Wezi wamevunja fremu na kuiba, sijui naanza hatua gani hapa wakuu. Naombeni msaada wenu

Yaani umeibiwa Nini ambacho kitakwamisha shughuli zako na ni msaada Gani unataka?

Watanzania kujielezea bado ni shida kidogo. Pole sana lakini
 
Yaani umeibiwa Nini ambacho kitakwamisha shughuli zako na ni msaada Gani unataka?

Watanzania kujielezea bado ni shida kidogo. Pole sana lakini
Msaada naotaka ni wa kimawazo je nifanye nini na nianziw wapi ili niweze kupata vitu vyangu.

Kingine mpaka mda hu tayari nisharipoti polisi
 
Watu wana deal nawee, hadi useme aunt Dorry kapata wapi pesa za kukuanzishia biashara.

Unalo hili, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Wewe coca kesho nakuja huko huko mpaka nikuoneshe
 
Poor Brian unoanekana ni wale vijana wachanga wadogowadogo..namana unavyoandika inanonesha

Umeonesha Rb ya polisi halafu unasema bado polisi hujaripoti halafu uende na Nini na nini

Location yako ni gomz biashara Iko hapo na ndio makazi yako then unaamwambia mtu utamtania pm😊

Kama ni kweli umeibiwa usisumbuke na polisi,kama gharama ni lkai 5 piga moyo konde,utazipata.tena maana polisi watatka pesa usaidiwe,hawatoki bure.sa utajikuta umemmaliza laki tatu kurejesha laki tano.na Ukute vingine vishauzwa.pole Kwa huu mtihani
Ukiweza hama hapo.vijana wengi wa maeneo ya uswahilini ni wezi
 
Aaaah mkuu ni kweli mi ni kijana mdogo mdogo japo namiliki mashangazi...

Kuhusu suala la rb na polisi zile ni updates ambazo nilikua natoa kila baada ya mda..

Yaani uzi ulikua unaendelea huku na mimi naenda polisi kufanya harakati.

Nilipopata rb nikatuma humu maana kuna watu walishaanza kusema chai.

Nachoshukuru mpaka sasa hakuna nilichopata ila kuna member humu yupo bega kwa bega na mimi hapa katika kunisaidia kufanikisha hili jambo..

Nitafanikisha vipi..? Hili ni swali hata mimi najiuliza ila naimani nitafanikiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…