ommytk
JF-Expert Member
- Jul 30, 2015
- 520
- 1,143
Kuna changamoto kwa sasa tunapitia watu kupandisha bei ya vitu kwa taarifa kuwa mafuta yamepanda bei sababu ikiwa vita vya Ukraine, sawa tunakubali ila kuna kama wengine wanafata mkumbo tu, maana jana mwenye nyumba wetu katuambia kodi mwezi ujao itapanda sababu ikiwa gharama za maisha kupanda sasa nyumba ushajenga kuna gharama gani zingine zimepanda naona hii hali ya Ukraine kuna watu wanaotumia kama nafasi kutudhulumu wanyonge.