Wezi ni wa kuchoma moto kabisa

Wezi ni wa kuchoma moto kabisa

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Wakati nipo mdogo chekechea tulikuwa tunakunywa chai shuleni. Sasa bibi yangu alikuwaga ni nesi hospitali. Kule hospitali alikuwa anafanya kazi kitengo cha lishe ya watoto. Ilikuwa kila jioni anarudi na maziwa na mikate tunajichana. Sasa siku moja amerudi na mkate wakasema ungine utunze utanywea chai shuleni. Nikalala na usongo wangu wa mkate. Asubuhi nikaenda nao shuleni na kuuweka hadi muda wa chai. Tumeenda kucheza, tumeitwa muda wa chai, kucheki kwenye mfuko mkate umebaki chenga chenga tu😭😭😭😭 roho iliniuma sana siku ile, iliniuma sana.

Itakuwa ni mijamaa ya madarasa ya juu ilipita nao. Wezi ni watu wa hovyo sana.
 
Basi nitakunulia sambusa za nyama na bagia.
 
Kwa uzi huu, hiyo ID haikufai badili jina
 
Sasa vipi hawa wezi tunaowapigia kura kabisa..?
 
Mkuu Inaonekana Uliumizwa Sana Na Kitendo Kile Maana Hadi Sasa Umekuwa Mzee Ila Unakumbuka Yote.
 
Mkuu Inaonekana Uliumizwa Sana Na Kitendo Kile Maana Hadi Sasa Umekuwa Mzee Ila Unakumbuka Yote.
Yah, kiliniuma sana. Umeenda kucheza ukijua kuwa wakati wa chai unamkate wako halafu unakuta crumbs tupu!!
 
Wakati nipo mdogo chekechea tulikuwa tunakunywa chai shuleni. Sasa bibi yangu alikuwaga ni nesi hospitali. Kule hospitali alikuwa anafanya kazi kitengo cha lishe ya watoto. Ilikuwa kila jioni anarudi na maziwa na mikate tunajichana. Sasa siku moja amerudi na mkate wakasema ungine utunze utanywea chai shuleni. Nikalala na usongo wangu wa mkate. Asubuhi nikaenda nao shuleni na kuuweka hadi muda wa chai. Tumeenda kucheza, tumeitwa muda wa chai, kucheki kwenye mfuko mkate umebaki chenga chenga tu[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24] roho iliniuma sana siku ile, iliniuma sana.

Itakuwa ni mijamaa ya madarasa ya juu ilipita nao. Wezi ni watu wa hovyo sana.
Mkuu! Huu ujumbe wa wezi umeuuleta kwa njia ya code! na ni wachache sana humu watakao kusoma na kukuelewa!!
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Nakumbuka tuko advance kuna dogo bonge akaletwa kuanza fm1 ,walivyo mdekeza home wakamkaangia nyama kindoo cha lita kumi kimejaa eti hawezi kula maharage.
Dogo kutoka kidogo tu kurudi anakabidhiwa ndoo yake haina hata kipande cha mnofu.
Mungu anisamehee kwenye ule upigaji
 
Red Giant said:
Wakati nipo mdogo chekechea tulikuwa tunakunywa chai shuleni. Sasa bibi yangu alikuwaga ni nesi hospitali. Kule hospitali alikuwa anafanya kazi kitengo cha lishe ya watoto. Ilikuwa kila jioni anarudi na maziwa na mikate tunajichana. Sasa siku moja amerudi na mkate wakasema ungine utunze utanywea chai shuleni....

Kibongo bongo na kishule shule hao huwa wanaitwa wadokozi...

Swali la kizushi, je bibi yako huko hospitali naye alikuwa anapewa au anadokoa hayo mazagazaga aliyokuwa akirudi nayo maskani?
 
Kibongo bongo na kishule shule hao huwa wanaitwa wadokozi...

Swali la kizushi, je bibi yako huko hospitali naye alikuwa anapewa au anadoko hayo mazagazaga aliyokuwa akirudi nayo maskani?
Mama kasema kuvimbiwa ndiyo kosa.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Nakumbuka tuko advance kuna dogo bonge akaletwa kuanza fm1 ,walivyo mdekeza home wakamkaangia nyama kindoo cha lita kumi kimejaa eti hawezi kula maharage.
Dogo kutoka kidogo tu kurudi anakabidhiwa ndoo yake haina hata kipande cha mnofu.
Mungu anisamehee kwenye ule upigaji
Dogo atakumbuka na kuumia hadi kaburini.
 
Mama kasema kuvimbiwa ndiyo kosa.
Kila Mtu ale kwa urefu wa kamba yake,hakuna kuingiliana kwenye ulaji!! Huyu Mama ndiyo Rais mzuri anaachia wenye nguvu wafanye wanavyotaka!! Rule of the Jungle "kila mnyama atakula kwa urefu wa kamba yake!!
 
Lakini umesahau pia bibi hosptali lishe ya watoto anakuja kuwalisha ninyi.
 
Back
Top Bottom