What is Wrong with Tanzania?!. Tunashindwa Nini Kufikisha Bidhaa Zetu Kwenye Masoko ya Kimataifa?!.

Ni ukosefu wa mitaji pengine,
Mitaji sio tatizo mkuu.
Kuna watu wana pesa lakini hawajui wazifanyie nini. Tatizo ni elimu yetu imetuandaa kuajiriwa hivyo wengi wetu hatuangalii fursa zilizopo ndani na nje ya nchi.
 
Mazao ni malighafi na malighafi tunazo nyingi, ishu ni ubora wa bidhaa tunazozalisha kutokana na hizo malighafi.

Je, bidhaa zetu zimekidhi viwango vya kimataifa kiasi cha kuleta ushindani kwenye soko la kimataifa?
IN TIME BE POSITIVE!
 
Wewe Chikundi hebu acha kujiabisha kwa hoja za kijinga, unawaharibia CCM zaidi . . , kama huwezi kujadili kacheze mdako . .
Wapinzani hawa wa kutegemea Tungo za mitandaoni hawawezi kufanya lolote zaidi ya kuinyonya na kuirudisha nyuma tanzania hatua zaidi ya 100000. Wasipobadilika kama CCM wanavyojaribu kujibadili wataendelea kutofaa hadi siku ya kiyama.
 
Ndio nimekubaliana na Paschal kuwa ccm ni mbovu sana lkn upinzani zaidi hivyo hatuna mbadala kwa sasa .

Umeuliza Nina ushahidi gani kuwa vyama vya upinzani haviwezi kwa sab havijawahi kushika nchi. Lkn kabla sijajibu kwanini sidhani hata wewe kama unaweza kujibu umejuaje kama upinzani utaweza bali unaamini kutokana na failure ya ccm kwenye nyanja kadhaa bali hujui chama kinavyoendesha mambo yake ni picha tosha ya kukihukumu kama kinaweza kuongoza nchi ama la.

Tukianza kwenye Mfumo.
Chadema ni chama cha kifamilia ushahidi unaonyesha mwenyekiti wake wake wa kwanza mtei alimuachia uenyekiti Shemeji yake Bob makani kisha akaagiza apewe mkwe wake baada ya Shemeji kufariki na mpk sasa yupo kwa miaka 14.

Mfumo kama huu lazima utajitokeza pia kwenye utawala wa nchi kitu ambacho ni hatari.

Tuje kwenye kusimamia katiba

Wameshindwa kusimamia katiba na makubaliano mbali mbali kuanzia chadema mpk ukawa

Wamembrand lowassa kama fisadi nchi nzima kwa miaka minane lkn all of the sudden wakasema ni msafi na kumpa nafasi ya kugombea urais huku wakikiuka katiba yao wenyewe kwani inasema kabla ya mwanachama hajagombea urais lazima afikishe miezi sita chamani lkn lowassa alikaa wiki moja tu chamani akapewa nafasi ya kugombea urais bila mchakato wowote. Hii ikapelekea wakongwe wawili Dr slaa na lipumba kujiengua.

Lkn vyama vilikiuka makubaliano yao kuwa ndani ya ukawa majimboni watoe mgombea mmoja lkn walishindwa kufanya hivyo matokea yake majimbo ya Masasi na ukonga walisimamisha zaidi ya mgombea mmoja.

Nao Cuf baada ya kuvunja sheria ya kujitangazia ushindi wakasusia uchaguzi uamuzi ambao unawatesa wanacuf wa znz mpk Leo kwani wamekosa wawakilishi ambao ni chaguo lao hakuna asiyejua pemba wamekuwa wakiwakilishwa na cuf tokea vyama vingi vianze. Hii yote ni sab ya ubinafsi.

Hali imejidhihirisha kwa uongozi wake wa juu kugombea ofisi vyeo na ruzuku.

Sasa vyama kama hivi unavipa uongozi wa nchi nzima kwa mazingira gani? Ubunge sawa sio urais.
 
Hii ni hoja inayostahili kujadiliwa kwa kina kitaifa. Nafikiri sababu moja wapo ni ya kihistoria fikiria kuna wakati ilikuwa hata kijijini (baadhi) huruhusiwi kufanya ujasiriamali hata wa mgahawa tu, kila kitu kifanywe na kijiji, ubunifu ulifubazwa. Mazingira ya uthubutu na ubunifu ni hafifu sana kuanzia shule za msingi hadi taifa. Badala ya kuweka kipaumbele katika katika vitu kama mashindano mathalani ya urembo miss so and so ingekuwa mashindano ya ubunifu wa uzalishaji na teknolojia kuanzia kijijini hadi Taifa na Mheshimiwa Rais anatoa tuzo kwa watu au taasisi waliofanya au zilizofanya ubunifu wenye tija kila mwaka. Ni shule chache zinaendesha debate (mambo mbalimbali ikiwemo biashara za ndani na nje) hivyo vijana wanashindwa kuendeleza stadi za kukabiliana na changamoto za kitaifa na kidunia. Udhaifu huu pia unasababisha raia kulalamikia serikali kila siku kwa kila jambo ningefurahi ifike siku serikali ishangae mbona raia sio lialia tena, kila changamoto wanajiongeza kama akili zimehama!
 

[emoji115]

SASA, HOJA YA PASKALI KUHUSU EXPORTS HAPA HAIJAJIBIWA, ILA UMEENDELEZA SARAKASI KAMA KAWAIDA YENU CCM.
MMEFILISIKA KIAKILI, NI WIZI TUU . . , NA ROHO MBAYA . . !
TUKIENDELEA NANYI HATUTAWEZA KUFANYA LA MAANA NCHI HII . .
 
[emoji115]

SASA, HOJA YA PASKALI KUHUSU EXPORTS HAPA HAIJAJIBIWA, ILA UMEENDELEZA SARAKASI KAMA KAWAIDA YENU CCM.
MMEFILISIKA KIAKILI, NI WIZI TUU . . , NA ROHO MBAYA . . !
TUKIENDELEA NANYI HATUTAWEZA KUFANYA LA MAANA NCHI HII . .
Hoja imejibiwa kuwa ccm imefeli
 
Pasco Kuna sababu ngingi na nitayaja chache sana.
1. Watanzania hatujawahi kuwa siriasi hata siku moja. Tuko siriasi kwenye kulalamika kwa Gavament.

2. Mentality ya ujamaa still inatusumbua sana bado haijatoka vichwani mwetu, ujamaa ni kuamini kwamba Serikali inatakiwa ifanye kila kitu. Hushangai mtu anafuga kuku halafu anaomba Serikali imtafutie soko?

3. Maisha bado hayajatushika ila kwa hii awamu nazani Watanzania tutafungua Turubo zetu.
Ukiangalia nchi kama Kenya kule wale jamaa hakuna cha Shangazi wala mjomna wala kaka wala Dada yaani ni wewe pekee.Wakenya wanapambana kwa sababu hakuna wakukusaidia make kila mtu ana beba mzigo wake. Hawana altenative ya maisha so ili afanikiwe lazima apambane kiume.

Tanzania bhana mtu anajua atakula na atalala tu so hakuna kujisumbua.

5. Exposure, Wakenya wamesambaa sana Duniania na wale jamaa wana umoja balaa, wanasaidiaiana sana, kwenye furusa.

Watanzania tunarudishana nyuma wenyewe kwa wenyewe.

Mwisho.

Serikali, Kwa kweli mchango wake hauwezo kwepeka, Taasisi nyingi ziko kimasirahi sana TBS wako kimasirahi yao ukiensa TRA wako kwenye kukomoa, sijawahi ona TRA hata inawatembelea wafanya biashara na kuwauliza changamoto zao na jinsi wanavyo weza kutatua. TRA wako bise kukusanya kodi.
Rushwa na upigaji.
 
Hivi Paskali hufahamu kuwa Kenya na Tanzania ni nchi mbili tofauti kiuchumi? Tanzania ni nchi ya kijamaa na Kenya ni nchi ya kibepari. Buy/process/pack and sell or manufacture/pack and sell ndiyo mfumo wa kiuchumi Kenya(ubepari). Sisi Tanzania ni Lima/zalisha then mpe dalali auze.(ujamaa). Chukulia mfano zao la chai. Nchi ya Burundi inauza chai kwenye soko la dunia, lakini Tanzania chai wananunu Wakenya na kwenda kuiuza soko la dunia. Akili zetu ni za kidalali tuu
 
Mkuu mimi ninachofahamu, kwanza sisi wenyewe hatuthamini vya kwetu. Hili tuliache kwanza.
Mkuu, nadhani hili tatizo ni la kutokua na mwamko wa fulsa za kibiashala za kimataifa akiwemo mtoa mada mwenyewe.
Hakuna wa kukaumiwa hapa, ni sisi wenyewe tunashindwa kujiongeza mbali ya serikali kujitahidi kutafuta fulsa mbalimbali
 
Kuna taasis za serikali hazijui kazi zake mfano BET
No, hiyo isue ni ya sisi wananchi, na mfumo wetu wa utawala. Viongozi wetu hawana tofauti na sisi wananchi wa kawaida wote ni madalali tuu. Mwananchi akiamka na kupambana kiuchumi, organs za kiserikali ni kuasidia kutimiza malengo na juhudi za mwananchi
 
Ni ukosefu wa mitaji pengine,
Ishu sio mitaji, ishu ni matangazo ya biashara (marketing) na lugha pia. Alafu Kingine Customers care tupo nyuma sana. Na ndio maana mahotel mengi wanataka kuajiri Wakenya kwa sababu wanafundishwa customers care.
Tanzania katika marketing tupo nyuma sana
 
Uko sahihi kabisa tumefeli kwenye eneo hili mfano halisi niliwahi kuomba BET wakati huo nafasi ya kwenda kwenye exhibition ya kazi za mikono Osaka Japan nafasi ambayo serikali ya Japan imewapa bure bileshi Tanzania ili isaidie wafanyabiashara wadogo wa Sanaa za mikono lkn baada ya kupata nafasi hiyo nilitakiwa nilipe ada ya ushiriki(participation fee) niwe na mzigo wa kuonyesha na kuuza niwe na nauli pesa ya kula pesa ya usafiri wa mzigo kutoka Tanzania mpk Japan pesa ya kutolea mzigo Japan hizo pesa zilikuwa nyingi kwa mfanyabiashara mdogo kumudu hivyo nilishindwa.

Lkn nafasi kama hiyo hiyo ukiomba south Africa unalipiwa nauli na serikali yao freight charges pesa ya kula na gharama ya kurudisha mzigo kama ukibaki kwenye show. Hapo unaona kabisa mfanyabiashara wa tz ataendelea kudoda wa south anapeta kwani gharama yake ni kununua mzigo tu.
 
Wanunuzi wengi wa Tanzanite pale Arusha ni wahindi,wakenya,wachina,na apolo kutoka SA. Wafanyabiasahara wakitanzania wachache ndio wanaweza kununua madini na kwenda kuuza nje.
Kwanini wachimbaji wenyewe wasiende kuuza nje hata wamiliki wa migodi?
 
Tangu tumeanza kuzalisha hizo bidhaa, zina mchango gani kwa Tanzania katika soko la kimataifa?
Maziku haya maswali yako unarudia maswali ya hoja(thread) kuu aliyoleta Paschal(Paskali). Na ndio tunahitaji majibu hapo haujajibu you are just spinning around. Ningeshauri tungejikita ktk kutafuta chanzo cha tatizo kwa namna au lengo la kupata ufumbuzi au njia mbadala kuliko kutafuta wa kumlaumu bila kupata ufumbuzi. Tufanye kama mbinu zinazotumika ku-improve human performance ktk industry ya aviation hasa civil aviation. Kule kukitokea tatizo wanatafuta chanzo nini sio nani, wanatafuta chanzo nani ili kupata historia kabla ya tukio ili kutambua vyanzo vya human errors na mazingira ya kazi kama yalichangia tatizo (i.e. Fatigue and ergonomics or other health and physicological problems). Kwa mfano kama tatizo chama fulani basi ijulikane ni kitu gani hasa wanafanya hao chama A au B kinasababisha hili tatizo, ukikiondoa kile chama bila kujua tatizo lao halisi ni nini kunauwezekano wa kuja chama kingine kikafanya makosa yaleyale lakini ukijua kipi hasa basi chama kingine kikija na huku kinaijua sababu ya kufeli wenzao hawatarudia kosa na hawatabahatisha huenda hiki ndio tatizo kumbe sio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…