Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,752
- 7,861
Rocky, nitavumilia yoooote lakini sio kupigwa mpaka kuumizwa kiasi cha kushindwa hata kutembea, kwa kweli hapo tu siwezi
...kwahiyo unajikubalisha kofi moja au mawili mradi uweze kutembea? 🙁
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Rocky, nitavumilia yoooote lakini sio kupigwa mpaka kuumizwa kiasi cha kushindwa hata kutembea, kwa kweli hapo tu siwezi
Dah!! Tuko yaani mimi nashindwa kuelewa ni kwanini na hichi kisa cha kaka yako ndio kimenimaliza kabisaMkuu inaniwia ngumu sana kupredict ni nini kinachwafanya wanawake waendelee na ndoa za namna hiyo, hasa katika dunia ya sasa (tukiacha yale ya wazee wetu zamani vijijini). Hii case uliyoitoa, naamini ni case tofauti, lakini kwa asilimia zaid ya 95 imafanana na case ya kaka yangu. Kamtesa mkewe kwa namna ya ajabu. mara ya mwisho nilipowaona, shemeji alinielezea namna alivyokuwa anateswa, na kaka alikiri ni kweli. Kwa wakati huo walikuwa wameachana na kaka alinisihi nimuombee msamaha kwa mkewe arudi home. Nilimwambia ngoja niongee nae in private, nikatumia mwanya huo kumsihi shemeji yangu asirudi kwa kaka kamwe, na kama ni watoto nitamsaidi japo kiasi fulani cha ada.
Kwa kweli sikupenda kushauri hivyo, lakini nilipoambiwa kuwa kaka alikuwa anampa kisago mkewe, tena gengeni, kisha anamvua nguo ZOTE mbele za watu na anamkokota kupeleka nyumbani, tena sio mara moja, sikuona ni kwa nini udhalilishaji wa namna hiyo unaweza kustahili msamaha, japo ni kaka yangu. Huwezi kuamini, miezi miwili tu baada ya mimi kuachana nao nilisikia walikuja kurudiana. Kama ilivyotegewa, haukupita mda mrefu, ngoma ikarudi pale pale, na kama wiki mbili zilizopita kaka alikuwa anapanda kizimbani kujibu tuhumu ta kujaribu kumchinja mkewe. kwa kuwa nilishaamua kujitoa katika mambo yao, sijui hata ni nini kinaendelea hadi sasa...
Nafikiri sijui kama watu wanaangalia upande wa pili, i just wish you could see this lady uone picha wakati alipokuwa anaolewa na sasa hivi alivyo machozi yanaweza kukutoka mkuuhivi, mwanamke anazaliwa hapa duniani aje kuozeshwa, kuzalishwa, na kumnyenyekea mumewe tu?
kama una mtoto wa kike,---binti--- hapo nyumbani na unampenda, jiulize utamteteaje mwanao kwenye hali kama hii...
Gaga ukimuona huyu dada sasa hivi unaweza kusema hivi duniani kuna watu wanyama kiasi hiki ngoja nisiendelee kuongea maana inauma na inasikitisha sana hivi kwanini binadamu tunabadilika tunakuwa na roho za ajabu kiasi hiki lakiniTf kwa kweli udhalilishaji wa aina hiyo uko mwingi sana, eti inasemekana wanawake wengi hawavumilii wanaume wao wanapo cheat ila kupigwa huwa wanavumilia, nina dda angu aliteswa ni mweupe half cast alikuwa anapigwa mpaka anakuwa wa purple mwili mzima, anabakwwa na mumewe, hakuna aliyeweza kumtoa pale kwenye mateso, tena ukimkuta na hali hiyo anakwambia kadondoka bafuni, mara mlangoni kwenye ngazi, ila watoto wake walikuwa wanatuambia, hakuna ushauri wa kuondoka alioupokea, mpaka kuna siku akanipigia simu niko mahala fulani nimehamia sina jiko wala sufuria wala nguo
kwenda pale nikaingia kapanga nyumba upande analia hapo ndipo alipoamua kuondoka, mwenyewe bila kulazimishwa na mtu,sasa hivi yuko happy na maisha yake na watoto wake anasema sijui ni nini alikuwa anang'ang'ania pale
Lol!!! Umeniacha hoi Bebii bana ulogwe na nanii tenatf weweeeee? Unataka nilogwe humu?
Rocky, nitavumilia yoooote lakini sio kupigwa mpaka kuumizwa kiasi cha kushindwa hata kutembea, kwa kweli hapo tu siwezi
Mimi huwa siamini kuvumilia kwenye kupigwa maana hapa ni kuwa unakaribisha kifo leo na kesho baba anapandishwa kizimbani kwa makosa ya kumuua mkewe sijui hapo watoto wanapata picha ganiWakati mwingine huwa wanavumilia tu na kuhisi labda mwanaume au mume anaweza kujirudi na kuacha tabia za namna hiyo (Kumpiga n.k) pia ni watu wengi tunapenda watoto wetu wawe kwenye malezi bora ya baba na mama na ndio maana (mama wengi) wanafanya hiivi
wewe uko occupied bwana tena upo na full securitylol!!! Umeniacha hoi bebii bana ulogwe na nanii tena
-kwanza ni kutojitambua ndiko kunafanya wanawake wengii kubaki katika maisha hayo
-jamii zetu jamani, haya mambo huwa yaanza taratibu,unapigwa mara ya kwanza hata watoto huna, malezi yetu wanawake tunaaambiwa mamboo ya ndoa siri usiseme,unavumilia humwambii mtu, anarudia tena unakaa kimya, akirudia tena tayari mna watoto, na wewe ndio unapata akili ya kwenda kushtaki kwa wazazi, unaambiwa vumilia tuu sasa mna watoto unafikiri ukiondoka itakuwaje?
-uchumi tegemezi sio wote lakini wapo wanawake ambao wapo kwenye maisha hayo coz ahahisi akiondoka hataweza kuhudumia watoto peke yake so heri apate hiyo shida ili watoto wake hata waende shule
-ukiachika jamii itakuonaje, hutaeshimika tena, hupewi nafasi kwenye jamii so ni bora kuvumilia mateso kuliko jamii kukunyoshea kidole umeshindwa ndoa
- viapo vya dini esp wakristo ndoa maanake hadi kifo kiwatenganishe so no matter wat u hv to hold on
-experience, haya mambo yapo sana kwenye familia zetu mwanamke aliyetoka kwenye familia ambayo mama yake alikuwa abused na baba yake hata yeye akipata shida kama hizo ataichukulia hiyo hali ni kawaida na kwamba maisha ya ndoa yanapaswa kuwa hivyo
- hoping that atabadilika siku moja!!
...kwahiyo unajikubalisha kofi moja au mawili mradi uweze kutembea? 🙁
gaga kwa hiyo ukipigwa ukavimba kidogo au ukapata tu maumivu ya kawaida na kesho ukaweza kwenda job utavumilia?
Lol!!! Weee Bebii duh full security tenawewe uko occupied bwana tena upo na full security
tatizo watu wanapenda kukimbilia kwenye ndoa bila kusomana inatakiwa watu mpitie hatua tati kabla ya ndoa
URAFIKI
UCHUMBA THEN
NDOA
maana kama mti ni rafiki yako hawezi kukuumiza hata kidogo mimi mume nimtakaye lazxima awe best yangu vibaya mno
Gaga ukimuona huyu dada sasa hivi unaweza kusema hivi duniani kuna watu wanyama kiasi hiki ngoja nisiendelee kuongea maana inauma na inasikitisha sana hivi kwanini binadamu tunabadilika tunakuwa na roho za ajabu kiasi hiki lakini
Kuna watu wanabadilika tena wale ambao hata haukutegemea hadi unaanza kusema hivi kweli ni huyu ama kuna kitu kingine zaidi ya hichobebii i knw i couple walikuwa na mahusiano for ten years before they got married n a year after they got married jamaaa akaanza kutandika mkewe hapo utasema hawakujuana hawa?
Domhome wengi wanakuja kuondoka au wanakuja kushtuka baada ya kuwa tayari mwilini ana ulemavu wengine hata kifo kinawakuta humo humoNi bora ndoa ikavunjika ukaondoka na viungo vyako vyote, kuliko ukaendelea kubaki kwa mumeo na ulemavu wa kudumu!!
Rocky, nitavumilia yoooote lakini sio kupigwa mpaka kuumizwa kiasi cha kushindwa hata kutembea, kwa kweli hapo tu siwezi
Tunahitaji sana kumuomba na kumshirikisha Mungu kwenye kila hatua ya masuala hayakwakweli haya mambo ni magumu sana, mm huwa najifikiria mara 2 kuhusu kuingia kwenye hiyo institution, cha ajabu Mungu aliweka ndoa kwa makusudi mazuri kabisa, lakini mwe mambo yamegeuka shetani anajua kabisa ndoa yenye furaha na upendo ndo chanzo cha mafanikio kila idara, mana kama nyumbani kuna migogoro hata kazi ofisin haziendi, watoto hawatafanya vizuri shuleni, tumuombe sana Mungu hasa ss ambao hatujaingia huko ili tupate wenzi ambao kwao tutajenga ndoa bora, kwa walioko ndani ya ndoa kuombea ndoa zenu ni jambo la muhimu sana, Mungu atutie nguvu