Wanaokataa kuhama Ngorongoro, labda watumie mabavu. Kwa msingi wa sheria, hawawezi kushinda.
Kwa sheria zetu, ardhi yote ni mali ya umma na msimamizi wake mkuu ni Rais wa JMT.
Rais ana mamlaka ya kubadilisha matumizi ya ardhi wakati wowote alimradi mabadiliko hayo yawe kwa manufaa ya umma.
Watanzania kama tunataka tuwe na maamuzi juu ya maisha yetu, ni lazima tupiganie kupata katiba mpya. Kwa katiba hii na sheria za ardhi zilizopo, wamasai wa Ngorngoro,watapigwa bakora, watalala mahabusu, mahakamani hawatashinda, na kuhama watahama. Wasipokaa vizuri, baadhi yao, na jela wataenda.