Wezi huwa wanafikiria nini kabla hawajaamua kuwaibia masikini wanaopambana kujikwamua na hali duni?

Wezi huwa wanafikiria nini kabla hawajaamua kuwaibia masikini wanaopambana kujikwamua na hali duni?

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Unaweza kujiuliza hili swali kama mimi na huenda usipate majibu yake.

Fikiria mtu upo unapambana ujikwamue kutoka kwenye umasikini, unafuga kuku, mbuzi; unajenga kabanda kako ka kujistiri na mvua, cha ajabu kuna mtu mwingine anawaza kuja kukuibia hata hicho kidogo ulichonacho!

Mwizi ni mwizi tu hata akiiba kuku wa mwenye uhitaji hapaswi kutetewa. Wezi ni watu wenye roho mbaya sana! Tena kwa wale wanaowaibia masikini wanapaswa kuongezewa adhabu!
 
Kila mtu Tanzania ni mwizi katika nafasi yake. Hata wewe. Kwa iyo ukiibiwa potezea tu songa mbele. Cha kufariji hao waliokuibia kuku nao wataibiwa tu na wengine na hao wengine waliowaibia nao watalizwa tu. It is a cycle kausha tu na kupotezea.
 
Unaweza kujiuliza hili swali kama mimi na huenda usipate majibu yake...
Njoo Muhimbili kuna story za wizi wa ajabu.

Wako wezi kila kona. Hizi ni story za kweli pale Muhimbili.

Leo nawapa kubwa kuliko. Mochwari. Kama mnavyojua Serikali yetu inaumdai hadi maiti. Sasa maheremu alikuwa akidaiwa kama 1.7mil, na wafiwa walikuwa na 1mil tu.

Akijitokeza msamaria mwema akisema kama mna hela pungufu leteni nitaenda kuongea na msimamizi mtapata mwili wa mpendwa wenu. Nisubirini kama kdg. Kweli wakamkabidhi.

Ndio ilikuwa kimoja. Kumbe alikuwa mwizi.
 
Kila mtu Tanzania ni mwizi katika nafasi yake. Hata wewe. Kwa iyo ukiibiwa potezea tu songa mbele. Cha kufariji hao waliokuibia kuku nao wataibiwa tu na wengine na hao wengine waliowaibia nao watalizwa tu. It is a cycle kausha tu na kupotezea.

Ila Rashford anakera sana asee.
Hii kauli huwa nawaambia wanafoka kama minyani...
Bongo kila mtu mwizi.

Atakuibia kwa mizani fake
Atakuibia kwa ku over price
Atakuibia kwa uchakachuaji
MBaya zaidi atakuibia muda...utasikia nakuja dakika sifuri...huu ni wizi mtupu
 
CHUNGA TAMAA MBAYA IN 20 ASILIMIA VOICE NYIMBO INA UJUMBE MZITO SANA NISHAWAHI IBIWA WALLET KWENYE DALADALA DAH NIKAPOTEZA VITAMBULISHO VYANGU VYOTE MUHIMU NA WALLET ILI NA MTASHA MMOJA TU KAKI NA BUKU MBILI MBILI TU DAHHH
 
Hao wezi na mafisadi wanaamini mali zoooote ni zao; nyie hapo ni wapangaji tu kwenye nchi yenu.

Ila mara moja moja huwa wanaonesha kahuruma fulani, wao wanakaita kupunguza ukali wa umaskini, ili mwendelee kuwatumikia mabwana kwa hiari na furaha ya kifukara, na wala si kwa shurti. Hapo upo?

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Mtu asiyewahi kuibiwa akiona mwizi anapigwa hua analia kua wanamwonea, hata mimi nilikua hivyohivyo mwanzoni ila saizi hua natamani hata nitoe hela niwape wakanunue petroli fasta wammalize... wezi wanarudisha nyuma guys 😓😭
 
Unaweza kujiuliza hili swali kama mimi na huenda usipate majibu yake.

Fikiria mtu upo unapambana ujikwamue kutoka kwenye umasikini, unafuga kuku, mbuzi; unajenga kabanda kako ka kujistiri na mvua, cha ajabu kuna mtu mwingine anawaza kuja kukuibia hata hicho kidogo ulichonacho!

Mwizi ni mwizi tu hata akiiba kuku wa mwenye uhitaji hapaswi kutetewa. Wezi ni watu wenye roho mbaya sana! Tena kwa wale wanaowaibia masikini wanapaswa kuongezewa adhabu!
Wewe unaongelea vibaka! Vipi wezi sekarini? Hao ndo wabaya kabisa
 
CHUNGA TAMAA MBAYA IN 20 ASILIMIA VOICE NYIMBO INA UJUMBE MZITO SANA NISHAWAHI IBIWA WALLET KWENYE DALADALA DAH NIKAPOTEZA VITAMBULISHO VYANGU VYOTE MUHIMU NA WALLET ILI NA MTASHA MMOJA TU KAKI NA BUKU MBILI MBILI TU DAHHH
Unatembea na vitambulisho vyote kwani wewe ni mkimbizi.
 
Back
Top Bottom