Leo tena tumepata kali ya kufungia mwaka huko
Katsina jimbo alilozaliwa raisi wa sasa wa Nigaria mheshimiwa Muhammad Buhari ambaye kwa sasa yuko mapumzikoni jimboni kwao.
Inadaiwa watu waliopanda piki piki waliivamia shule ya mchepua wa Sayansi na kufyatua bunduki hewani halafu wakaondoka na zaidi ya wanafunzi 800 ambao mpaka sasa jeshi halijafanikiwa kuwapata wote .
Jeshi la nchi hiyo baada ya kupata taarifa hizo lilifika eneo la tukio na kufanya upekuzi kwenye msitu ulio karibu na shule hiyo pamoja na kushambuliana na watekaji hao.
Bado jeshi halijatoa taarifa rasmi.Hata hivyo maafisa wa serikali wa eneo hilo wamesema hakuna taarifa ya kujeruhiwa hata mwanafunzi mmoja.
Majirani wa shule hiyo wanasema walisikia milio ya bunduki usiku wa manane ambapo walinzi wa shule hiyo walifanikiwa kuwarudisha watekaji hao kabla ya jeshi la Polisi kufika.Majirani wengine wanasema walishuhudia watu hao wenye silaha wakiondoka na wanafunzi waliowateka.
View attachment 1648898