Kalpana
JF-Expert Member
- Jun 16, 2017
- 32,603
- 62,269
Umemaliza watakwambia kombe la Hedex kwani wanaumwa vichwa? Wajibu waambie hatuchagui mashindano
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umemaliza watakwambia kombe la Hedex kwani wanaumwa vichwa? Wajibu waambie hatuchagui mashindano
Kwann usipeleke katk gazeti la dimba uwez kosa alfu tatuFAHAMU HAYA VYEMA MKAJUA SIMBA IMEFANYA NINI AFRIKA HII.
Mwaka 1977, Simba iliweka rekodi katika mechi za watani wa jadi kwa kuifunga Yanga mabao 6-0. Zaidi ya miaka 42 rekodi hiyo haijafikiwa.
—
Mwaka 1938, Sunderland (kwa sasa Simba SC) ilikuwa timu ya kwanza kucheza na jezi ilipocheza na timu ya kombaini ya mabaharia wa meli zinazotia nanga kwenye bandari ya Dar es Salaam.
—
Mwaka 1941, (Sunderland) kwa sasa Simba SC ilikuwa timu ya kwanza nchini kuvaa viatu kwenye mechi rasmi ya mashindano dhidi ya timu ya jeshi la maji la mkoloni la Afrika Mashariki.
—
Mwaka 1959, kabla ya uhuru wa Tanganyika, kipindi hicho ikiitwa Sunderland (kwa sasa Simba SC) ilikwenda Ethiopia na ikawa timu ya kwanza kutoka nchini kupanda ndege. Ilikwenda kwa mwaliko wa Mfalme Haile Selassie wa Ethiopia.
—
Mwaka 1965, Simba ilikuwa klabu ya kwanza kushinda ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania.
—
Mwaka 1968, Simba ilikuwa timu ya kwanza nchini kumiliki basi lake.
—
Mwaka 1974, Simba ilikuwa klabu ya kwanza kuwa Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati. Pia mwaka huo Simba ikawa klabu ya kwanza kutoka Tanzania kufika nusu fainali ya Klabu Bingwa ya Afrika.
—
Mwaka 1979, Simba ilikuwa klabu ya kwanza na ya pekee duniani kwenye mashindano ya mabara tofauti kufungwa nyumbani magoli 4-0 na kushinda ugenini magoli 5-0 (dhidi ya Mufulira Wanderers).
—
Mwaka 1993, Simba ilikuwa klabu pekee nchini kuwahi kufika fainali ya mashindano yanayoandaliwa na CAF (kwa sasa Kombe la Shirikisho) na kucheza fainali na klabu ya Stella Abidjan ya Ivory Coast.
—
Simba ndio mabingwa wa muda wote wa Kombe la Afrika Mashariki na Kati (makombe 6).
—
Mwaka 2003, Simba ilivunja rekodi ya Zamalek ya Misri kwa kuitoa kwenye Ligi Mabingwa Afrika na kutinga hatua ya makundi. Zamalek walikuwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo.
—
Mei 6 Mwaka 2012 simba iliinyuka Yanga mabao matano kwa nunge kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa wafungaji wakiwa ni Felix Sunzu akifunga mara mbili Emanuel Okwi akifunga mara moja marehemu Patric vierra Mutesa Mafisango pamoja na Juma K Juma ..
Simba ndio klabu yenye makombe mengi ya jumla kuliko klabu yoyote Afrika Mashariki, ikiwa na vikombe rasmi vya kimashindano hamsini na nane(58) Hakuna klabu yoyote zaidi yetu yenye mataji rasmi kwenye kumbukumbu za makabati yao
Kinachokuja kirahisi hakidumu na kinachodumu hakiji kirahisi ndugu zangu ..Pichani ni Mohamed Dewji na wachezaji wetu ilikuwa ni mwaka 2002 timu klikuwa chini ya kocha James Siang'a
Acheni ball itembee Ukinielewa mimi umelielewa SOKA
Simba Sunderland
View attachment 2412952
Wakati huo alikuwa kwao amevaa shati reeefu bila kaptura anachunga mbuziUna miaka mingapi mkuu?kipindi Simba inawapiga mabingwa watetezi wa CL Zamalek ya Misri katika ardhi ya Misri ulikuwa pori gani? Sio hao wanaoshiriki kombe la failure
Wakati huo alikuwa kwao amevaa shati reeefu bila kaptura anachunga mbuzi
Mliwafunga hao Zamaleki magoli mangapi? Mimi naongelea kuwatoa hao Waarabu kwa kuwafunga kwenye ardhi yao! Nipe majibu sahihi hapa. Mliwafunga goli ngapi pale Misri?Una miaka mingapi mkuu?kipindi Simba inawapiga mabingwa watetezi wa CL Zamalek ya Misri katika ardhi ya Misri ulikuwa pori gani? Sio hao wanaoshiriki kombe la failure
Wewe kiboko yako ni yule Mwenyekiti wako tu aliyekuita mbumbumbu! Unamgwaya kiasi hutaki hata kulisikia jina lake.Wakati huo alikuwa kwao amevaa shati reeefu bila kaptura anachunga mbuzi
Hatoki akilini mwako 24/7Wewe kiboko yako ni yule Mwenyekiti wako tu aliyekuita mbumbumbu! Unamgwaya kiasi hutaki hata kulisikia jina lake.
Umeweka vitu vingi vya uongo na havijawahi kutokea. Mfano mdogo kuandika Simba ana vikombe 9 vya muungano na vikombe 5 vya tusker. Yanga ndio miamba wa muungano na Tusker, achana na ivyo vya Nyerere cup na Hedex ivyo havina idadi.
Wewe manara alishawahi kutoka kichwani mwako hata kwa sekunde moja tu?Hatoki akilini mwako 24/7
Mbna hizi takwimu ni za uongo.
Alifungwa kwao bao 2 kwa 1,na akavuliwa ubingwa kwao misri,kama misri sio uarabuni basiMliwafunga hao Zamaleki magoli mangapi? Mimi naongelea kuwatoa hao Waarabu kwa kuwafunga kwenye ardhi yao! Nipe majibu sahihi hapa. Mliwafunga goli ngapi pale Misri?
Maana kama ni ushindi wa kubahatisha wa penati, basi hata Yanga miaka michache iliyopita angeweza kumtoa Al Ahly kwenye ardhi yake kupitia hiyo hiyo mikwaju ya penati. Ni bahati mbaya tu Said Bahanuzi alikosa penati ya mwisho.
Sahihisha na uweke takwimu sahihiUmeweka vitu vingi vya uongo na havijawahi kutokea. Mfano mdogo kuandika Simba ana vikombe 9 vya muungano na vikombe 5 vya tusker. Yanga ndio miamba wa muungano na Tusker, achana na ivyo vya Nyerere cup na Hedex ivyo havina idadi.
Rekodi zako zina mashaka Kaka, inamaana YANGA Hana kombe lolote la Asfc? Bingwa wa mwaka Jana alikuwa ni Nani?Weka zilizo sahihi nakungoja hapa
Vizuri na ndo nilikuwa nataka uje hapo, hv unajua kabla ya kuitwa ASFC lilikuwa inaitwaje Hilo kombe, na unajua Simba na Yanga washachukua mara ngapi kabla halijabadilishwa jina na kuitwa ASFC?? Mbona sijaona kwenye list yako??Soma vizuri?hiyo list ilikuwa ni ya mwaka jana kabla ya fainali ya azam cup