Wewe ni mzazi usisahau jukumu lako la kumlea na kumlinda mwanao

Wewe ni mzazi usisahau jukumu lako la kumlea na kumlinda mwanao

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
MHADHARA (106)✍️
Hata kama una majukumu...
1. Mlinde mwanao katika kipindi cha mvua kali. Kamwe asicheze kwenye mitalo ya maji, mabwawa, mito, n.k.
2. Mlinde mwanao dhidi ya ukatili wa kijinsia. Mkague mara kwa mara na umpe elimu.
3. Mlinde mwanao dhidi ya makundi mabaya ya wavuta bangi, wezi, n.k.
4. Mlinde mwanao dhidi ya maeneo hatarishi (mashimo ya vyoo, mashimo ya taka, visima vya maji, n.k).

NB:
👁️
Jenga tabia ya kumtafuta mwanao na kujua alipo (kupata taarifa zake) pindi inapotokea hukumwona machoni kwa muda mrefu (saa nyingi).

👁️ Punguza mazoea ya kuamini kwamba "Yupo kucheza, atarudi". Jiridhishe kama kweli anacheza na wenzake, kwasababu anaweza asirudi milele.

RIGHT MARKER
Dar es Salaam.
 
Back
Top Bottom