Wewe mzazi unayemtegemea mwanao utalipwa kile ulichomfanyia mzazi wako (karma is real)

Wewe mzazi unayemtegemea mwanao utalipwa kile ulichomfanyia mzazi wako (karma is real)

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
5,715
Reaction score
13,739
Mzazi unataka nikujengee nyumba kubwa nikununulie na usafiri, haya unayoyahitaji kutoka kwangu sijui kama uliwahi kumfanyia mzazi wako hata robo yake, mmekuwa ni watu wa kututishia kutupa laana na hali ya kuwa nyinyi wenyewe wazazi wenu waliwavumilia vituko vyenu mpaka kuwa na familia na kutuzaa sisi.

Sijui ni ubinafsi sijui ndio roho mbaya ila niseme tu mtalipwa kile mlichowatendea wazazi wenu
 
mzazi unataka nikujengee nyumba kubwa nikununulie na usafiri, haya unayoyahitaji kutoka kwangu sijui kama uliwahi kumfanyia mzazi wako hata robo yake, mmekuwa ni watu wa kututishia kutupa laana na hali ya kuwa nyinyi wenyewe wazazi wenu waliwavumilia vituko vyenu mpaka kuwa na familia na kutuzaa sisi....sijui ni ubinafsi sijui ndio roho mbaya ila niseme tu mtalipwa kile mlichowatendea wazazi wenu
Amen
 
Maisha itakuwa yananyoosha vijana sana mpaka hawataki utegemezi tena usioeleweka🤣
maisha ni magumu sana mkuu, mzazi alidhike na kile kidogo nitakachompa....mimi sina uwezo wa kumjengea ghorofa , sina uwezo wa kumnunulia v8 .......ajira zenyewe zimekuwa ngumu kama jiwe, vijana tunakandiwa kila sehemu.
 
😅😅😅😅😅 wazazi wengine Hadi Raha ,juzi kati nipo na bi mkubwa mara sister kapigaa wakaongea weee na bi mkubwa,baadae bi mkubwa kabla ajakata cm anamwambia npo na dogo lako hapa kaja kunisalimiaa,,,sister akaropoka Bora kaja akuachie laki hapo ufanyie matumizi c kuonga tu wanawake wa mjiniii😅..bi mkubwa akamjibu kwani unamuonea wivu akiwaonga hao wanawake wa mjini 😅.bi mkubwa akamwambia mwache kijana ale Hela zake anajua anazipatajee😅😅😅 ,mm nshazeeka Hela za nn tenaa kijana anipeee ,badala afaidi nguvu zakee,,sister akaishia kukata cm...
 
Kwanza wazazi baadhi hawakupenda kuwajali wazazi wao ili watulee sisi Kwa mujibu wao,, maana nilikuwa nikiona maisha wanaishi na kupitia Babu na bibi yalikuwa magumu Sana.

Ila kwakuwa sisi tumejariwa uchumi haina sababu ya kushindwa kuwasaidia wazazi.
 
Kuna vizee vya ajabu sana, vimeponda ujanja, kuzaa mpaka uzeeni nakutakia kuwaachia majukumu ya ulezi na kusomesha watoto wa mwanzo. Unakuta mtu Hana maendeleo kwake kumbe anapambana kufukia machimo aliyoacha mzazi wake.

Vijana wa Sasa msirudie tabia mbovu hii ya wazee wa zamani.
 
Back
Top Bottom