Wezi waliojifanya maafisa wa polisi, wamepora pesa kwenye gari la kubeba Pesa huko Italia

Wezi waliojifanya maafisa wa polisi, wamepora pesa kwenye gari la kubeba Pesa huko Italia

mcTobby

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2018
Posts
7,894
Reaction score
22,679
Tukio hili limetokea mchana kwenye barabara moja huko Italia baada ya wezi kuisimamisha gari ya pesa na kuipora.. wawili wamekamatwa...

Tukio hili limenikumbusha filamu moja ya Money heist inayoitwa HEAT
==============
Genge lenye silaha limefanya shambulio la mchana kwenye gari la kusafirisha fedha lenye ulinzi kusini mwa Italia leo asubuhi. Shambulio hilo lililenga gari la BTV kwenye barabara kuu ya SS 613 kati ya Lecce na Brindisi, karibu na njia ya kutoka ya Tuturano katika eneo la Puglia.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Italia, takribani watu 8 wenye silaha, baadhi yao wakijifanya polisi na kutumia taa za kuashiria, walizuia barabara kwa kuchoma magari moto. Washambuliaji walitumia vilipuzi kulipasua gari hilo na kulikuwa na mabadilishano ya risasi kati yao na askari wa Carabinieri waliowasili eneo la tukio.

Hakuna majeruhi wala vifo vilivyoripotiwa. Watuhumiwa wawili walikamatwa wakati wa jaribio la kutoroka.

 
Italy wana mambo mengi sana hao jamaa ukute ni mchongo kabisa huo hao jamaa waliwahi kuwa na kesi za kupanga matokeo ligi nzima mpaka anapatikana bingwa kwa sababu ya Kamari..
 
Italy wana mambo mengi sana hao jamaa ukute ni mchongo kabisa huo hao jamaa waliwahi kuwa na kesi za kupanga matokeo ligi nzima mpaka anapatikana bingwa kwa sababu ya Kamari..
Mafia state ile.. ma don
 
Sasa hivi kuna wimbi kubwa la uhalifu ulaya, juzijuzi kuna tukio la uhalifu limetokea Ufaransa.
 
Back
Top Bottom