What Made You Stay?

Dah!! Tuko yaani mimi nashindwa kuelewa ni kwanini na hichi kisa cha kaka yako ndio kimenimaliza kabisa
 
hivi, mwanamke anazaliwa hapa duniani aje kuozeshwa, kuzalishwa, na kumnyenyekea mumewe tu?
kama una mtoto wa kike,---binti--- hapo nyumbani na unampenda, jiulize utamteteaje mwanao kwenye hali kama hii...

Nafikiri sijui kama watu wanaangalia upande wa pili, i just wish you could see this lady uone picha wakati alipokuwa anaolewa na sasa hivi alivyo machozi yanaweza kukutoka mkuu
 
Gaga ukimuona huyu dada sasa hivi unaweza kusema hivi duniani kuna watu wanyama kiasi hiki ngoja nisiendelee kuongea maana inauma na inasikitisha sana hivi kwanini binadamu tunabadilika tunakuwa na roho za ajabu kiasi hiki lakini
 
Rocky, nitavumilia yoooote lakini sio kupigwa mpaka kuumizwa kiasi cha kushindwa hata kutembea, kwa kweli hapo tu siwezi

gaga kwa hiyo ukipigwa ukavimba kidogo au ukapata tu maumivu ya kawaida na kesho ukaweza kwenda job utavumilia?
 
Mimi huwa siamini kuvumilia kwenye kupigwa maana hapa ni kuwa unakaribisha kifo leo na kesho baba anapandishwa kizimbani kwa makosa ya kumuua mkewe sijui hapo watoto wanapata picha gani
 
Nailyne uliyoongea hapa ni moja katika ya vitu vilivyotokea kwa huyu dada nafikiri naweza kusema kujitambua pia ni jambo muhimu
 
tatizo watu wanapenda kukimbilia kwenye ndoa bila kusomana inatakiwa watu mpitie hatua tati kabla ya ndoa
URAFIKI
UCHUMBA THEN
NDOA
maana kama mti ni rafiki yako hawezi kukuumiza hata kidogo mimi mume nimtakaye lazxima awe best yangu vibaya mno
 
bebii i knw i couple walikuwa na mahusiano for ten years before they got married n a year after they got married jamaaa akaanza kutandika mkewe hapo utasema hawakujuana hawa?
 
Gaga ukimuona huyu dada sasa hivi unaweza kusema hivi duniani kuna watu wanyama kiasi hiki ngoja nisiendelee kuongea maana inauma na inasikitisha sana hivi kwanini binadamu tunabadilika tunakuwa na roho za ajabu kiasi hiki lakini

..Ibilisi amekamata ufahamu wao.
Nasema ni Shetani kwasababu iweje yule ulompenda kuliko wengine wooote, umtendee hivyo?
Aliimba Ndalla Kasheba(rip) wimbo uitwao Gaba, ulikuwa na maneno haya.."bora maskini huru kuliko tajiri mtumwa", alikuwa akiongelea kisa cha mwanamke anayeteswa na kupigwa na mumewe daily!!!

Ni bora ndoa ikavunjika ukaondoka na viungo vyako vyote, kuliko ukaendelea kubaki kwa mumeo na ulemavu wa kudumu!!
 
bebii i knw i couple walikuwa na mahusiano for ten years before they got married n a year after they got married jamaaa akaanza kutandika mkewe hapo utasema hawakujuana hawa?
Kuna watu wanabadilika tena wale ambao hata haukutegemea hadi unaanza kusema hivi kweli ni huyu ama kuna kitu kingine zaidi ya hicho
 
kwakweli haya mambo ni magumu sana, mm huwa najifikiria mara 2 kuhusu kuingia kwenye hiyo institution, cha ajabu Mungu aliweka ndoa kwa makusudi mazuri kabisa, lakini mwe mambo yamegeuka shetani anajua kabisa ndoa yenye furaha na upendo ndo chanzo cha mafanikio kila idara, mana kama nyumbani kuna migogoro hata kazi ofisin haziendi, watoto hawatafanya vizuri shuleni, tumuombe sana Mungu hasa ss ambao hatujaingia huko ili tupate wenzi ambao kwao tutajenga ndoa bora, kwa walioko ndani ya ndoa kuombea ndoa zenu ni jambo la muhimu sana, Mungu atutie nguvu
 
Ni bora ndoa ikavunjika ukaondoka na viungo vyako vyote, kuliko ukaendelea kubaki kwa mumeo na ulemavu wa kudumu!!
Domhome wengi wanakuja kuondoka au wanakuja kushtuka baada ya kuwa tayari mwilini ana ulemavu wengine hata kifo kinawakuta humo humo
 
Rocky, nitavumilia yoooote lakini sio kupigwa mpaka kuumizwa kiasi cha kushindwa hata kutembea, kwa kweli hapo tu siwezi

Ila huwa nashangaa sana katika hali ya sasa bado kuna watu wananyanyua ngumi kuwapiga wake zao. Ni jambo la ajabu sana
 
Tunahitaji sana kumuomba na kumshirikisha Mungu kwenye kila hatua ya masuala haya
 
Bebii TF yuko single na in search

BTW hgaijalishi hata kujuana wala kukaa na uchumba muda mrefu. Watu wengine hata kwenye uchumba wanawatandika watu wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…