Wewe ni mhenga?

Wewe ni mhenga?

Hahahahahahaha tulikuwa tunajificha kwenye mashamba ya Mahindi na mihogo basi huko kwenye mihogo hatutoki mapema tunachimba na kutafuna juu kwa juu
Hahaha huu mchezo watoto wahuni Walikuwa wana tafunana sana aise. .wakienda kujificha ndio wana zamia huko huko
 
Hahahahahahaha mdako ilikuwa nikianza sikosi kizembe
Hahaaa hatari sana. .ule mchezo mpaka leo sijui kucheza. ... Kuna michezo ilinishinda sana mpaka leo licha ya kuzungukwa na watu walio kuwa wanaicheza. ... mmoja wapo ukiwa ni kucheza karata
 
Hahaha hatari sana ' Aise ni mwendo wa kubadilishana t-shirt tu kwaajili ya kumzubaisha mlinda kopo
Hahahahahahaha tulikuwa tunajificha kwenye mashamba ya Mahindi na mihogo basi huko kwenye mihogo hatutoki mapema tunachimba na kutafuna juu kwa juu
 
Bata wana ndala au ni ndala zilikuwa zinaitwa bata?
Kama ulivaa ndala za bata zikakatika ukaweka mwimba kamba zisichomoke.

Wewe ni mhenga tena uliyeshiriki kutunga methali.
 
Kama wewe ulipiga picha na pozi la dole gumba wewe ni muhenga
 
Kama ulikulaga zile pipi ndefu nyembamba zina mistari alafu zina sukari nyingi wewe ni muheng
 
Hahahah kushika sikio kama mkono haufiki huruhusiwi kuanza la kwanza dah!
Kama umeenda shule kwa kushika sikio na mkono wewe ni mhenga mbobezi.

Kama shuleni umetazamwa kwa kioo na kuambiwa rangi ya chupi yako wewe ni mhenga.

Kuna zile chupi unakuta za rangi moja kama kijani halafu zinavutika kama manati ndiyo mlikuwa mnaziitaje? Usiniulize nimezijuaje
 
Hahahah

Nimeunguza sana sukari jamani
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] sana

Kama umekunywa maji ya kwny mtungi na kikombe cha bati wewe ni muhenga na nusu

Kama umekunywa chai ya kuunguza sukari ( inaitwa twi in one maana umeokoa majani ya chai na sukari pia) ndg yangu wewe ni muhenga
 
Kama umenyoosha nywele kutumia chanuo la chuma wewe ni muhenga
 
Kama ulikua unaweka wadudu fukufuku kifuani kisingizio maziwa yakue makubwa wewe ni muhenga
 
Kama uliruka kamba na ukawa unaimba kantiii kantiii basi jua wewe ni muhenga.
 
Kama ulitumia vitu vifiatavyo hakika wewe u mhenga;

Madaftari yenye cover la Sungura, badae simba, badae sana wakaweka big five

Peni za Bic, Beifa, badae Cello
Ruler za Haco au zile za mbao, nimesahau brand yake

Kichongeo cha duara chenye ka kioo
Saa za mkononi za ASAHI
Viatu aina ya Losso, Manjia
Tai zenye vimulimuli kwa mbele
Majeans brand ya tiger
Mgauni special (ya dukani) yenye vikengele kwa mbele
Pipi sigara
Kanda mbili za Umoja zile nyembamba ngumu (haziishi)
Betri aina ya Bell (zinavuja hatari)
Sabuni za kufulia za Mbuni, Komoa, Mshindi, Skadi
Vitabu vya hadithi vya Mchera ziwani, Kapotei na Lulu, Mji wa Mawe,
Vipindi ITV vya The bold and beautiful, African soccer show, Africa Journal (ya enzi hizo)
Vipindi RTD vya Majira, Twende na Wakati, Zinduka, cheichei shangazi,
.....nitarudi kuendelea.....
 
Back
Top Bottom