DullyJr
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 13,983
- 11,857
FAHAMU HAYA VYEMA MKAJUA SIMBA IMEFANYA NINI AFRIKA HII.
Mwaka 1977, Simba iliweka rekodi katika mechi za watani wa jadi kwa kuifunga Yanga mabao 6-0. Zaidi ya miaka 42 rekodi hiyo haijafikiwa.
—
Mwaka 1938, Sunderland (kwa sasa Simba SC) ilikuwa timu ya kwanza kucheza na jezi ilipocheza na timu ya kombaini ya mabaharia wa meli zinazotia nanga kwenye bandari ya Dar es Salaam.
—
Mwaka 1941, (Sunderland) kwa sasa Simba SC ilikuwa timu ya kwanza nchini kuvaa viatu kwenye mechi rasmi ya mashindano dhidi ya timu ya jeshi la maji la mkoloni la Afrika Mashariki.
—
Mwaka 1959, kabla ya uhuru wa Tanganyika, kipindi hicho ikiitwa Sunderland (kwa sasa Simba SC) ilikwenda Ethiopia na ikawa timu ya kwanza kutoka nchini kupanda ndege. Ilikwenda kwa mwaliko wa Mfalme Haile Selassie wa Ethiopia.
—
Mwaka 1965, Simba ilikuwa klabu ya kwanza kushinda ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania.
—
Mwaka 1968, Simba ilikuwa timu ya kwanza nchini kumiliki basi lake.
—
Mwaka 1974, Simba ilikuwa klabu ya kwanza kuwa Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati. Pia mwaka huo Simba ikawa klabu ya kwanza kutoka Tanzania kufika nusu fainali ya Klabu Bingwa ya Afrika.
—
Mwaka 1979, Simba ilikuwa klabu ya kwanza na ya pekee duniani kwenye mashindano ya mabara tofauti kufungwa nyumbani magoli 4-0 na kushinda ugenini magoli 5-0 (dhidi ya Mufulira Wanderers).
—
Mwaka 1993, Simba ilikuwa klabu pekee nchini kuwahi kufika fainali ya mashindano yanayoandaliwa na CAF (kwa sasa Kombe la Shirikisho) na kucheza fainali na klabu ya Stella Abidjan ya Ivory Coast.
—
Simba ndio mabingwa wa muda wote wa Kombe la Afrika Mashariki na Kati (makombe 6).
—
Mwaka 2003, Simba ilivunja rekodi ya Zamalek ya Misri kwa kuitoa kwenye Ligi Mabingwa Afrika na kutinga hatua ya makundi. Zamalek walikuwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo.
—
Mei 6 Mwaka 2012 simba iliinyuka Yanga mabao matano kwa nunge kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa wafungaji wakiwa ni Felix Sunzu akifunga mara mbili Emanuel Okwi akifunga mara moja marehemu Patric vierra Mutesa Mafisango pamoja na Juma K Juma ..
Simba ndio klabu yenye makombe mengi ya jumla kuliko klabu yoyote Afrika Mashariki, ikiwa na vikombe rasmi vya kimashindano hamsini na nane(58) Hakuna klabu yoyote zaidi yetu yenye mataji rasmi kwenye kumbukumbu za makabati yao
Kinachokuja kirahisi hakidumu na kinachodumu hakiji kirahisi ndugu zangu ..Pichani ni Mohamed Dewji na wachezaji wetu ilikuwa ni mwaka 2002 timu klikuwa chini ya kocha James Siang'a
Acheni ball itembee Ukinielewa mimi umelielewa SOKA
Simba Sunderland
View attachment 2412952