What is the biggest lie you have ever told Or heard on JF?

Daby

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2014
Posts
33,894
Reaction score
76,810
Tuachane na kizungu maana wengi tutashindwa kujieleza.....

JF watu tunafanganya saana....wengine huenda mbali na kuvaa uhusika usio wao hasa PM....

Utakuta mtu anamuimbisha mdada PM atamtajia vyeo na mafanikio yote hadi vyeo vyote vitaisha.

Waafrika utaratibu wa kufunguka huwa hatuna ila leo mtajaribu.

Ni uongo gani ulishawahi kuutoa hapa JF hadi mwenyewe ukajiambia kweli hapa nimepitisha mipaka ya udanganyifu.

Kuna uongo ambao hadi unamuuma mwoongo mwenyewe.

Mimi uongo wangu mkubwa hapa JF....ni niliwahi kutoa utambulisho wa uongo kwa dada yangu mmoja ila baadae nikaona aibu nika-confence.

Jukwaani alidhani tunakaribiana kiumri kuja kumuuliza mwenzangu anatofautiana miaka mitatu na mama yangu. Ikabidi nami nikiongeze kiaina umri na kumtumia picha ya jirani yangu ambaye ni mzee.

Sasa siku nakaribishwa kwake nikawa namzungusha wee hadi nikaja kuusema ukweli....

[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]JF kuna watu wazima hata wewe mwenye 45 yako unajiona mzima ila kuna watu wazima zaidi yako.
 
Kuna yule mmoja aliniambia PM baba yake ni Ridhiwan Kikwete kwa hiyo nisiwe na shida kwenye suala la pesa
Akasema atakuwa ananipa 300K kila siku kama nitakubali kuwa nae

Badae nikaja kujua ni kapuku mwenzangu anasoma zake hapa MUHAS
 
Dah Nimecheka kwa sauti sana , mzee mmoja hapa jukwaani kuna mambo alinicheki PM tuyaweke Sawa kutokana na huku niliko, saa ngapi siku moja asinipange ati yeye ni wale wa IDARA PENDWA, nilimcheka sana mpaka akaniomba msamaha, akaniblock kote , ila dingi popote ulipo kama unasoma hii komenti issue yako nilifanikisha ila punguza uongo mbaba.

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Kuna uongo nausikilizia hapa ngoja kwanza [emoji736].
Unanifuatilia kwa ukaribu mno.

Nitarudi
Kumbe wewe bibi Chakorii

Ulipokuwa member mpya ulikuwa rafiki yangu saana humu jukwaani ila sikuhizi naona vibopa vya JF vishakuopoa......

Hata nyuzi zangu hulike tena.
 
Kuna uongo nausikilizia hapa ngoja kwanza [emoji736].
Unanifuatilia kwa ukaribu mno.

Nitarudi
Kumbe wewe bibi Chakorii

Ulipokuwa member mpya ulikuwa rafiki yangu saana humu jukwaani ila sikuhizi naona vibopa vya JF vishakuopoa......

Hata nyuzi zangu hulike tena.
 
Kuna yule mmoja aliniambia PM baba yake ni Ridhiwan Kikwete kwa hiyo nisiwe na shida kwenye suala la pesa
Akasema atakuwa ananipa 300K kila siku kama nitakubali kuwa nae

Badae nikaja kujua ni kapuku mwenzangu anasoma zake hapa MUHAS
Hivi wewe haujawahi kunidanganya....nadhani mimi nimewahi kukudanganya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…