Wenyeji na wazoefu wa mkoa wa Mtwara naombeni Shule

Wenyeji na wazoefu wa mkoa wa Mtwara naombeni Shule

Nimeambiwa sasshv ni msimu wa korosho hivyo kuna hela sana,

Je vitu gan naweza kupeleka huko tukabadilishana na hela zao

(Bidhaa) nimetamani kwenda ila nimetamani kupata ABC
Mkuu hongera kwa wazo zuri.
Mimi siyo mwenyeji wa maeneo hayo lakini nimeishi na kufanya shughuli zangu ndani ndani huko Mahuta Newala, Tandahimba nk nk.
Mimi naona vitu wanavyopenda ni magodoro, Sub woofer, Pikipiki, Simu, Solar Panels, Mabati na Pump za kunyunyiza dawa kwenye mikorosho. Ngoja wengine wajje kukupa data mkuu.
Hongera kwa kuthubutu.
 
Kama una mtaji mdogo tafuta pesa ya kiroba cha ngano na mafuta lenga vijiji vya masasi kauze maandazi na chai, kweny chai sukari tia mwenyewe wamakuwa ukiwaachia kujitilia sukari unaweza kukuta sukar kg 1 wametumia watu wa 3 tu imeisha [emoji1][emoji1]
[emoji23]
 
Mkuu hongera kwa wazo zuri.
Mimi siyo mwenyeji wa maeneo hayo lakini nimeishi na kufanya shughuli zangu ndani ndani huko Mahuta Newala, Tandahimba nk nk.
Mimi naona vitu wanavyopenda ni magodoro, Sub woofer, Pikipiki, Simu, Solar Panels, Mabati na Pump za kunyunyiza dawa kwenye mikorosho. Ngoja wengine wajje kukupa data mkuu.
Hongera kwa kuthubutu.
Ahsante mkuu
 
Wamakua kwa sukari🙌🏽
Kuna mmoja alikutwa mgahawan kajaza sukar kweny chai hadi imetokeza juu ya kikombe utadhan anatengeneza asali 😄😄
Wanamsemo wao wenyew wanasema Ilimpite nkijilamba
Mkuu ukienda zingatia zaid vijiji vya masasi huko kwa wamakuwa ndio wanajua kutumia hela kuanzia watoto hadi wazee, ila wamakonde wabahili sana labda vijana na wamama
 
Mm nipo masas vijijini uku ukileta radio,memory card, sendo za ke na me na vinguo vya mitumba utauza.
 
Back
Top Bottom