Mla Bata
JF-Expert Member
- Jan 24, 2013
- 7,841
- 17,491
- Thread starter
- #41
Well, swali zuri Kiranga nadhani pia ingefaa ningeanza uzi wangu kwa kushare maana ya life purpose because for i what i have seen kwa michango ya watu wachache waliotangulia wengi hawajui nini maana ya LIFE PURPOSE.First things first, what is purpose?
Kwa kuanzia a life purpose ni lile lengo au dhumuni kuu ambalo individual anakuwa nalo apart from all the basic things, kila mtu ana Life purpose yake, wapo walioumbwa duniani hapa kwaajili ya kutimiza jambo fulani kwenye jamii, kuwafikisha watu mahali fulani, wao wenyewe kufikia mahali fulani etc, like unafanya kazi unapata hela na kuwa na uwezo wa kupata milo na pesa za matumizi ya kila siku lakini you feel that is not enough kipo kitu ambacho kina maana kubwa sana kwenye maisha yako na ni zaidi ya vitu basic, kugundua your life purpose sio jambo rahisi, wapo watu mpaka wanakufa hawajawahi kujua kwanini wamekuja duniani kuishi, hii inakwenda beyond a normal thinking capability.
Hujawahi kukaa peke yako kukawa kuna kitu ndani ya nafsi yako kinakwambia there is something missing in your life? Wapo watu wana kazi zinazowaingizia kipato kizuri lakini from nowhere wanaamua kuacha na kwenda kufanya jambo ambalo halimuingizii hata pesa kwasababu tu linampa furaha na kumpa maana ya maisha, thats a Life purpose, ni kile kitu ambacho ukikifanya nafsi yako inakuwa na amani zaidi na kupata maana na furaha ya maisha.
Hii utaipata pale ambapo hivi vitu basic vinakuwa in surplus sasa masikini wenzangu hawawezi kuona purpose ya maisha wakati hata kupata mlo wa siku tu ni tatizo, unajikuta unaspend the rest of your life kutafuta mkate wa siku na kusahau hata kujua ulikuja duniani kufanya nini.