Wenye mitandao mnatukera na meseji zenu za matangazo

Wenye mitandao mnatukera na meseji zenu za matangazo

Tena kama hawa TIGO hawaaa mfyuuuuu, wananikera sana. Yaani kuna wakati nasubiria sms ya pesa halafu ninaona sms ya TIGO pesa, ukifungua nakutana na meseji yao: Hamisha......
mfyuuuuuu. halafu nilishawahi kuuuliza hivi wenyewe huwa hawana a/c hapa JF kama walivyo TANESCO, NMB, DAWASCO na wengineo?
 
We acha tu mkuu....
 
Na zile za waganga sijui zinafikaje aisee,japo nambà sio za mtandao
 
Hahahha

Pole

Siju iz wanakupigia na kukushawishi ujiunge na 4g au kuelezwa ofa za vifurushi dstv

yeesuu siku moja nilikuwa kwenye kipindi kigumu stranded somewhere halafu nasubiria muamala kisha simu haina chaji iliyobaki inaleta kelele kuwa itazima muda wowote halafu simu ikaita kisha aghrrrrrrrrrrrr kupokea nasikia mitangazo maninarrr nilipiga simu ukutani mpaka ikaharibika mfuniko wa nyuma dadeeek hihihi yaani wapuuz kweli

instead wangekuwa wanatutangazia mambo muhimu kama umeme utakatika maji yatakatika nk nk nk
 
Jamani wenye mitandao mmezidi kuturundikia SMS za matangazo na promosheni zenu zisizokoma mpaka usiku wa manane.Yaani kwa siku unaweza kupokea SMSs kama 5+, kwa maana hiyo ukiwa na SIM card nyingi ndio unaongeza kero.

Watumiaji tunahitaji kuwasiliana ili kufanikisha shughuli zetu za kila siku siyo bughudha za ku-persuade adverts ambazo zingine ni usaniii tu aka wizi.

TUPUNGUZIENI KERO.
Kwa kweli Hawa watu ni kero. TCRA ilipiga marufuku hizi msg na zile zilizokuwa zinaanza kwenye miito ya Simu. Tatizo nadhani hawafuatilii. Kuna haha ya ku-file complaints dhidi ya hawa watu. Wanaogopa kuweka mabango ya matangazo, wanageuza Simu zetu kuwa mabango yao.
 
Nakereka sana na hizi meseji zenu kila baada ya dakika mnatuma kiukweli ingekuwa inawezekana kusajili line nyingine ningefanya hivyo na kuepukana na hizi kero.

Kila baada ya dakika 15 mnatuma meseji zenu kwa kutumia namba 15670 au 15671.

Acheni huu utaratibu; mnakera sana. Ingekuwa inaruhusiwa kusajili line nyingine ningefanya hivyo kuepuka hizi kero. Mbona wenzenu Halotel hawana huu usumbufu?

Mnaweza tuma meseji moja tu ya matangazo kwa siku, sio mbaya. Lakini nyie kila dakika 15 meseji mnatuma kwa 24 hours.

Badilikeni, mnaboa. Mwambieni huyo aliyeshauri huu mpango kuna baadhi ya wateja unatukera.

IMG_20200630_005006[1].JPG
 
Sasa kama kumbe nia yako ni Kuufagilia Mtandao wa Halotel japo hapa umeandika Halitel kwa Gharama za Kuuchafua Kimkakati Mtandao wa Tigo kwanini umepita njia ndefu sana Ndugu badala ya kwenda moja kwa moja tu? Na je, hao Halitel ( Halotel ) wako wameshakuhakikishia kuwa endapo ukijiunga tu huko Kwao basi hizi Karaha na Kero unazozipata huku Tigo zitakuwa Historia? Kwani Tigo walikulazimisha uwe Mteja Wao?
 
Kusema ukweli hicho kitu kinanikera Cha kutuma sms Kila baada ya dakika chache. Unaweza kukuta kwa siku umetumiwa SMS nyingi mpaka unashindwa kuzisoma. Tigo nawaomba mbadilike mnatukera wateja wenu.
 
Nakereka sana na hizi meseji zenu kila baada ya dakika mnatuma kiukweli ingekuwa inawezekana kusajili line nyingine ningefanya hivyo na kuepukana na hizi kero.

Kila baada ya dakika 15 mnatuma meseji zenu kwa kutumia namba 15670 au 15671.

Acheni huu utaratibu; mnakera sana. Ingekuwa inaruhusiwa kusajili line nyingine ningefanya hivyo kuepuka hizi kero. Mbona wenzenu Halotel hawana huu usumbufu?

Mnaweza tuma meseji moja tu ya matangazo kwa siku, sio mbaya. Lakini nyie kila dakika 15 meseji mnatuma kwa 24 hours.

Badilikeni, mnaboa. Mwambieni huyo aliyeshauri huu mpango kuna baadhi ya wateja unatukera.

View attachment 1492832
Pole. Ila ni nani huyo kakuzuia usihamie mtandao mwingine?
 
Soka wezi na wasimbufu... Sijui kwa mm tcra Wana waangalia na hawachukui hatua yyte... Inawezekana mapato ya hiyo soka wanakula na maafisa wa tcra..
 
Hili suala mm nilishawapigia tigo na kuwaeleza kusudia langu la kuwapeleka mahakamani naona bado hawajakoma tu
 
... kwanini hao tigo na mitandao mingine wasiweke option kama mteja hataki kupokea mameseji yao awe na uwezo wa ku-block number zinazotuma such messages.
 
Mimi nime block ya soka... leo nina siku 5 sijaziona maana ilikuwa too much
 
Back
Top Bottom