Wenye pikipiki wateka mamia Nigeria

Wenye pikipiki wateka mamia Nigeria

kwa kiukujulisha tu nimebobea katika historia ya makabila jamii. Naifaham vema Historia ya Nigeria
Hujuu chochote wewee. Kamwe huwezi kukuta kabila la Igbo kaskazini ni maji na mafuta. Kaskazini ni Fulani, Kanuri na Hausa.

Igbo wanapatikana Kusini masharaki ambapo imeenda akapaka na Cameroon kusini ambayo ndio Biafra mji wao mkuu Port Harcout. Na ambapo kunapatikana Niger delta na mafuta ya Nigeria ndio maana Igbo people wanataka kujitenga na Nigeria na kuanzisha taifa lao la Biafra

Hausa wameenea kutoka kaskazini hadi wamepitiliza kidogo hadi central Nigeria ambapo wamebaka wakristo wachache katika mji wa Jos.

Haya kusini Magharibi ni Kwa Yoruba ambapo Ndio Lagos ilipo.

Lakini katikati ya Southern east na southern west kuna Benin state (kumbuka siyo Benin nchi iliyotawaliwa na france) bali ni Benin state wanawake wa hawa wa Benin wanasifa ya kujiuza ni machungu ulaya.

Turudi kwa fulani nilishaleta hadi uzi wake humu. Fulani ni Nomads walihama na kuingia Nigeria kutoka Guinea na kuwabadilisha Hausa kuwa waislamu.

Kuna makabila ambayo yanashabiana ka Hausa kama Kanuri ambao pia walicganganyikana na Fulani.

Bono, Katsina Kano ni majimbo ya kaskazini mwa Nigeria ambayo ni Fulani, Kanuri na Hausa.

Hujui kitu weweee kuhusu Nigeria
Fulani si ndio wenye Boko Harama hao. Kisha Igbo ni bright ila mafisadi, misifa na ujuaji mwingi.
 
Kwa taarifa yako hao wa Kaskazini hawawataki wakristo. Hausa wakristo wachache waliobakia wamesukumizwa ha Joz. Kusini kwa wa Kristo kumetulia. Kaskazini licha ya sheria kali za kiislamu ndio huko boko Haram wanachinjana wenyewe kwa wenyewe.

Buhari ni Fulani.
Ibrahim Babangida ni Hausa
Sani Abacha Kanuri
Mashud Abiola ni Yoruba muislamu kwasababu Fulani waliupeleka uislam hadi Yorubaland.

Olesegun Obasanjo Yoruba

List ya Igbo maarufu
Nwanko Kanu
Sunday Olise
Mikel Obi
Goodluck Jonathan
MKO Abiola angekuwa rais angebadili hii nchi kutoka kuwa failed state. Ingawa angepata sana upinzani au angeshindwa kama angekuwa mzembemzembe na mpole.
 
Mpaka lini waafrika itakuwa tunadanganyika na vitu ambavyo wengine hawadanganywi.Mikasa kama hii haipatikani hata nchi zenye machafuko ya miaka mingi.Kwamba ni maigizo na utiaji chumvi hakuna shaka na kuhusu malengo tukifuatilia hatutoweza kukosa jibu.
Kwanini unalazimisha kukubali kitu ambacho kina dalili zote za kuwa na kasoro.
Kama kulikuwa na lori la kuwapakia wanafunzi haijatajwa na majirani wa shule hiyo.Na kama wana malori ya kijeshi kwanini wajiunge kwenye msururu wa pikipiki kwenda kufanya uhalifu wa kitaifa kama huo.Wanafunzi 800 ni wengi sana.Mpango wa kuwateka hauwezi kufanywa na kikundi cha wenye pikipiki.Ikiwa kila jambazi moja aliondoka na mwanafunzi mmoja itakuwa pikipiki 800 kuelekea msituni.Hizo piki piki katika teknolojia ya kisasa kama si video basi hata picha moja ingepatikana.Hakuna kitu !.
Kama walifika salama huko msituni bila kuteleza wote basi kutakuwa na kambi kubwa itakayohitaji bajeti kubwa kuwalisha mateka.Hawawezi kukaa kwenye miti kama tumbili.Baada siku moja tu wote wanaweza kuanza kupata kipindupindu.
Lazima yule mkuu wa majeshi wa Nigeria atoe majibu mazuri zaidi aliposema ugaidi Nigeria utaendelea hata miaka 20 ijayo.
Upo sahihi kabisa.Mwenyewe nimejiuliza maswali hayo.Wanafunzi 800 sio mchezo!
 
Usiwe unakurupuka

Makabila ya kaskazini ambao ni waislamu wanalalamikia uwepo wa Igbos ambao ni wa kusini wakiwa maeneo ya kaskazini wamejipa majina ya kiislamu

Hivi wewe famba kama hujui kitu kukiandika inakuwasha nini?
Unajua Historia Ya Fulani hapo Nigeria?
Ulishasikia kitu kinaitwa Jihad za fulani?
Hawa jamaa walekuwa wakichinja wakristo kabla hata ya wakoloni.
 
Kwa taarifa yako hao wa Kaskazini hawawataki wakristo. Hausa wakristo wachache waliobakia wamesukumizwa ha Joz. Kusini kwa wa Kristo kumetulia. Kaskazini licha ya sheria kali za kiislamu ndio huko boko Haram wanachinjana wenyewe kwa wenyewe.

Buhari ni Fulani.
Ibrahim Babangida ni Hausa
Sani Abacha Kanuri
Mashud Abiola ni Yoruba muislamu kwasababu Fulani waliupeleka uislam hadi Yorubaland.

Olesegun Obasanjo Yoruba

List ya Igbo maarufu
Nwanko Kanu
Sunday Olise
Mikel Obi
Goodluck Jonathan
Goodluck Ebele Jonathan sio Igbo

Wote wanafitiniana ila makabila ya kusini ambao wakristo ndio wengi ni matatizo wale watu ila sio wote ni baadhi

We hujiulizi Yoruba wanataka nchi ya kabila lao ,Igbo nao wanataka nchi ya kabila lao lakini Kaskazini kwa waislamu licha ya kuwa makabila makubwa nao wanayo lakini hawana hizo mambo za makabila za kutaka nchi za kikabila nani mbaya hapo ?
 
Hivi wewe famba kama hujui kitu kukiandika inakuwasha nini?
Unajua Historia Ya Fulani hapo Nigeria?
Ulishasikia kitu kinaitwa Jihad za fulani?
Hawa jamaa walekuwa wakichinja wakristo kabla hata ya wakoloni.
Matusi ya nini na yanakufaidisha nini ewe mjinga uliejawa na chuki ?
 
Upo sahihi kabisa.Mwenyewe nimejiuliza maswali hayo.Wanafunzi 800 sio mchezo!
Na sasa wameshabadili stori,mara 300.Msemaji wa raisi jana tena amesema wamebaki 10 mikononi mwa magaidi.Mkasa mzima ni ujinga mtupu.
Umoja wa mataifa ungekuwa ndio wasimamizi wa mienendo ya ya viongozi nchi mbali mbali basi wangetoa pendekezo Muhammada Buhari aondoshwe madarakani kwa kuruhusu mambo ya kipuuzi nchini mwake.
Kinyume chake Muhammad Buhari angekuwa raisi makini na mwenye nguvu za kimadaraka angesema kuanzia mwezi huu sitaki tena habari za kipuuzi za Bokoharamu wala maharamia kuteka watu.Hilo lingewezekana na dunia ikatulia kufanya mambo ya maana.
Angetoa muda maalum asisikie habari hizo.Na ikipita muda huo akafukuza wakuu wa majeshi wote akaweka wengine wenye sifa za kishujaa katika masuala hayo.
Nchi za ulaya zinakula uchumi wa Afrika na sisi tunashughulika na vitu hewa ambavyo hata katika enzi za giza visingetajwa kutokea.
 
Fulani wana roho mbaya sana. Hawa ni Nomads wanathamini Ng'ombe sana na kujiona superior. Wanasogea kusini nakuvamia ardhi na mashamba na Ng'ombe zao.

Wametapakaa Africa magharibi hadi Western Sudan Darfur. Wengi wako Guinea. Kama unakumbuka al hadj Diouf wa Senegal ni Fulani.

Lakini Hawa Fulani waliona Cha mtwma kuni Central Africa Republic. Ndio wale walikuwa Seleka waliotimuliwa na Anti Balaka. Ni wachache wakatleta dharau na kutaka kuingiza utawala wa sheria na kuwa dharau wazawa na wengi wakristo Antibalaka wakawaambia hawataki upuuzi. Hawatasahau walichofanyiwa
Fulani wana tatizo la kulisha ng'ombe mashamba ya watu

Ila kusini mwa Nigeria kuna wizi na ujambazi viwango vikubwa vya dunia kabisa level za Amerika kusini naweza kusema

Mtu anapita barabarani na gari watampora pasua pasua gari kata na mapanga , wapangaji kuvamiwa na majambazi wenye bunduki kwa ajili ya kutoa waliyokuwa navyo ni kawaida kusini mwa Nigeria tofauti na Bongo hapa anavamiwa tajiri ,duka lenye hela nyingi ,utapeli upo juu sana kusini mwa Nigeria wenyewe wanaita 'yahoo boys' , ushirikina tena wa makundi makubwa ya halaiki nayo ni kusini mwa Nigeria
 
Igbo wanajulikana kwa janjajanja lakini siyo magaidi. Licha ya janja zao wanajituma sana kwa kufanya kazi na biashara za umachinga ukienda Cameron ndio wenyewe wametawala biashara ya spea za magari. Toka 1960s walipigana kujitenga kuanzisha taifa lao la Biafra Kamwe huwezi kumkuta Igbo kaskazini kwasababu ni wakristo watamuua lakini fulani na hayo makabila ya kaskazini utawakuta hadi kusini.

Dangote mwenyewe ni Hausa.
Igbo wanasifika kwa uhalifu (wizi,utapeli,ujambazi,kidnapping,ushirikina('Cult groups')) kuliko hata Yoruba ingawa Yoruba ni watu nao wa kusini

Igbo licha ya sifa ya 'uchagga' kwa Nigeria ila pia wapo na sifa ya uhalifu 'uliotukuka' in Gentamycine voice
 
Igbo wanajulikana kwa janjajanja lakini siyo magaidi. Licha ya janja zao wanajituma sana kwa kufanya kazi na biashara za umachinga ukienda Cameron ndio wenyewe wametawala biashara ya spea za magari. Toka 1960s walipigana kujitenga kuanzisha taifa lao la Biafra Kamwe huwezi kumkuta Igbo kaskazini kwasababu ni wakristo watamuua lakini fulani na hayo makabila ya kaskazini utawakuta hadi kusini.

Dangote mwenyewe ni Hausa.
Igbo/Ndigbo wapo waislamu pia ila ni kwa kiasi kidogo sana

Niliona kwenye media kuhusu uhalifu wenyeji wa kaskazini wakawa wanalalamika Igbo waliopo kaskazini wamejipa majina ya kiislamu wanafanya uhalifu maeneo ya kaskazini
 
Maana ya boko haram ni -Western Education is forbiden
Yaani elim dunya ni haram

Sasa wanáteka wanafunzi wa shule na shule nyingi za hilo jimbo zimefungwa baada ya hilo tukio...kwahyo its win for Boko haram.

Hata pakistan,Afghanistan ISIS wamekuwa wakivamia mashule kama ambavyo alshabaab kenya walivamia chuo..

ujumbe ni uleule elimu ya kidunia ni adui wa Uislam
 
Hilo genge kumbe linatambulika zaidi ya miaka 40 na limekodiwa na Boko Haram.

Source UTV.

Hivi najiuliza yaani genge linakaa vipi miaka 40 wakati serikali ipo,yaani nchi ikitawaliwa na ufisadi na rushwa ngumu kutawalika.Nimeisikiliza hii habari mpaka nashangaa,inafikia hatua mpaka Boko Haram wanalikodi ,sasa siku ndio wakiungana na Boko haram si wanajitengenezea utawala wao kwa baadhi ya maeneo ya Nigeria.
 
MKO Abiola angekuwa rais angebadili hii nchi kutoka kuwa failed state. Ingawa angepata sana upinzani au angeshindwa kama angekuwa mzembemzembe na mpole.
Kwanini una imani sana na huyu jamaa?

Nadhani Buhari amejitahidi sana kwa kiasi kikubwa kuituliza Nigeria, kumbuka mauaji makubwa ya kikabila na mzozo wa kila mara wa kidini huko Jos kipindi Goodluck Jonathan ni Rais bila kusahau Bokoharam kupata nguvu.

Ila toka Buhari amekamata madaraka amejitahidi sana, japo Kuna udhaifu mfano wavulana 300 waliotekwa ila angalau utawala wake unaonekana kuwajibika.
 
Hilo genge kumbe linatambulika zaidi ya miaka 40 na limekodiwa na Boko Haram.

Source UTV.

Hivi najiuliza yaani genge linakaa vipi miaka 40 wakati serikali ipo,yaani nchi ikitawaliwa na ufisadi na rushwa ngumu kutawalika.Nimeisikiliza hii habari mpaka nashangaa,inafikia hatua mpaka Boko Haram wanalikodi ,sasa siku ndio wakiungana na Boko haram si wanajitengenezea utawala wao kwa baadhi ya maeneo ya Nigeria.
Yaani genge la kihuni linaishi miaka yote na serikali ipo?

Nadhani serikali zilizopita ndio zinastahili lawama japo hii ya Buhari pia imeonyesha udhaifu kushindwa kulinda usalama wa wanafunzi.
 
Back
Top Bottom