Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Wakati nipo mdogo chekechea tulikuwa tunakunywa chai shuleni. Sasa bibi yangu alikuwaga ni nesi hospitali. Kule hospitali alikuwa anafanya kazi kitengo cha lishe ya watoto. Ilikuwa kila jioni anarudi na maziwa na mikate tunajichana. Sasa siku moja amerudi na mkate wakasema ungine utunze utanywea chai shuleni. Nikalala na usongo wangu wa mkate. Asubuhi nikaenda nao shuleni na kuuweka hadi muda wa chai. Tumeenda kucheza, tumeitwa muda wa chai, kucheki kwenye mfuko mkate umebaki chenga chenga tu😭😭😭😭 roho iliniuma sana siku ile, iliniuma sana.
Itakuwa ni mijamaa ya madarasa ya juu ilipita nao. Wezi ni watu wa hovyo sana.
Itakuwa ni mijamaa ya madarasa ya juu ilipita nao. Wezi ni watu wa hovyo sana.