Wenye pikipiki wateka mamia Nigeria

Wenye pikipiki wateka mamia Nigeria

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Leo tena tumepata kali ya kufungia mwaka huko Katsina jimbo alilozaliwa raisi wa sasa wa Nigaria mheshimiwa Muhammad Buhari ambaye kwa sasa yuko mapumzikoni jimboni kwao.

Inadaiwa watu waliopanda piki piki waliivamia shule ya mchepua wa Sayansi na kufyatua bunduki hewani halafu wakaondoka na zaidi ya wanafunzi 800 ambao mpaka sasa jeshi halijafanikiwa kuwapata wote .

Jeshi la nchi hiyo baada ya kupata taarifa hizo lilifika eneo la tukio na kufanya upekuzi kwenye msitu ulio karibu na shule hiyo pamoja na kushambuliana na watekaji hao.

Bado jeshi halijatoa taarifa rasmi.Hata hivyo maafisa wa serikali wa eneo hilo wamesema hakuna taarifa ya kujeruhiwa hata mwanafunzi mmoja.

Majirani wa shule hiyo wanasema walisikia milio ya bunduki usiku wa manane ambapo walinzi wa shule hiyo walifanikiwa kuwarudisha watekaji hao kabla ya jeshi la Polisi kufika.Majirani wengine wanasema walishuhudia watu hao wenye silaha wakiondoka na wanafunzi waliowateka.
1607857994746.png
 
Dah!..mbona hatujaona kampeni ya 'bring back our boys' ? Au kwasababu ni wavulana basi watajipambania?

...anyway serikali ya Nigeria ni dhaifu kwenye upande wa usalama.

Si wangeanza huo wakati wanapandishwa pikipiki lakini Lo umma wote huo wakapandiswa piki piki wakajiunga kwenye msafara kuingia msituni na inaonekana hakuna hata pikipiki moja iliyopata pancha.

Na bahati iliyoje watu wa Katsina hawakuweza kushika hata picha moja ya msafara wa pikipiki 800.

Shule nzima walitekwa hakukuwa na hata mmoja aliyebaki nyuma kibahati bahati kwa sababu yoyore ile hata ugonjwa au wakati wa utekaji alikuwa yuko chooni akijisaidia

Angesaidia polisi kuwatambua watekaji.
 
Si wangeanza huo wakati wanapandishwa pikipiki lakini Lo umma wote huo wakapandiswa piki piki wakajiunga kwenye msafara kuingia msituni na inaonekana hakuna hata pikipiki moja iliyopata pancha.Na bahati iliyoje watu wa Katsina hawakuweza kushika hata picha moja ya msafara wa pikipiki 800.
Shule nzima walitekwa hakukuwa na hata mmoja aliyebaki nyuma kibahati bahati kwa sababu yoyore ile hata ugonjwa au wakati wa utekaji alikuwa yuko chooni akijisaidia.Angesaidia polisi kuwatambua watekaji.
Unajaribu kujenga hoja kwamba huu utekaji ni maigizo?.... Na kama ni maigizo unadhani wanafanya kwa malengo gani?

Lazima ukubali mkuu kwamba ugaidi upo, washambuliaji kuja na pikipiki haina maana waliotekwa wote walibebwa na pikipiki huenda walipakiwa kwenye magari/malori au walitembezwa tu.
 
Unajaribu kujenga hoja kwamba huu utekaji ni maigizo?.... Na kama ni maigizo unadhani wanafanya kwa malengo gani?

Lazima ukubali mkuu kwamba ugaidi upo, washambuliaji kuja na pikipiki haina maana waliotekwa wote walibebwa na pikipiki huenda walipakiwa kwenye magari/malori au walitembezwa tu.
Mpaka lini waafrika itakuwa tunadanganyika na vitu ambavyo wengine hawadanganywi.Mikasa kama hii haipatikani hata nchi zenye machafuko ya miaka mingi.Kwamba ni maigizo na utiaji chumvi hakuna shaka na kuhusu malengo tukifuatilia hatutoweza kukosa jibu.
Kwanini unalazimisha kukubali kitu ambacho kina dalili zote za kuwa na kasoro.
Kama kulikuwa na lori la kuwapakia wanafunzi haijatajwa na majirani wa shule hiyo.Na kama wana malori ya kijeshi kwanini wajiunge kwenye msururu wa pikipiki kwenda kufanya uhalifu wa kitaifa kama huo.Wanafunzi 800 ni wengi sana.Mpango wa kuwateka hauwezi kufanywa na kikundi cha wenye pikipiki.Ikiwa kila jambazi moja aliondoka na mwanafunzi mmoja itakuwa pikipiki 800 kuelekea msituni.Hizo piki piki katika teknolojia ya kisasa kama si video basi hata picha moja ingepatikana.Hakuna kitu !.
Kama walifika salama huko msituni bila kuteleza wote basi kutakuwa na kambi kubwa itakayohitaji bajeti kubwa kuwalisha mateka.Hawawezi kukaa kwenye miti kama tumbili.Baada siku moja tu wote wanaweza kuanza kupata kipindupindu.
Lazima yule mkuu wa majeshi wa Nigeria atoe majibu mazuri zaidi aliposema ugaidi Nigeria utaendelea hata miaka 20 ijayo.
 
Ila hao Boko Haram wameonesha dharau sana kwa Rais Buhari. Yaani ni sawa na kwenda kuteka wanafunzi huko Chato wakati MSHUWA yupo huko kwao Chato kwa mapumziko😅😅😅
Buhari aliombwa na serikali ya uingereza kuwa walete jeshi kumaliza tatizo: buhari alikataa
 
Back
Top Bottom