Wewe ni wa thamani. Je, watembea katika uthamani wako?

Wewe ni wa thamani. Je, watembea katika uthamani wako?

MR BINGO

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2016
Posts
1,164
Reaction score
2,500
Nianze na hadithi fupi itakayoambatana na swali mwishoni mwake

“Robin ni farasi wa thamani sana aliyeshinda mashindano mbalimbali ya kidunia na amekuwa akipata medali kadhaa na pia anasifika kuwa na umbo bora kabisa la kiushindani ambalo limekuwa likimsaidia kushinda mbio mbalimbali za farasi , Robin amekuwa akitunzwa katika mazingira bora yanayojumuisha mlo bora na sehemu nzuri ya kulala na kufanya mazoezi”

Swali:

Je, ukipata nafasi ya kumnunua farasi Robin utampa matunzo ya kawaida au utampa matunzo anayostahili kupewa farasi ambaye ni mshindi?

Sijajua jamii yako imekuwa ikikuchukuliaje lakini nina uhakika kuwa wewe ni wa thamani na Mungu (au chochote unachoamini kuwa chanzo chako) aliyekuumba aliumba kitu cha thamani swala ni je unatembea katika uthamani wako katika maisha yako ya kila siku?

Stori ya farasi Robin hapo juu inaonyesha jinsi tunavyojiweka ndivyo jamii na watu wanaotuzunguka watakavyotuchukulia na kutupa thamani kutokana na matendo yetu ya kila siku. Kupitia maneno, matendo na imani zetu za kila siku kuhusu mambo mbalimbali yanatujengea au kutubomolea thamani yetu katika jamii, hii inamaanisha kuwa kwa mfano mtu ukiamua kuenenda kama kiongozi, ukatenda kama kiongozi na ukanena kama kiongozi basi jamii na watu wako wa karibu hawatakuwa na namna zaidi ya kukuchukulia kama kiongozi.

Kwa nini basi watu wengi wamekuwa hawatembei katika uthamani wao?

Jibu la swali hili ni rahisi kuwa watu wengi hawaujui uthamani wao nah ii inasababishwa na kuwa na “picha binafsi hasi”(negative self- image)

Picha binafsi (self-image) ni jinsi mtu anavyojichukulia yeye mwenyewe, yaani ukijichukua wewe mwenyewe ukajiweka mbele yako, je ni mtu wa aina gani unayemuona?Je unamuona mtu mdhaifu?Je unamwona mtu asiye na mwelekeo?Je unamwona mtu jasiri mbele yako?Je unamwona mtu mwenye aibu? Je unamwona kiongozi mbele yako?

JIbu la swali hilo hapo juu litakupa kujua jinsi unavyojichukulia. na kwa bahati mbaya tunaishi katika ulimwengu ambao ni hasi hivyo watu wengi wanakuwa na mtizamo binafsi ambao ni hasi pia. Mtizamo huu hujengwa kuanzia kipindi cha mwanzo katika maisha yetu pale ambapo wazazi na jamii zetu zinatuambia mabo mbalimbali kuhusu sisi na hivyo kupandikiza imani katika akili zetu kuwa hivyo ndivyo ulivyo.

Mfano: mzazi anaweza kumwambia mtoto wake “wewe na sauti lako baya hilo hata huwezi kuimba” au mwalimushuleni akakuambia “huyu ana aibu hawezi kuongea mbele za watu”,inawezekana hayo yanayosemwa na jamii au wazazi wetu yanasemwa katika hali ya utani tu lakini yanajenga imani ndani yetu inayotuaminisha kuwa hivyo ndivyo tulivyo. hivyo basi tunaishia kuwa na picha hasi kuhusu maisha yetu hivyo tunashindwa kuijua thamani yetu na hivyo kushindwa kuishi kuendana na thamani yetu.

Ningependa siku hii ya leo ujiulize thamani yako kwa kufanya zoezi la kujitoa wewe na kujiweka mbele yako na kuandika kila unachokiona mbele yako na uandike kila sifa unayoiona kuhusu wewe na uanze kuishi kulingana na thamani yako.

Kumbuka jinsi unavyojichukulia ndivyo unavyotufundisha na sisi kukuchukulia hivyo hivyo, kwa hiyo endapo utajichukulia kama kituko na sisi tutakuchukulia kama kituka na endapo utajichukulia kama mtu wa thamani na sisi tutakuchukulia kama mtu wa thamani uamuzi ni wako

USIJICHUKULIE KAWAIDA WEWE SIYO WA KAWAIDA!
 
In other words ur not special than others.

Unless u prove you are.
 
So Logically;

Binadamu wote ni wa thamani

Mana wote si binadamu/tumeumbwa na Mungu huyo huyo
Yap!!! Binadamu wote ni wa thamani ila ukishakuja duniani wapo watu watakaotaka kukuaminisha kuwa wewe siyo wa thaman na endapo utawaamini basi watakuwa wamefanikiwa kukuondolea thamani yako
 
Back
Top Bottom