Wezi waiba silaha ofisi za TAKUKURU

Wezi waiba silaha ofisi za TAKUKURU

Tanga. Watu wasiojulikana wamevunja mlango wa ofisi ya Kamanda wa Takukuru wilayani Handeni na kuiba bastola mbili zilizokuwa na jumla ya risasi 21.

Habari zilizolifikia Mwananchi jana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Henry Mwaibambe zinasema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana, baada ya watu hao kutumia funguo bandia kufungua mlango wa mbele wa jengo hilo, kabla ya kuingia ndani na kuvunja mlango na sefu iliyokuwa imehifadhi bastola hizo aina ya Beretta, moja ikiwa na risasi 16 na nyingine tano.

“Wafanyakazi walipofika ofisini, wakakuta mlango uko wazi na ofisini kwa kamanda kumevunjwa, walipoingia ndani wakakuta kasiki (sefu) ya kuhifadhia fedha ikiwa wazi na silaha hizo zimechukuliwa,” kilisema chanzo chetu ambacho hakikutaka kutajwa gazetini.

Akizungumza na Mwananchi ofisini kwake, Kamanda Mwaibambe alisema tayari ametuma maofisa wake kufuatilia hatua kwa hatua tukio hilo.

“Wameiba bastola mbili zote aina ya Beretta, moja ikiwa na risasi tano na nyingine ikiwa na risasi 16, ndani kulikuwa na silaha nyingine aina ya shotgun, lakini hawakuichukua,” alisema Mwaibambe.

Hata hivyo, alisema tayari wanamshikilia mlinzi wa mgambo aliyekuwa akilinda jengo hilo, ambaye polisi wamegundua hakuwa mwajiriwa wa Takukuru, bali alimshikia mlinzi halisi ambaye yupo likizo.

“Bado timu yangu ipo Handeni ikiongozwa na msaidizi wangu (mkuu wa upelelezi wa mkoa) inafanya uchunguzi wa tukio hili, tutalitolea taarifa rasmi baada ya uchunguzi,” alisema Kamanda huyo.

Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Takukuru mkoani Tanga, Zainab Bakari alishindwa kukataa wala kukubali kutokea kwa tukio hilo, bali alisema kwa mujibu wa taratibu zao, hapaswi kulizungumzia.

“Kama unavyojua taratibu za vyombo vya usalama, mimi bado sitakiwi kueleza chochote na sina taarifa kamili, nitakapokuwa na taarifa baada ya ziara ya mkuu wa mkoa, basi nitazitoa au zitatolewa na mkurugenzi wetu,” alisema kamanda huyo ambaye alidai yupo kwenye ziara ya mkuu wa mkoa wa Tanga, Omary Mgumba.

Mwananchi lilimtafuta Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru nchini, Salum Hamduni ambaye alisema suala hilo linazungumziwa na polisi kwa sababu “matukio ya uhalifu wa silaha yanaangukia Jeshi la Polisi. Tukio la kihalifu wenye mamlaka ni polisi.”

Alipoulizwa nani wanalinda ofisi za Takukuru, Hamduni alisema, “zinalindwa na walinzi, sasa ni kutoka wapi ni suala la mfumo.”

Mwananchi
Ukiona wakwepa hivyo ujue wahusika ni wao
 
Watu wasiojulikana wamevunja mlango wa ofisi ya Kamanda wa Takukuru wilayani Handeni na kuiba bastola mbili zilizokuwa na jumla ya risasi 21.

MWANANCHI
Wanachadema wa Tanga muwe makini wanataka wa kulibebesha zigo hilo.

Ukiweza mimbia kabisa Mkoa japo Mwaka usiwepo mtaani.
 
wahusika wakuu katika hili ni maafisa wa TAKUKURU.
Wezi walipata wapi sample za funguo
walijuaje silaha zinapokaa?
Haya mambo ya kulewa na kutoa siri za ofisini ni ushamba mtupu
 
Tukiwa jeshini ukipoteza silaha ilikuwa inakuwa shughuli kweli, hadi vyoo mtavunja na kukoroga kinyesi. Yaani kupoteza silaha ya serikali na kuweka uwezekano kwamba itaua raia ilikuwa ni dhambi ambayo tulipaswa kuielewa sana!

Sasa hawa Takukuru, wengi hawajapitia hata jeshini, wakifanyishwa hivyo silaha zao hazitaibiwa tena. Waambieni kuna tetesi hizo silaha zimefichwa vyoo vya Handeni mjini wakatafute
 
Silaha inapolala lazima kuwe na ulinzi ,centry ajile usiku kucha ,hii tabia ya kila idara kuitwa jeshi inakwenda kuigharimu nchi, Tfs jeshi, migration jeshi,Tanapa jeshi, takukuru jeshi, Konde bouy naye jeshi,tutafika tumechoka mno
Hii inaitwa inside job. Hivi Bujibuji Simba Nyamaume niko huku Itumbili Magu, nawezaje tu kuja huko kwenu nikaiba si
 
Tanga. Watu wasiojulikana wamevunja mlango wa ofisi ya Kamanda wa Takukuru wilayani Handeni na kuiba bastola mbili zilizokuwa na jumla ya risasi 21.[emoji23]
 
Back
Top Bottom