Kimwakaleli
JF-Expert Member
- Apr 16, 2018
- 7,755
- 11,737
Kufuatana na kichwa hapo juu, nimeandika kwa wanajamii forums yaliyonikuta ili kupeana mawazo.
Nilikumbana na usumbufu sana kutoka kwenye wenye mamlaka kunishinikiza nimlipie mwanangu ada kwenye shule za kulipia!
Huyu mwanangu alikuwa akisoma shule ya kata hapa Dodoma, lakini mama yake na mtoto wa mama yake mkubwa walinipa taarifa ya kumhamisha kwenda shule ya kulipia huko Moshi, jambo ambalo sikulipinga kwani ada wanatoa wao.
Mwaka huu wa mwisho ndipo changamoto zikaanza. Ghafla naletewa barua za wito ofisi ya Mkuu wa Wilaya. Kwa ufupi lilikuwa shinikizo kwamba lazima nilipe ada nitake nisitake hata kwa kuwashinikiza wapangaji wangu wakope pia popote wanipe nilipe!