Mimi niliishi nyumba moja ya kupanga Kinyerezi chumba na sebule, nyumba ipo juujuu, kwa chini kuna mama mmoja anaishi na watoto wake wawili wa shule ya msingi, alikuwa akifungulia subwoofer asubuhi mpaka saa 4 usiku, nikamfata mara mbili. Akaniambia yupo kwake yeye hajapanga, nikaenda serikali za mitaa sikupata msaada, nikabakiwa na njia moja tu ya kibabe. Nilikuwa na amplifier ya technics watts 1000 na speaker mbili za Sony, mimi mtu wa kupiga vyombo(kvant) na nimejiajiri. Ili nisimuonee huruma na watoto wake wa primary, nikaanza kampeni ya siku 5, jumatatu hadi ijumaa kimyakimya. Nilikuwa napiga vyombo bar narudi saa 4 usiku, akizima mziki wake saa 4 namuachia saa limoja la kujiandaa na kulala, Saa 5 usiku naweka Speaker mbili madirishani kuelekea kwake, moja sebuleni moja chumbani dirishani, napiga muziki hadi saa 12 asubuhi. Baada ya siku mbili kiliitishwa kikao na mjumbe, akimshirikisha mwenyekiti serikali za mitaa. Tukaitwa wote tunaokaa eneo hilo,Ukatolewa mwongozo kuhusu kuweka muziki sauti ya juu. Kuanzia siku hiyo nikaonekana shujaa kila ninakopita, na nilikuwa mpangaji mgeni, nikawa maarufu kwamba nimekuja kumkomesha yule mama alishashindikana. Hakuwahi kuweka sauti ya juu tena mpaka naondoka, nilikaa mwaka nikaondoka. Sometimes dawa ni jino kwa jino😂