Wenzetu wamefiwa...

Wenzetu wamefiwa...

Invisible

JF Admin
Joined
Feb 26, 2006
Posts
16,286
Reaction score
8,380
Kuna mwanachama mwenzetu anayejiita MwenyeNeema amenitumia email hii:

MwenyeNeema said:
Hi Familia ya Jamii Forums,

Ninajisikia kuwashirikisha katika msiba wa mwanangu binti yangu mpendwa Mary, aliyefariki kwa ajali ya gari tarehe 25 August 2009 na kuzikwa tarehe 27 August 2009.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa, lihimidiwe jina lake.

Ni kipindi kigumu kwangu lakini kwa faraja ya Mwenyezi Mungu na ninyi wenzangu, kipindi hiki kigumu sana kitapita.

Kwa niaba ya wana JF wenzangu (ambao hawataandika wenyewe) na kwa niaba ya safu ya uendeshaji wa JF tunapenda kutoa salaam zetu za rambi rambi kwa mwenzetu MwenyeNeema kwa msiba huu.

Pole ndugu yetu na Mungu akujalie uvumilivu katika kipindi hiki kigumu
 
Pole sana kwa kuondokewa na kipenzi binti yako. Ni mapema mno kwa yeye kuondoka na kukuacha lakini nina uhakika huko aliko yuko kwenye mapumziko ya amani ya milele. Mungu akubariki na akupe nguvu za kushinda kipindi hiki kigumu.
 
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe,
raha ya Milele umpe ee bwana na mwanga wa Milele umwangazie,
astarehe kwa Amani.
Amen.
 
Nami naungana na wenzangu katika kuwapa pole wafiwa.
Wawe Wa Neema. Amina.

SteveD.
 
Pole sana Mungu akupe faraja katika kipindi hiki kigumu!
 
Hakika sisi ni mavumbi na mavumbini tutarudi. Pole sana mdau. Mola akupe moyo wa uvumilivu na subira.
 
Hakika sisi ni mavumbi na mavumbini tutarudi. Pole sana mdau. Mola akupe moyo wa uvumilivu na subira.
Kuna member mmoja aliniuliza Yo Yo yuko wapi mbona yuko kimya?

Nimepata taarifa toka Dar kuwa yuko Tz na amekumbana na "ukosefu wa internet mtaani" ugonjwa unaowasumbua wengi wafikapo Tz. Nafahamishwa ni mzima na atarejea JF karibuni baada ya vacation.
 
Kuna member mmoja aliniuliza Yo Yo yuko wapi mbona yuko kimya?

Nimepata taarifa toka Dar kuwa yuko Tz na amekumbana na "ukosefu wa internet mtaani" ugonjwa unaowasumbua wengi wafikapo Tz. Nafahamishwa ni mzima na atarejea JF karibuni baada ya vacation.

Mimi nilidhani Yo Yo yuko bongo (though najua hayuko bongo)...Lol

I hope watamkatalia kurudi kiwanja. Na asirudi tena JF
 
wafiwa poleni sana hii huwa mbaya inapokuwa kwako wacha tu machungu si mchezo kilio kisikie kwa mwenzio bwana
 
Poleni wafiwa wote.

Newakagone (wakalale kwa amani)
 
poleni sana, Mungu awapenguvu za kustahimili na awape faraja ya kweli ili muweze kuendelea na maisha yenu kwa mafanikio.
 
Mungu awajalie faraja katika kipindi hiki kigumu na cha kuhuzunisha kwenu.

Poleni sana.

Tuzidi kumuomba Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi - Amina
 
MwenyeNeema, my deepest sympathies to you and your family.
 
Ndugu MwenyeNeema, pole sana kwa kuondokewa na binti yako mpendwa. Mungu akupe uvumilivu na awe nawe zaidi katika kipindi hiki kugumu na cha majonzi.
Apumzike kwa amani binti yako,Amen!..
 
Ndugu Mwenyeneema pole sana kwa msiba wa bint yako,yote hiyo ni mipango ya Mwenyezi Mungu!!!!
 
Mwenyezi Mungu akujalie Faraja katika Kipindi hichi kigumu cha Majonzi.Pole sana Ndugu yetu MwenyeNeema.Upo pamoja nasi katika sala zetu!

Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani binti yetu mpendwa..
 
Pole Mwenye Neema, msiba ni mojua ya neema za Mungu kwa kuitwa makao ya milele mapema, Sisi tulimpenda, ila Bwana amempenda zaidi na amemuita, yu pamoja nae.
 
Back
Top Bottom