Wezi wanazidi mitaani, wanaiba mchana kuliko usiku kuweni makini

Wezi wanazidi mitaani, wanaiba mchana kuliko usiku kuweni makini

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Kwa jinsi maisha yanavyozidi kuwa magumu, kumeibuka kundi la wezu wengi wao wadogowadogo vitoto kabisa ambavyo vinaiba sana Pesa Na vitu vidogo kama simu.

Wanachofanya, wanajua nyumba nyingi za kupanga mida ya mchana hukuti watu wameenda kwenye mihangaiko yao. Unakuta nyumba mchana ipo kama Kanisa, kimyaa, aliyepo asiye na kazi amejifungia anacheki movies.

Wezi wanavunja mlango, wana-search, na kwa sababu watu wanaogopa makato makato kila utoapo hivyo wanaficha cash ndani; usipendelee kuweka pesa kwenye kabati au kitanda. Kwanza ni hatari, zikiliwa Na panya je?

Kama una kibunda chako hutaki kukiweka bank au kwenye simu basi bora uzimwage kwenye kapeti kwa chini humo wezi sio rahisi kunusa.
 
Back
Top Bottom