata bei ya tofali hatuijui.

Wajanja hawa kama wangekuwa na nia nzuri na sisi masikini wangeweka bima ya afya (NHIF) tuilipe kwenye mfumo wa LUKU, hii ingetuwezesha tusio na uwezo wa kulipa kwa mkupuo tuwe na bima.

Rais Samia wajanja wamekuzidi kete kwa hili, ondoa kodi ya jengo masikini kuwalipia matajiri weka masikini kujilipia Bima ya Afya kwa mfumo wa LUKU.
Kwa sasa maskini na wenye kipato cha chini, wasio na nyumba ndio wanalimia kwa meno kuzalisha na kuwalisha wenye kipato cha kati, kipato cha juu, wenye nyumba na matajiri na hakuna mtetezi tena wakitumia msemo 'kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe'!!!

Miswada inajadiliwa na wabunge kibinafsi, miswada inafichwa kwenye mitandao eti wakitafuta maoni lakini mwananchi wa kawaida ambaye hana uwezo wa kuingia huko na kuhoji au kuukataa kisha inapelekwa bungeni inapitishwa kuwa sheria mwananchi hajui lolote, rais anasaini bila kujiridhisha athari ya sheria husika, waziri anatunga kanuni, tangazo la serikali linatoa taarifa hizo ambapo gazeti hilo haliuzwi kama magazeti mengine ili mwananchi asome kisha muda uliotolewa unaisha na utekelezaji unawekwa wazi kwa umma kisha unazua mtafaruku usio wa lazima.

Kodi ya jengo ilipwe na mwenye nyumba mwenyewe sio mpangaji. Jengo sio mali ya mpangaji kwa hiyo sio sahihi kumtoza mpangaji kodi ya jengo. Utaratibu utasababisha wamiliki halali kuporwa nyumba zao na wapangaji wake. Wamiliki wa nyumba walazimishwe kutoa risiti pindi mpangaji anapolipa kodi na madalali wafutwe au walipe kodi nao pia. Huu uonevu haufai kwa wananchi; hakuna mwakilishi anayewasemea wala kuwatetea kwa sasa.

Ni bora Dr Slaa agombee nafasi kuu kabisa ya nchi hapo maonevu yatakomeshwa
 
Wakati inapitishwa na Bunge Mwigulu alisema kwa dharau kuwa anatuonea huruma watanzania kwa jinsi tutakavyowalipia mijengo yao badala ya wao! Alijua watanzania ni wanyonge hawawezi kulalamika.
 
Hii kodi wameiweka makusudi wakijua fika wapangaji ni wengi zaidi ya wenye nyumba, watavuna zaidi.
 
Mwenye nyumba anatakiwa akurudishie
Mwenyenyumba anirudishie withholding tax na kodi ya jengo! Huo ni utani, na kama nyumba ni ya serikali? Na Mwigulu na mawaziri wenzake na wote wale maelfu wanaolipiwa umeme na serikali?
 
Back
Top Bottom