What is Wrong with Tanzania?!. Tunashindwa Nini Kufikisha Bidhaa Zetu Kwenye Masoko ya Kimataifa?!.

Bila ccm kuondoka madarakani usitarajie jipya!!
Inawezekana ccm wabovu lkn mbadala wa ccm bado hakuna kwa sab waliokuwepo ni wabovu kuliko ccm. Kwa mfano mamvi ndiye ataleta madiliko? Anayetaka urais ili amkomeshe kikwete? Mtu aliyethibitishwa kuwa ni fisadi na chombo chenye mamlaka kikatiba? Au chadema chama cha kifamilia? Au cuf chama chenye makundi? Tanzania upinzani wenye uwezo wa kutawala nchi bado haujatokea.
 
Siku hizi inaitwa TanTrade
Tatizo sio tantrade ni sisi mtanzania mmoja mmoja hatuna mwako wa kutafuta fursa za nje na kutafuta taarifa sahihi kwa watu kama hawa tantrade. Pia ni wavivu linapokuja suala la kukidhi viwango vya kimataifa tunaona kama mzigo mzito maana tunapenda vitu rahisi na njia za mikato. Ndio maana hivi hivi vyetu Wakenya wananunua wanaboresha kukidhi viwango wanauza ulaya
 
Hili ndio jibu mkuu! Hayo mengine hayana maana! Na ndio mpaka sasa tunaendelea kuona uozo na maigizo ya kutosha!! Tutangoja sana! So far nawapongeza sana India na South Africa kwa kuwa wauzaji bora wa tanzanite!
Usirudie kuedit comment yangu plz
 
1. Hatuna mtaji wa kutosha
2. Bidhaa zetu duni/Hatuziongezi thamani kukidhi viwango vya Kimataifa
3. Kizingiti cha lugha/Language barrier(Kizungu hatujui vizuri,kiarabu hatujui vizuri,Kifaransa ndo kabisaa)
4. Hatuna Middle men/women wenye udiriki, wengi wamezoea kutupiga tu humu soko la ndani

BIDHAA TUNAZO...Njombe pale kuna Apple fruits nzuri sana ila zinauzwa na akina mama kwenye mabasi na nyingine zinaoza, Mufindi Muheza kote huko kuna Matunda ya kila aina na kwingineko Tz.
Maua tunayo.
Tukuyu Parachichi mbegu bora zipo ila zinaozea chini
Nyanya Ilula zinazalishwa na eneo linasapoti kila varieties lakini hatuwezi kuuza nje etc...Elimu,Elimu,Elimu
 
Hatuna mtaji wa kutosha wakati tunanunua mapangaboi kwa cash??
 
Hakuna sapoti kutoka kwa serikari kwenda kwa mkulima au mfanya biashara, viongozi husika hawajari wakulima/wafanya biashara zaidi ya kumpendelea mgeni kwani kuna pesa wanapata. Mfanya biashara au mkulima ili upeleke bidhaa zako nje kuna vikwazo vingi hasa vya kipesa kwasababu itakubidi utoe sana pesa.
 
Hii ni hoja yenye mashiko.
 
Mkuu Mkaruka, anzisha basi huo mjadala wa maana, na sisi tutachangia na kuisifu serikali yetu, badala ya kuiponda!.

Paskali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…