Wenye Nyumba kaeni kitaalamu: Kama mpangaji wako atakutwa na dawa za kulevya nyumba yako itataifishwa!

Wenye Nyumba kaeni kitaalamu: Kama mpangaji wako atakutwa na dawa za kulevya nyumba yako itataifishwa!

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Kama una nyumba sehemu kaa kwa chonjo kuna habari mpya huku kutoka DCEA.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amewahimiza wamiliki wa nyumba za kupangisha kuwa waangalifu na wapangaji wao.

Alieleza kuwa baadhi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya wamekuwa wakitumia nyumba walizopanga kama maghala ya kuhifadhi dawa hizo, huku wao wakiishi sehemu nyingine.

madawa ya kulevya.png

Soma pia: Makonda: Ukichagua viongozi wa mtaa waaminifu wasiyojihusisha na madawa ya kulevya utaleta chachu katika ngazi hiyo

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Novemba 25, 2024, jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali Lyimo alisisitiza kuwa kwa mujibu wa sheria, mali yoyote, kama nyumba au gari, ikikutwa na dawa za kulevya, itataifishwa.

Kamishna huyo amewataka wamiliki wa mali hizo kuhakikisha wanachukua tahadhari na kusimamia vyema mali zao ili kuepuka hasara na kuhusishwa na vitendo haramu.

Source: Wasafi FM

My take:
Mbona kama kuna watu specific wanatafutwa kwa tochi kupitia agizo hili?

1. Mimi kama mwenye nyumba ntajuaje kama mtu anaweka madawa ya kulevya ndani ya nyumba? Niweke CCTV au niwe nafanya doria za kushtukiza?

2. Hiyo nyumba ikishataifishwa inapelekwa kwa nani au taasisi gani?

3. Kama inaenda kwa serikali hamuoni kwamba kuna baadhi ya vigogo serikalini wanaweza wakatumia mwanya huo kupora nyumba za watu iwapo watazipenda?

4. Huo utaratibu wenu wa kutaifisha nyumba ni watanzania pekee au ni utratibu wa kimataifa? Ni mataifa gani yana utaratibu kama huo?

5. Hiyo sheria ya kutaifisha nyumba ambayo sio ya mtuhumiwa ipo kwenye ibara gani kwenye Katiba yru ya inchi?
 
SHERIA ya hovyo kabisa hii... Likikamatwa gari la Serikali inakuwaje!?? Kama zilivyokamatwa ambulances na macruiser ya serikali!? Zikikamatwa kwenye quarters za Serikali!?

Ama kwenye maghorofa ya shirikabla nyumbal la Taifa?

Mpangaji akipangishwa nyumba mwenye nyumba ana uhuru gani wa kukagua nyumba kila siku?

Huyu Lyimo atakuwa ni mchaga mjinga wa kwanza.
 
Wakuu,

Kama una nyumba sehemu kaa kwa chonjo kuna habari mpya huku kutoka DCEA.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amewahimiza wamiliki wa nyumba za kupangisha kuwa waangalifu na wapangaji wao...
Nilichogundua kuweka vipengele muhimu kwenye mkataba wako wa upangishaji,ambavyo viwe na masharti yatakayokuepusha na iyo kadhia ikitokea
 
SHERIA ya hovyo kabisa hii... Likikamatwa gari la Serikali inakuwaje!?? Kama zilivyokamatwa ambulances na macruiser ya serikali!? Zikikamatwa kwenye quarters za Serikali!?? Ama kwenye maghorofa ya shirikabla nyumbal la Taifa !??
Mpangaji akipangishwa nyumba mwenye nyumba ana uhuru gani wa kukagua nyumba kila siku!!? Huyu Lyimo atakuwa ni mchaga mjinga wa kwanza.
Hakika
 
Hapo deal ni kuweka hicho kipengele kwenye Mkataba wakati wa kumpangisha mtu.

Mimi niliwahi kuweka kipengele cha kumtaka Mpangaji kueleza kazi ama shughuli aifanyayo kuendesha maisha yake

Hii ilisaidia kutowapangisha watu Wasumbufu kulipa Kodi

Hopefully na hicho kipengele kikiwepo kwenye Mkataba wa kupangisha, kitasaidia kumlinda mwenye nyumba
 
Back
Top Bottom