Wenye mitandao mnatukera na meseji zenu za matangazo

Wenye mitandao mnatukera na meseji zenu za matangazo

naunga hoja mkono hasa hawa eatel na namba yao hii +15656 kwa cku napokea sms karibu kumi wanakera sana!!!!!!!!!!!!!!!

Msg nyingine ni za kukushawishi kitapelitapeli ushiriki hayo makamari yao msg inaingia unafikiri kitu cha maana unakutana na huu upupu "namba 078.........(wanaandika namba yako) imepewa nafasi mbili kwa mpigo kushinda milioni 20 leo tuma KWANJUKA kwenda+15656" shit!! wengine hatuamini katika kamari.Aaaaaarrgh!! wanakera
 
Biashara matangazo.
Mzee ulikatishwa uhondo nini ukajua sms ya dili kumbe tangazo.

Mkuu Fidel wangekuwa wanafanya hivi kama kweli ni lazima tuyapate hayo matangazo....

Ni heri kama wangeacha matangazo yabaki kuonekana unapouliza salio & kwenye cell Info Display yapokezane na taarifa za minara maana ukiyachoka unaswitch off, huyaoni tena kuliko sasa. Na matangazo haya naamini hayamo katika Vigezo na Masharti (Terms and Conditions).
 
Mkuu ninasoma thread yako, nanyanyua simu yangu nakutana na hili eti "ZAWADI YA KUAMINIKA KUTOKA AIRTEL, KWA AJILI YAKO TU uloanza MAPEMA! TUMA MUAMINIFU-15656" Hata sikukumbuki kama niliwahi anza mapema hii kamari,
 
Wanaboa sana, yaani hadi usiku! unaweza kushtuka ukadhani ni ujumbe unaohitaji msaada kumbe ni tangazo!!!!
 
Hawa jamaa bado wanatuma tuu,na simu wanapiga.Kero aah.
 
Mimi niliamua kuweka TTCL Land line kwa ajili ya emergency za usiku, So siku hizi nazima simu yangu usiku ku-avoid disturbunces zao. I hope they will stop this!!! really mnatupa mauzi usiku!! Hao Vodacom na sms zao za kudownload nyimbo! usiku wa manane!! akhhhhhhhh inakera, mara M-pesa......
 
You are right,unajua kuzima nako mtu unaona labda kuna issue yaweza tokea ya maana ndo maana tumezoea kuacha on.Matokeo ndo hayo.KERO.
 
Wanasema ukipenda ua penda na boga. Kwa hiyo hayo matangazo yao wayafanyie wapi ? Any way kuna baadhi wachache ni kero lakini mlio wengi shukuruni hata hizo meseji kwan simu zenu kuanzia wiki hadi mwezi zipo kimya khaaa !!!
 
Imekuwa too much....
 
Hawa jamaa bado wanatuma tuu,na simu wanapiga.Kero aah.
Ukitaka kusitisha hii aina ya matangazo tuma neno "STOP" au "ONDOA" kwenda kwenye namba ya tangazo lenyewe. Mfano, kama ni airtel namba yao mara nyingi ni +15656
 
Ukitaka kusitisha hii aina ya matangazo tuma neno "STOP" au "ONDOA" kwenda kwenye namba ya tangazo lenyewe. Mfano, kama ni airtel namba yao mara nyingi ni +15656
Kwa njia hiyo utaandika mpaka ukome na haitoki japo ujumbe unakwambia wameshatoa.Yalishanikuta.
 
Japo biashara ni matangazo,zipunguzeni.KERO SANA.
 
Aisee hakuna kitu kinaudhi kama yale matangazo wanayoweka kabla ya simu kuita au kama haipatikani au kama inatumika, ni bora wakakwambia kama hiyo namba haipatikani then ndo waweke matangazo kama unapenda ndo usikilize! Sijui TCRA wanalichukuliaje hili?
 
TCRA hawana meno,wanajali mshiko tu.
 
Kero kero,japo biashara matangazo,imezidi..!!
 
Na huu ujio wa tiGO-pesa,m-pesa na zapp etc,kila siku unakuta mtandao uko down.
 
Nimepata sasa hivi toka TIGOPESA nikaanza kupata mawazo kibao nani kanitumia pesa! Maana tarehe ngumu hizi, kufungua niicheki, pambafu kabisa nakuta upupu, eti nikajiandikishe......hata sijamalizia kuisoma nikaishia kuifuta! Yaani sina pesa halafu mtu anakutumia li sms lakijinga
 
Wanatumia vibaya matangazo yao,kero.
 
Back
Top Bottom