The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dar Es Salaam(DAWASA), Mhandisi Mkama Bwire ametoa wito kwa wenyeviti wa serikali za mitaa kutoka wilaya ya Kigamboni kuhamasisha wananchi kuweza kujiunga na mtandao wa maji ili waweze kuvutiwa maji majumbani kwao.
Mhandisi Bwire amesema hayo akizungumza leo Februari 21 akiwa mtaa wa kigogo Kigamboni alipokuwa akikagua mradi wa kusambaza maji wa kilomita zaidi ya 21 unaotekelezwa katika mtaa huo.
Katika ufunguzi wa Kikao Kazi na Wenyeviti wa Mitaa ya Kigambo Mhandisi Bwire amesema mamlaka hiyo inatambua nafasi muhimu ya viongozi wa mitaa katika kuhamasisha wananchi katika kusambaza maji majumbani lakini pia ameahidi kushirikiana nao kwa karibu kupata suluhisho la kusaidia kuhamasisha wananchi kujiunga na mtandao wa maji ya DAWASA.
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Kigogo Ramadhan Mohammed ameishukuru DAWASA kwa kuwafikishia maji na kueleza kuwa wamefurahi kwani ilikua ni haja yao ya muda mrefu.
“nashukuru DAWASA kwa kutuletea mradi huu mkubwa katika mtaa wangu kutokana na visima vingi kuwa katika mtaa huu hii kwetu ni faraja wametukumbuka”
Wenyeviti wa mitaa ya Kigamboni wametembelea miradi ya kuzalisha maji iliyopo kimbiji, tenki kubwa la kusambaza maji lenye uwezo wa kubeba lita milioni 15 lililopo mtaa wa kigogo pamoja na mradi wa kusambaza maji uliopo mtaa huo huo.