Wenzetu sikukuu zenu mnatuvunja moyo.

Tatizo nyie watu huwa mnajibagua sana hata kabla hamjabaguliwa! Ona mentality yako kwa nini usijichanganye!
 
Mkuu uko right sio TZ hata Ug wako hivyo kwenye Eid fitri huwa wanaaza kunikumbusha kwenye Chungu cha 20 Leo mwaka wa pili ikifika Xmass wanajifanya hawana habari , utawasikia ' merry xmass see u next year'' Leo nimegonga ugali wa karo wakati wafanyazi wenzangu wanagonga vyuku, wamejikomesha next time will not invite non Muslim kabisa kwa eid
 
Leo waislamu mmecharuka. Christmas imewatia uchizi au? Mnapoalika huwa mmelazimishwa au ni kufuata misingi ya mtume wenu? Kuna aliyewalazimisha mfuturu nje ya nyumba?

PAMBANENI NA HALI ZENU MNABOA SASA AAAH!!!!!
Uwe na tabia ya kusoma ili uelewe,
Sio kumaliza kusoma.
Kuna mwenzio namlisha nyamafu hapa, mwaliko wa Krismasi utamtokea puani
Mungu anakuona.
 
Omba mualiko vizuri...hii tabia ya kulialia imeanza kuota sugu
 
Umenena,
Ila waache uroho kwa vya watu basi.
 
Mpaka muda huu bila bila

Yaani sikukuu kama sio sikukuu

Kila mtu anapikia ndani.......

 
Alaaaaa?
Laki hapana, mmhmmhmmh.
siwezi ita sheikh anichinjie kuku wakati mwenyewe ni mtaalam. kama huko tayari karibu tule ndio wanapakua hapa ila kumbuka aliyechinja ni mimi kutoka ile jamii iitwayo ya makafiri vingine lipo pilau na mboga za majani kwa ajili yako
 
Kumbe wanajialika wenyewe.
Unasubiri anayejialika akualike.
Haya subiri kadi.
Nayaangaliga yanavyopaparika yakisikia harufu na makaangizo ya mahanjumati.
Ila, binafsi Sina hiyo tabia, kujialika?
No.
 
Achana na huyo mkuu, karibuni sana, hatuko hivyo na wote wanajua huyu jamaa ana lake
Huwa nawasumbua sana jamaa zangu wakati wa Mfungo (mwezi mtukufu) as if na mimi ni mfungaji..!

Napenda sana wanavyo kuwa wakarimu katika kipindi hiko..

Mapishi matamu yanayo ambatana na vinywaji Maridhawa (Uji wa Pilipili Manga)

Kimbembe ni pale inapo tufikia Kwarezima, huwa tunashindwa angalau kuonesha/kutoa ushirikiano.
 
Sasa pilau ya uku home limechanganywa na kitimoto je utaweza kula? ?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Pole sana Mkuu hao majirani zao hawajafanya poa kabisa. Ila Mkuu hali ya sasa mhhh isije ikawa na hao uliowategemea bado hawajapata grisi. Hatahivyo pole sana ni kweli haipendezi kwa jirani pilau linanukia alafu we unakula harufu tu watanzania huo sio utamaduni wetu. Wasamehe bure!!!
 
Na wengi huwa wanafuata uji tu. Nisikufiche huwa tunafarijika sana, ukisikia adhana ya Magharibi tu sogea Baraza lililo karibu ahahahahaa hiyo ndio Ramadhani
 
Usifanye hivyo, naamini hukulelewa ktk tabia hiyo wewe unaitoa wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…