Wenye Nyumba kaeni kitaalamu: Kama mpangaji wako atakutwa na dawa za kulevya nyumba yako itataifishwa!

kwani mkuu mtu anaweza kuwa na kazi moja ya kumuingizia kipato mtu anaweza kuwa na biashara tatu lakini akakutajia moja tu..unajua kuna biashara hazionekani kwenye macho ya wengi lakini zinalipa pesa ndefu
Ni kweli usemacho, lakini pale kwenye Mkataba atasema kazi yake Moja halali

Kwahiyo akikamatwa na ishue ya madawa itakuwa ni suala lake binafsi kwahiyo nyumba yako haiwezi kuwa kwenye risk ya kutaifishwa
 
Wakuu,

Kama una nyumba sehemu kaa kwa chonjo kuna habari mpya huku kutoka DCEA.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amewahimiza wamiliki wa nyumba za kupangisha kuwa waangalifu na wapangaji wao.

Alieleza kuwa baadhi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya wamekuwa wakitumia nyumba walizopanga kama maghala ya kuhifadhi dawa hizo, huku wao wakiishi sehemu nyingine.

Soma pia: Makonda: Ukichagua viongozi wa mtaa waaminifu wasiyojihusisha na madawa ya kulevya utaleta chachu katika ngazi hiyo

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Novemba 25, 2024, jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali Lyimo alisisitiza kuwa kwa mujibu wa sheria, mali yoyote, kama nyumba au gari, ikikutwa na dawa za kulevya, itataifishwa.

Kamishna huyo amewataka wamiliki wa mali hizo kuhakikisha wanachukua tahadhari na kusimamia vyema mali zao ili kuepuka hasara na kuhusishwa na vitendo haramu.

Source: Wasafi FM

My take:
Mbona kama kuna watu specific wanatafutwa kwa tochi kupitia agizo hili?

1. Mimi kama mwenye nyumba ntajuaje kama mtu anaweka madawa ya kulevya ndani ya nyumba? Niweke CCTV au niwe nafanya doria za kushtukiza?

2. Hiyo nyumba ikishataifishwa inapelekwa kwa nani au taasisi gani?

3. Kama inaenda kwa serikali hamuoni kwamba kuna baadhi ya vigogo serikalini wanaweza wakatumia mwanya huo kupora nyumba za watu iwapo watazipenda?

4. Huo utaratibu wenu wa kutaifisha nyumba ni watanzania pekee au ni utratibu wa kimataifa? Ni mataifa gani yana utaratibu kama huo?

5. Hiyo sheria ya kutaifisha nyumba ambayo sio ya mtuhumiwa ipo kwenye ibara gani kwenye Katiba yru ya inchi?
Hii sheria imepitishwa na watanzania wenye akili timamu kabisa wenye bachekor degree kabisa ya miaka mitatu/minne?
 
Hapo deal ni kuweka hicho kipengele kwenye Mkataba wakati wa kumpangisha mtu.

Mimi niliwahi kuweka kipengele cha kumtaka Mpangaji kueleza kazi ama shughuli aifanyayo kuendesha maisha yake

Hii ilisaidia kutowapangisha watu Wasumbufu kulipa Kodi

Hopefully na hicho kipengele kikiwepo kwenye Mkataba wa kupangisha, kitasaidia kumlinda mwenye nyumba
Umeweka kipengele mpangaji ameona na amesaini
Then anakutwa na Unga
Kipengele kitasaidia nini?
Mimi nadhani hii kitu kuna mtu anatafutwa na asipokuwa makini ataingia kwenye mfumo
 
Nyumba zangu za kupangisha Kuna kupengele Mali ya mpangaji ni yake haisiani na mwenye nyumba hata ulinzi WA Mali zake ni juu ya mpangaji mwenyewe,Sheria ya Lyimo inakinzana na masharti ya wapangaji wangu
daah! lakini mkuu sheria zako binafsi na wapangaji wako haziwezi kuwa juu ya sheria za kitaifa za wenye mamlaka walioshika mpini si unajua mfumo wa hii nchi unavyotenda kazi zake itabidi uwe mpole tu..
 
Umeweka kipengele mpangaji ameona na amesaini
Then anakutwa na Unga
Kipengele kitasaidia nini?
Mimi nadhani hii kitu kuna mtu anatafutwa na asipokuwa makini ataingia kwenye mfumo
Hicho kipengele kitamlinda mwenye nyumba, kwamaana hatowajibishwa Kwa makosa yasiyo yake
 
Wakuu,

Kama una nyumba sehemu kaa kwa chonjo kuna habari mpya huku kutoka DCEA.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amewahimiza wamiliki wa nyumba za kupangisha kuwa waangalifu na wapangaji wao.

Alieleza kuwa baadhi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya wamekuwa wakitumia nyumba walizopanga kama maghala ya kuhifadhi dawa hizo, huku wao wakiishi sehemu nyingine.

Soma pia: Makonda: Ukichagua viongozi wa mtaa waaminifu wasiyojihusisha na madawa ya kulevya utaleta chachu katika ngazi hiyo

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Novemba 25, 2024, jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali Lyimo alisisitiza kuwa kwa mujibu wa sheria, mali yoyote, kama nyumba au gari, ikikutwa na dawa za kulevya, itataifishwa.

Kamishna huyo amewataka wamiliki wa mali hizo kuhakikisha wanachukua tahadhari na kusimamia vyema mali zao ili kuepuka hasara na kuhusishwa na vitendo haramu.

Source: Wasafi FM

My take:
Mbona kama kuna watu specific wanatafutwa kwa tochi kupitia agizo hili?

1. Mimi kama mwenye nyumba ntajuaje kama mtu anaweka madawa ya kulevya ndani ya nyumba? Niweke CCTV au niwe nafanya doria za kushtukiza?

2. Hiyo nyumba ikishataifishwa inapelekwa kwa nani au taasisi gani?

3. Kama inaenda kwa serikali hamuoni kwamba kuna baadhi ya vigogo serikalini wanaweza wakatumia mwanya huo kupora nyumba za watu iwapo watazipenda?

4. Huo utaratibu wenu wa kutaifisha nyumba ni watanzania pekee au ni utratibu wa kimataifa? Ni mataifa gani yana utaratibu kama huo?

5. Hiyo sheria ya kutaifisha nyumba ambayo sio ya mtuhumiwa ipo kwenye ibara gani kwenye Katiba yru ya inchi?
Hata kama ya msikiti au kanisa?
 
Na mabasi ya abiria,treni na ndege zitaifishwe pia zitakazo beba abria wenye madawa ya kulevya,

Wamejilinda kwa maandishi madogo yenye kanuni, sheria na masharti.

Hivyo wenye nyumba mikataba iwe na kanuni, masharti na vigezo katika maandishi ili kujikinga na usumbufu au utapeli.
 
Back
Top Bottom