Wenye Nyumba kaeni kitaalamu: Kama mpangaji wako atakutwa na dawa za kulevya nyumba yako itataifishwa!

Wenye Nyumba kaeni kitaalamu: Kama mpangaji wako atakutwa na dawa za kulevya nyumba yako itataifishwa!

Wakuu,

Kama una nyumba sehemu kaa kwa chonjo kuna habari mpya huku kutoka DCEA.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amewahimiza wamiliki wa nyumba za kupangisha kuwa waangalifu na wapangaji wao...
Huo sasa ni uhuni kwa hiyo hata apartment mpagaji mmoja akikutwa na madawq ya kulevya apartment nzima itataifishwa?

Nani mwenye uwezo wa kujuwa mpagaji anafanya nini nyumbani kwake masaa 24? Tukisema siasa ni maisha muwe mnaelewa.
 
Kwa hiyo hii ni kauri ya mwisho kabisa baada ya kuwashindwa wauza Ngada ama nini?kwa hiyo wakikuta kwenye Nyumba za Serikali mzigo utakuwa wa nani au itapigwa Mnada na pesa tupewe Wananchi?
 
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema imebaini kuwa Wahusika wa biashara haramu ya dawa za kulevya hutumia mbinu ya kupanga nyumba ambazo zinageuzwa kuwa maghala ya kuhifadhia dawa za kulevya, huku wao wakishi katika maeneo mengine.

Akiongea Jijini Dar es salaam leo November 25,2024, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amesema “Mamlaka inatoa rai kwa Wamiliki wa nyumba kuwa makini wanapopangisha nyumba zao, kwani nyumba inayotumika kwa shuguli za dawa za kulevya ni kinyume cha sheria na inaweza kutaifishwa”

“Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Sura ya 95, imeweka katazo kwa Mmiliki au Msimamizi wa nyumba, Msimamizi wa eneo au chombo cha usafirishaji kuruhusu vitumike wa lengo la kutengeneza, kuvuta, kujidunga, kuuza au kununua dawa za kulevya”

“Mmiliki anapojua kuwa kosa linatendeka kwenye eneo lake, anajukumu la kutoa taarifa kwa Mamlaka, kushindwa kufanya hivyo ni kosa la jinai, na akitiwa hatiani, adhabu yake inaweza kuwa faini kuanzia shilingi milioni tano hadi milioni hamsini, au kifungo cha miaka mitano hadi miaka thelathini jela, au vyote kwa pamoja”


20241125_164350.jpg
 
“Kuruhusu vitumike ndo kosa, sasa Kama kwenye mkataba kutakuwa na kipengele cha mpangishwa Kama atahifadhi Madawa ya kulevya hapo sawa”
 
Hata kama bongo ni nyoso

Hana uwezo wa kulopoka upupu kama huu...

Kwanza kisheria hakuna hio sheria, huu upupu katoa kichwani kwake.

Lakini muuza unga mwenye kumiliki mali zinazo hisiwa zilipatika kutokana na hio bishara ndio anaweza

kutaifishwa mali zake ikiwemo nyumba kama viko kwenye hati ya jina lake tu, na kama si jina lake pia hawawezi.
Hata mahakama zetu ni za kijinga, lakini huu upupu hauwezi simama kisheria.
 
Kuna watu wamelengwa hapa, Wananchi wana shida kibao bado mtu analeta sheria za kipumbavu.
Kwa hiyo Mimi mwenye nyumba nigeuke kuwa TISS wa mpangaji au.
Period
 
Siyo rahisi kiasi hivyo, it's very dangerous kuapply hiyo kitu, ni lazima itakuja kukutokea puani.
 
Wauza unga wakubwa Ni CCM.
Umemaliza kaka, kuna bodygurd wa Ex PM. Huyo alikuwa akipita nazo na kuweka kwenye jumba huko (x) hiyo nyumba kazi yake ni hiyo tu. Wangeanza na hao na wanajuana wote.

Kuna msanii, rafiki yake alidakwa na dawa, yuko ndani. Yeye sasa anaendeleza. Hao wote wanashabikia ccm, huoni wakibughudhiwa. Kama mtoa mada anavyosema, kuna mtu anatafutwa na nyumba zake.
 
Wakuu,

Kama una nyumba sehemu kaa kwa chonjo kuna habari mpya huku kutoka DCEA.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amewahimiza wamiliki wa nyumba za kupangisha kuwa waangalifu na wapangaji wao.

Alieleza kuwa baadhi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya wamekuwa wakitumia nyumba walizopanga kama maghala ya kuhifadhi dawa hizo, huku wao wakiishi sehemu nyingine.


Soma pia: Makonda: Ukichagua viongozi wa mtaa waaminifu wasiyojihusisha na madawa ya kulevya utaleta chachu katika ngazi hiyo

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Novemba 25, 2024, jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali Lyimo alisisitiza kuwa kwa mujibu wa sheria, mali yoyote, kama nyumba au gari, ikikutwa na dawa za kulevya, itataifishwa.

Kamishna huyo amewataka wamiliki wa mali hizo kuhakikisha wanachukua tahadhari na kusimamia vyema mali zao ili kuepuka hasara na kuhusishwa na vitendo haramu.

Source: Wasafi FM

My take:
Mbona kama kuna watu specific wanatafutwa kwa tochi kupitia agizo hili?

1. Mimi kama mwenye nyumba ntajuaje kama mtu anaweka madawa ya kulevya ndani ya nyumba? Niweke CCTV au niwe nafanya doria za kushtukiza?

2. Hiyo nyumba ikishataifishwa inapelekwa kwa nani au taasisi gani?

3. Kama inaenda kwa serikali hamuoni kwamba kuna baadhi ya vigogo serikalini wanaweza wakatumia mwanya huo kupora nyumba za watu iwapo watazipenda?

4. Huo utaratibu wenu wa kutaifisha nyumba ni watanzania pekee au ni utratibu wa kimataifa? Ni mataifa gani yana utaratibu kama huo?

5. Hiyo sheria ya kutaifisha nyumba ambayo sio ya mtuhumiwa ipo kwenye ibara gani kwenye Katiba yru ya inchi?
Kwa waxo hili bibi atapewa Tena PhD na chuo Kikuu cha Tumaini sasa.
 
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema imebaini kuwa Wahusika wa biashara haramu ya dawa za kulevya hutumia mbinu ya kupanga nyumba ambazo zinageuzwa kuwa maghala ya kuhifadhia dawa za kulevya, huku wao wakishi katika maeneo mengine.


Akiongea Jijini Dar es salaam leo November 25,2024, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amesema "Mamlaka inatoa rai kwa Wamiliki wa nyumba kuwa makini wanapopangisha nyumba zao, kwani nyumba inayotumika kwa shuguli za dawa za kulevya ni kinyume cha sheria na inaweza kutaifishwa"


"Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za


Kulevya, Sura ya 95, imeweka katazo kwa Mmiliki au Msimamizi wa nyumba, Msimamizi wa eneo au chombo cha usafirishaji kuruhusu vitumike wa lengo la kutengeneza, kuvuta, kujidunga, kuuza au kununua dawa za kulevya"


"Mmiliki anapojua kuwa kosa linatendeka kwenye eneo lake, anajukumu la kutoa taarifa kwa Mamlaka, kushindwa kufanya hivyo ni kosa la jinai, na akitiwa hatiani, adhabu yake inaweza kuwa faini kuanzia shilingi milioni tano hadi milioni hamsini, au kifungo cha miaka mitano hadi miaka thelathini jela, au vyote kwa pamoja"

Ni sawa, inakuaje kwa mmiliki ambaye hayupo na hajui kuwa mpangaji wake ni muuza madawa, hajui kama mtu anajidunga au amekufa kwa matumizi ya madawa na kutupwa au kufia hapo akiwa sio mkazi wa wa nyumba hiyo na taarifa hana juu ya hayo but mainly n hilo la madawa kukutwa ndani madawa kwenye nyumba ya mmiliki?

Kama sheria hiyo inasema hivyo ina maana mnajua nani anahifadhi hayo nyumbani, ni kama mnahabarisha atoe apoteze ushahidi, hii doesn't make sense at all, DCEA kama imeamua kufanya kazi ifanye sio kuleta hizi habari. Mtusaidie wahalifu hawa wakikamatwa watajwe majina ili wananchi tujue nani hafai kuwa kioo kwa jamii na anyooshewe kidole.

Its me,
Concern Citizen 😁
 
Acha kupotosha, umeleta habari nusu kwa makusudi. Ameeleza kwamba ni endapo mwenyenyumba alikuwa anafahamu na hakuripoti.., sasa hapo utaprobe vipi mwenye nyumba alikuwa anafahamu?
hapo sasa labda mwenye nyumba nae awe anaishi humo pamoja na wapangaji wake na sheria hii inafaa sana kwa zile nyumba za kupanga chumba kimoja kimoja huku mitaani..ila zile full zenye fensi na mageti hiyo ukishapangisha hauna mamlaka nayo tena mpaka mwisho wa mkataba maana ni ngumu kumbana uliyempangisha ..ila wafanya maamuzi wa nchi hii wanasikitisha sana
 
Umemaliza kaka, kuna bodygurd wa Ex PM. Huyo alikuwa akipita nazo na kuweka kwenye jumba huko (x) hiyo nyumba kazi yake ni hiyo tu. Wangeanza na hao na wanajuana wote.

Kuna msanii, rafiki yake alidakwa na dawa, yuko ndani. Yeye sasa anaendeleza. Hao wote wanashabikia ccm, huoni wakibughudhiwa. Kama mtoa mada anavyosema, kuna mtu anatafutwa na nyumba zake.

Huwa nashangaa jambo moja tu, Jeshi la polisi na DCEA kwa nini huwa wanaanza mbali ikiwa jambo lina mtu mzito ndani yake.

Kama wahalifu wengine kwanini wasitajwe Mfano Bw Mzito X kakutwa na madawa kiasi kadhaa bila kumuonea mtu aibu maana wanasimamia sheria, maajabu ni kwamba mpaka wazunguke na chai vitafunwa asubuhi for what sake, tingisha mtu kama mbwai mbwai tu vyeo vipo tuu, kwani wazito hao hawajui kuwa ni uhalifu but hela serikali tamu bana 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom