Wenzangu mnaishije na jirani anayefungulia sabufa hadi mwisho

Huu ujinga ndo niliukataa

Nkiwa natoka job shift ya usiku mwenzangu anawasha kwa sauti ya juu inapelekea mimi kutokupata usingizi wakati nimerudi kutoka job halafu kibaya sasa me huwa sisemi hata kidogo huwa natulia tu

Ebhanaee nkaona huyu ananichezea nna li home theater hapo ya kibabe asee alijuta kukaa nyumba moja na mimi yani alidiriki kunifata na kuniambia nipunguze na kupunguza kwenyewe ni kidogo sana

Dawa ya moto ni moto mzee acha unyonge
 
Jino kwa jino. Kodi spika moja kubwa ,yeye akizima wewe washa na weka matangazo ya sumu ya panya au Kodi Generator la sauti kubwa akizima wewe washa, akirudia huyo ni kichaa hivyo inabidi uhame tu.
Hapo kwenye generator fresh maana mimi wkt mwingine huwa nachanganyaga beat za singeli na mlio wa jenereta,, sounds the same πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„. Piga generator kwa huyo mwamba.πŸ˜‚
 
Ni vile maisha magumu, ungekuwa kwako usingekiwq na hizi kero
....

Chumba chako hakina ceiling board?
Hakina ceiling board bado najitafuta si unajua tena

Ina maana hapa ni kama kambi mtu ukichoka na makaz ya hapa na pale unakuja kupumzika hasa wakati wa kupumzika ndo unakuja unakutana na hayo makelele
 
haya bhana sema daah nimecheka sana
 
Watu kama hao ni washamba halafu malimbukeni
 
Kama Una pikipiki hasa hizi kubwa, iingize ndani halafu uwe unaiwasha na kupiga resi mwanzo mwisho, itegee kamba accelator isirudi chini, sema mambo ya kitoto Sana halafu kama mfuko unaruhusu Bora uhame kabisa.
 
Na Mimi
Hicho kitu kilinikuta ... Nilienda nikanunua sea piano kubwa nikamtetemesha ndani usiku kuchat na mapiano huku Mimi nimekaa njeee... Toka hapo akiniona tuu sauti ikiwa kubwa anaenda kupunguza mwenywe

 
Jino kwa jino. Kodi spika moja kubwa ,yeye akizima wewe washa na weka matangazo ya sumu ya panya au Kodi Generator la sauti kubwa akizima wewe washa, akirudia huyo ni kichaa hivyo inabidi uhame tu.
Mimi sitaki kelele sasa nikiwa kama yeye tofauti gani itakuwepo?
 
solution tit for tat diplomacy … kodi mziki wa sherehe weka ndani ukiuwasha mpka ardhi inatikisika alafu uone kama atasumbua
 
Na mfungulia langu hadi anazima au unahama tu
 
Jino kwa jino. Kodi spika moja kubwa ,yeye akizima wewe washa na weka matangazo ya sumu ya panya au Kodi Generator la sauti kubwa akizima wewe washa, akirudia huyo ni kichaa hivyo inabidi uhame tu.
😁😁😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…