Tuachane na kizungu maana wengi tutashindwa kujieleza.....
JF watu tunafanganya saana....wengine huenda mbali na kuvaa uhusika usio wao hasa PM....
Utakuta mtu anamuimbisha mdada PM atamtajia vyeo na mafanikio yote hadi vyeo vyote vitaisha.
Waafrika utaratibu wa kufunguka huwa hatuna ila leo mtajaribu.
Ni uongo gani ulishawahi kuutoa hapa JF hadi mwenyewe ukajiambia kweli hapa nimepitisha mipaka ya udanganyifu.
Kuna uongo ambao hadi unamuuma mwoongo mwenyewe.
Mimi uongo wangu mkubwa hapa JF....ni niliwahi kutoa utambulisho wa uongo kwa dada yangu mmoja ila baadae nikaona aibu nika-confence.
Jukwaani alidhani tunakaribiana kiumri kuja kumuuliza mwenzangu anatofautiana miaka mitatu na mama yangu. Ikabidi nami nikiongeze kiaina umri na kumtumia picha ya jirani yangu ambaye ni mzee.
Sasa siku nakaribishwa kwake nikawa namzungusha wee hadi nikaja kuusema ukweli....
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]JF kuna watu wazima hata wewe mwenye 45 yako unajiona mzima ila kuna watu wazima zaidi yako.
Hahah ..Nilidanganya sana
Kwa wanaume wote waliokuja PM
Wote nilidanganya....
Na ukweli ni kwamba....
Ngumu sana kuacha.....
Ni tamuuu.... [emoji28][emoji39][emoji39][emoji39]
Hahah ..
Mimi pia nadanganya saana...JF unaweza ukawa unachat na ID 4 za mtu mmoja.
Ninaweza hata kumuomba mtu awasiliane na wewe kwa ajili yangu.
Yes bibi chakoriiKumbe wewe bibi Chakorii
Ulipokuwa member mpya ulikuwa rafiki yangu saana humu jukwaani ila sikuhizi naona vibopa vya JF vishakuopoa......
Hata nyuzi zangu hulike tena.
Nilikuwa natania bhana...Yes bibi chakorii
Nakukumbuka mchango wako sana Daby na Siwezi kuusahau kabisa naomba uamini my dear.
Sikubadilika kwako na wala sitobadilika isipokuwa niliona nikupe nafasi lakini pia kuna wakati ulikuwa hauko hewan kabisa.in short haikuwa active jf.
Nakukumbuka sana.niliijua jf browser kupitia wewe
Siwezi kukusahau kabisa.
Hiyo nchi uliyopo sasa hivi uko salama?ninaimani hauko ukraine wala urusi
Mama nani yule wa kipindi kila sijui yuko salama?
Ulikuwa unamaanisha 😂😂Nilikuwa natania bhana...
Mie nipo majukumu tu yanabana.....nipo nyumbani.
Yupo bado tunadunda tu.
[emoji3][emoji3]
Kwema lakini! Hopefully.... you are enjoying your time?
Nimekusamehe... usirudie tena.Uongo niliodanganya humu siwezi hata kuandika. Muhusika anisamehe tu (katika mahusiano).Na nimeacha hayo mambo
Hahah.. Asante bibieNimekusamehe... usirudie tena.
🤣🤣🤣 daaaah!!Kuna yule mmoja aliniambia PM baba yake ni Ridhiwan Kikwete kwa hiyo nisiwe na shida kwenye suala la pesa
Akasema atakuwa ananipa 300K kila siku kama nitakubali kuwa nae
Badae nikaja kujua ni kapuku mwenzangu anasoma zake hapa MUHAS
Mfano nani alihongwa buku 2? 🤔Buku 2 tuu🤣🤣🤣🤣 na wengine ata hao wakuwahonga hawana...muulize Kelsea akwambie