Wenye Nyumba kaeni kitaalamu: Kama mpangaji wako atakutwa na dawa za kulevya nyumba yako itataifishwa!

Na mabasi ya abiria,treni na ndege zitaifishwe pia zitakazo beba abria wenye madawa ya kulevya,
 
kwani mkuu mtu anaweza kuwa na kazi moja ya kumuingizia kipato mtu anaweza kuwa na biashara tatu lakini akakutajia moja tu..unajua kuna biashara hazionekani kwenye macho ya wengi lakini zinalipa pesa ndefu
 
Ni mambo ya ajabu sana haya, kweli hilo ndio suluhisho la kupambana na dawa za kulevya?

Mfano nina nyumba chanika,boko,kimara, kinondoni, mbezi beach na ubungo, hapo mimi kama mwenye nyumba nitazilinda vipi na watu haujui wanaingia na nini kila siku kwenye hizo nyumba?

Kweli kabisa wao wanaona hii ni rahisi kwa raia wa mtaani tuu kuweza kubaini madawa kirahisi namna hii?

Kama umempata muhusika na dawa zake iweje utaifishe nyumba kitu ambacho hakijahusika na usafirishaji wa dawa hizo?

Kosa la nyumba ni kuhifadhi na si mtu aliyezibeba kutoka huko zilikotoka?


Vipi watu wakifanya hujuma za kutaka nyumba za watu mtawazuia kwa namna ipi?

Ndugu Kamishna tunaomba hili mlitazame kwa undani na mje na plan nyingine ya kudhibiti madawa na si hili la kutaifisha nyumba za watu, nyumba hazina makosa makosa yapo kwa wabebaji, taifisheni vyombo vya usafiri ingawa sijawai kusikia ndege ikitaifishwa kwa kumbeba mtu mwenye madawa ya kulevya.
 
Biashara ya nyumba za kupanga, ni changamoto kwa baadhi ya maeneo na kwa baadhi ya wapangaji wasio waaminifu coz anaweza fanya tukio huko au nyumba yako ikahifadhiwa vitu vibaya kama hilo angalizo.
 

Hivi DCEA hawamo humu waje watujibu maswali yetu?

Sheria hii itawaumiza wengi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…