Da Vinci XV
JF-Expert Member
- Dec 7, 2019
- 3,862
- 6,438
Na Da Vinci XV
Chanzo: Forbes
Wasalaam
Wahenga walisema wakati ni ukuta.
Sasa wakati huo ambao mimi nikihangaika kumpigia kelele mbunge wangu nilie mchagua miaka 4 iliyopita anijengee daraja walau niweze kuifikia zahanati kwa urahisi ili mimi na familia yangu tuweze kupata huduma bora za kiafya , ndio wakati huohuo wenzetu huko Ulaya na Nchi za magharibi wakiendelea kutuacha hatua nyingi nyuma,mithili ya mbio za farasi na kobe.
Wakati wenzetu wakifika hatua ya kueneza njia tofauti tofauti za kumhudumia mgonjwa ili kufanikisha usahihi wa huduma iliyo makini kama Robotic Surgeries na nyinginezo kwenye nchi zilizoendelea na zinazoendelea, sisi kwetu tunahangaika walau tupate wauguzi wawili kwenye zahanati inayohudumu zaidi ya wananchi 7000 kule kijijini namtumbo.
Kwa mujibu wa National Library of Medicine (NLM) kwa mwaka 2023 tu zaidi ya system 7733 za Robotic Surgiries zimesanikishwa nchi mbalimbali duniani na zaidi ya surgeries 10 Millioni zimefanyika, surgires hizo zimehusisha idara tofauti tofauti kama Urology, gynacology ,na cardiothoracic surgeries.
Wakati wenzetu wakifanikisha hayo yote sisi bado hata wataalamu wetu hawana ujuzi unaojitosheleza kufikia kiwango cha juu kabisa cha ubora katika utoaji wa huduma za afya, malalamiko yapo kila iitwayo leo.
Naam, kwa tulipoanza hadi tulipofikia si haba , sio tulipoazimia kuwepo hili halina shaka. Tulipotoka kulikuwa na wingu jeusi zaidi ya tulipofikia sasa
Kongole kwa serikali na sekta za Afya katika kuijenga Tanzania nyoofu.
Lakini bado sana kufikia kiwango cha nchi za waliondelea kama tunataka kuinua sekta zetu walau tufikie hata level ya Afrika kusini.
Chanzo: Emerging Health Initiatives
Natangulia kusema hayo baada ya jitihada tele za serikali na wizara ya Afya katika kuboresha na kufikia lengo la huduma bora kwa jamii.
Ni miezi miwili tu hapo nyuma ambapo serikali kupitia wizara ya Afya ilidhamiria kuanzisha Taasisi mahususi ambayo itakuwa inashughulika na masuala ya upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu ili kuboresha zaidi huduma za kibingwa kutoka katika Taasisi ya mifupa (MOI)
Hayo yote yalianishwa na Mh.Ummi Mwalimu tarehe 27 mwezi April Mwaka huu Wakati wa Uzinduzi wa chama cha Madaktari bingwa wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (Tanzania Neurosurgical Society).
Kwenye swala hili tutapigia makofi ni jitihada za kuwezesha kufikia tanzania tuitakayo katika nyanja za Afya na teknolojia.
Jitihada nyingi zimefanyika kuboresha huduma kwa kuongeza miondombinu ya kuifikia huduma ya afya, ujengwaji wa barabara na madaraja katika vijiji ili kufikia huduma za kiafya kiurahisi ,ujengwaji wa hospitali, zahanati na vituo vya afya ili kusambaza huduma za afya hadi vijijini ambapo ndiko kuna changamoto kubwa katika masuala ya afya.
Na hii imesaidia mambo mengi , ikiwemo kupunguza vifo vya mama na mtoto kupunguza magonjwa mlipuko kama kipindu pindu n.k.
Lakini je tumejitosheleza katika kufikia lengo hilo kiteknolojia, maarifa na Utendaji ????
JE WAHUDUMU WETU WAMEJITOSHELEZA KI UTENDAJI NA MAARIFA KATIKA UTOAJI HUDUMA ZA KIAFYA.???
Wakati serikali ikipambana kuongeza wahudumu na wafanyakazi (utendaji) katika vituo vyetu ambao bado takwimu zinaonyesha kuwa hawajitoshelezi. Wenzetu huko nchi za magharibi na Ulaya hata ukanda wa mashariki wameongeza system za utendaji kufikia hatua ya mifumo mingi ya Roboti kufanya upasuaji.
Mfano kwa mujibu wa www.merillife.com mpaka kufikia mwaka 2021 india tayari kulikuwa na roboti 76 za kufanya upasuaji na zaidi ya surgeons 500 ambao wana mafunzo kamilifu ya kufanya upasuaji kwa kutumia system ya Roboti, na kwa nchi za Afrika , Afrika kusini wao wamefanikiwa kuwa na Roboti 6 ambazo zinafanya upasuaji mpaka kufikia sasa.
Chanzo: Orthopaedic wing, pretoria East hospital
Sasa kama ilivyoanishwa Mh.Ummi Mwalimu hiyo tarehe 27 April mwaka huu.
Mh.Ummi alipata kusema Tanzania kuna Madaktari bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya fahamu 25 tu, ambapo kwa mujibu wa shirika la Afya duniani (WHO) inapendekezwa walau katika kila watu 150000 kuwe na daktari mmoja bingwa wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu.
Sasa gap lipo hapa kama utachukua madaktari wetu hawa bingwa 25 tulionao maana yake daktari bingwa huyu mmoja atahudumu kwa watanzania MIL 2,400,000 na kama alivyoanisha Mh.Ummi huduma hizi bado hazijawafikia watanzania wengi hivyo sambamba na hilo alipendekeza kuwapa hamasa hata madaktari wengine kusomea fani hizi ili kufikia lengo fulani.
Kwa mfano huo nadhani unapata picha ya gap tulilonalo si katika fani hiyo tu bali fani zote zina upungufu wa watendaji katika kuhudumia watu na haswa haswa maeneo ya vijijini lakini pia wahudumu waliopo je wana weledi wa kutosha katika kuhudumia watanzania haswa haswa katika nyanja za kiteknolojia na sayanisi kwa Ujumla??. Jibu ni HAPANA
Hili swala limeimbwa sana na liko wazi takwimu zinatujuza hili hivyo mapungufu yetu kama taifa
Mosi, Watendaji kazi katika kutoa huduma za kiafya zilizo bora
Pili, Weledi katika utendaji, je tumeweza kutoa maarifa ya kutosha kuwawezesha watendaji wetu kupunguza gap hili lilipo
Kama wenzetu wameweza kuingiza mifumo ya roboti katika njia zao za kimatibabu je sisi miaka mitano mpaka kumi ijayo tutajaribu kufanya nini??? Na kuboresha kipi katika sekta hii ya Afya.
Chanzo: IG account Ummimwalimu
TUFANYE NINI ILI TUWEZE KUBORESHA HILI. NA KUONDOKANA NA CHANGAMOTO HIYO.
(Utendaji na weledi)
1- KUBORESHA VITUO VYETU VYA MAFUNZO KITEKNOJILIA NA VITENDEA KAZI
Dunia ya sasa inakimbizana sana na mfumo wa maisha ambao sayansi na teknolojia vimechukua sehemu kubwa sana ya maisha ya walimwengu hivyo basi hivi vyuo vya kati na vikuu ambavyo vinaandaa hawa watendaji kazi wanaokuja kutuhudumia hapo mbeleni
Serikali na sekta za kusimamia hivi vyuo Wahakikishe vinaboreshwa kwa namna ambayo italeta athari chanya katika kuwapika wahitimu wa fani za Afya na Watendaji ikiwemo
Upatikanaji wa vifaa vya kujifunzia kama Kompyuta za kutosha, Maabara , Skills Labs na vingine vingi vyenye ubora wa hali ya juu ili kumwezesha mwanafunzi huyu ambaye ni mtumishi wa baadae kupata elimu nyoofu na sahihi ili kuwa na maarifa yanayojitosheleza.
Chanzo:Hamilton Health Sciencies
2- KUTOA SEMINA KATIKA FANI TOFAUTI TOFAUTI KILA BAADA YA MIEZI KADHAA KWA HAWA WATUMISHI WALIO MAKAZINI
Ili linaweza kupunguza kwa namna moja au nyingine ule woga na ujinga ambao baadhi ya watendaji wamekuwa nao juu ya task fulani ., hivyo basi semina hizi zitaongeza weledi ,maarifa na kujiamini kwa watendaji wetu katika utoaji wa huduma na kutoa huduma ipasavyo. Kila wapatapo update mpya juu ya huduma fulani ili kuweza kufukia mashimo ya changamoto za kiafya kila tupatapo mbinu mpya ya kumpatia mhitaji huduma nzuri.
3- KUHAMASISHA WATENDAJI WETU KUONGEZA ELIMU KATIKA FANI TOFAUTI ILI KUPATA WATAALAMU WENGI KATIKA NYANJA TOFAUTI ZA AFYA
Kama alivyolisema waziri Ummi, hii itasaidia kupata wataalamu wengi wabobezi katika fani tofauti tofauti ambao kwa namna moja au nyingine watasaidia kusukuma gurudumu la afya katika taifa ili kuepusha changamoto hizl tunazopitia
Wengi katika watumishi wameridhika elimu waliyonayo toka machuoni hivyo serikali pamoja na wadau wa afya wana jukumu kubwa katika kuhakikisha wanatoa hamasa na chachu kwa watendaji wetu uli waweze kuongeza elimu katika fani tofauti tofauti ili kupata wataalamu bobezi kiafya.
4- KUTOA UFADHILI KWA WANAFUNZI NA WATENDAJI WANAOHITIMU KATIKA FANI NA KADA ZA AFYA KUJIPATIA ELIMU NJE
Wanafunzi na watendaji wanaokizi vigezo vya kupata elimu kutoka nchi nyingine zilizopiga hatua kiafya, serikali ingeweka mpango mkakati madhubuti wa kutoa ufadhili ili watendaji wetu na wanafunzi kujizolea maarifa ambayo yanaweza kuwa tija kwa taifa kwa miaka mitano hata kumi ijayo katika huduma zetu za kiafya nchini.
Ubora wa maarifa wayapatayo huko nje yanaweza kuboresha kwa kiwango kikubwa mfumo wetu wa afya kupata huduma nzuri ambayo pengine nchi nyingi za kiafrika hazijafikia huko.
5- KUKUZA USHIRIKIANO (Forster collaboration and Partnership)
Kuna mashirika makubwa kama NGOs na mengineyo ambayo tukishirikiana nayo na kuchota waliyonayo na uzoefu wao wa kazi katika nchi nyingine walizohudumu basi tutapiga hatua kubwa sana , organization zetu , serikali na sekta ya afya kwa ujumla zinapaswa kukuza ushirikiano ili kujizolea maarifa ya kiutendaji katika kutoa huduma za kiafya na vitendea kazi.
Pia ushirikiano na mataifa yaliyoendelea katika utoaji huduma za Afya kama Marekani na Cannada ambao wenzetu kwa kiwango kikubwa wameweza kuvuka changamoto nyingi ambazo zinagharimu sekta zao za afya hii inaweza kuwa njia moja wapo ya kufikia Tanzania yenye mwanga katika utoaji huduma za afya
SIO LAZIMA NDANI MIAKA 5 HADI 10 TUFIKIE WALIPOFIKA WENZETU WENYE MIFUMO YA ROBOTI ZA UPASUAJI LA HASHA!!... LAKINI WALAU TUWE TUNA MIFUMO YETU AMBAYO INAEPUKA CHANGAMOTO NYINGI ZA MFUMO WA AFYA AMBAZO TUNAKABILIANA NAZO HIVI SASA.
ASANTENI.

Upvote
5