MWENDAKULIMA
JF-Expert Member
- Jul 17, 2009
- 951
- 355
naunga hoja mkono hasa hawa eatel na namba yao hii +15656 kwa cku napokea sms karibu kumi wanakera sana!!!!!!!!!!!!!!!
Biashara matangazo.
Mzee ulikatishwa uhondo nini ukajua sms ya dili kumbe tangazo.
Ni heri kama wangeacha matangazo yabaki kuonekana unapouliza salio & kwenye cell Info Display yapokezane na taarifa za minara maana ukiyachoka unaswitch off, huyaoni tena kuliko sasa. Na matangazo haya naamini hayamo katika Vigezo na Masharti (Terms and Conditions).
You are right,unajua kuzima nako mtu unaona labda kuna issue yaweza tokea ya maana ndo maana tumezoea kuacha on.Matokeo ndo hayo.KERO.Mimi niliamua kuweka TTCL Land line kwa ajili ya emergency za usiku, So siku hizi nazima simu yangu usiku ku-avoid disturbunces zao. I hope they will stop this!!! really mnatupa mauzi usiku!! Hao Vodacom na sms zao za kudownload nyimbo! usiku wa manane!! akhhhhhhhh inakera, mara M-pesa......
Imekuwa too much....Wanasema ukipenda ua penda na boga. Kwa hiyo hayo matangazo yao wayafanyie wapi ? Any way kuna baadhi wachache ni kero lakini mlio wengi shukuruni hata hizo meseji kwan simu zenu kuanzia wiki hadi mwezi zipo kimya khaaa !!!
Ukitaka kusitisha hii aina ya matangazo tuma neno "STOP" au "ONDOA" kwenda kwenye namba ya tangazo lenyewe. Mfano, kama ni airtel namba yao mara nyingi ni +15656Hawa jamaa bado wanatuma tuu,na simu wanapiga.Kero aah.
Kwa njia hiyo utaandika mpaka ukome na haitoki japo ujumbe unakwambia wameshatoa.Yalishanikuta.Ukitaka kusitisha hii aina ya matangazo tuma neno "STOP" au "ONDOA" kwenda kwenye namba ya tangazo lenyewe. Mfano, kama ni airtel namba yao mara nyingi ni +15656
TCRA hawana meno,wanajali mshiko tu.Aisee hakuna kitu kinaudhi kama yale matangazo wanayoweka kabla ya simu kuita au kama haipatikani au kama inatumika, ni bora wakakwambia kama hiyo namba haipatikani then ndo waweke matangazo kama unapenda ndo usikilize! Sijui TCRA wanalichukuliaje hili?
Wanatumia vibaya matangazo yao,kero.Nimepata sasa hivi toka TIGOPESA nikaanza kupata mawazo kibao nani kanitumia pesa! Maana tarehe ngumu hizi, kufungua niicheki, pambafu kabisa nakuta upupu, eti nikajiandikishe......hata sijamalizia kuisoma nikaishia kuifuta! Yaani sina pesa halafu mtu anakutumia li sms lakijinga