The Finest..............this is so touchy jamani. Hivi wanaume wengine wamelelewaje/ hivi jamii yetu inafikiria je?.
Ni kweli kuwa hii inachangiwa na kutokujitambua lakini naamini pia malezi na jamii zetu kwa kiasi kikubwa zinachangia na kama kuwajibika basi a major transformation need to be done. Maneno ya ndoa ni kuvumilia yawe na mipaka i.e. limit? kuvumilia vitu gani na gani vya kutovumilia.
I have been there. Yes in a very abusive relationship tena ya mtu ambaye nilimpenda kiasi cha kusacrifice mambo mengi sana including elimu yangu and all that (najua mpo mtakaosema MWJ1 ulikuwa mjinga, unaacha elimu ikupite kushoto kwa ajili ya mwanaume!!? nitawaelewa). Sacriface nyingi sana ambazo nilizifanya kwa jina la mapenzi ! The Sacrifice ambayo ilinibidi niiweke katika moja wapo ya items muhimu na endelevu kwenye maisha yangu. Nikiwa kama binadamu ambaye siko perfect ninakiri na ninaamini kuwa nilikuwa na part yangu lakini kwa mtazamo wa nje na yale yote muhimu nilijitahidi (na yeye anakiri leo kuwa ali'pitiwa na shetani) nilikuwa mjinga na ilinichukua muda kurealize kuwa ninakuwa abused. (Ninapenda kuwajulisha kuwa MWJ1 wa enzi hizo ni yule alokuwa anafahamika kama mlokole....... yule ambaye alikuwa akimaliza kugawa tunda pamoja na kuwa ni halali anahisi anatakiwa kutubu!) Kila siku ikawa ni sacrifice, sacrifice only to realize kuwa haitokaa siku akatosheka na wala akabadilika. Ilinichukua muda kuamua kwanza kuuvunja ukimya na kisha kuchukua hatua ambayo nakiri haikuwa kazi rahisi hata kidogo na hii ilichangiwa na jamii niishiyo ambapo mpaka wazazi wangu (ambao si kuwa tu mimi ni mtoto wao wa kwanza, bali pia mtoto pekee kati ya watoto 5) ambaye angalau nilikuwa na kajidiploma kangu ualimu, hata hao wazazi walinifukuza wakitoa sharti la kurudi kwenye uhusiano wangu na huyo mwenza. Katika mwaka ambao sitakaa niusahau humu duniani ni mwaka ule. Nilijuta kuingia katika kifungo nikingali msichana (si mdogo sana) but nikingali mchanga ambaye sikuwa na pa kusimamia. Pocket money niliyokuwa napewa na wazazi ilikatwa, nikaishi maisha ya kuhangaika na kudowea kwa marafiki (namshukuru MUNGU sikuwahi kuwaza maovu zaidi lakini shukrani zangu za maisha ziende kwa rafiki yangu wa kike ambaye yeye pamoja na kuwa si tajiri bali aliwezakunikimu kwa kugawana pocket money aliyokuwa akichangiwa na dada zake na kunipa kalazi na chakula mpaka nilipomaliza chuo).
Haikuishia hao, chuoni nilipokuwa nasoma nilionekana msichana niliyeshindikana, anawezaje kuondoka kwenye mahusiano madhubiti kama yale! anataka awe huru ili awe changudoa, ameona anabanwa na maneno chungu mbovu kiasi cha kuona kabisa unapopita unanyooshewa vidole na unaposogelea kundi lal marafiki wanatawanyika. ! Mtaani ndio usiseme. Maisha yalikuwa magumu kupindikia mpaka MUNGU aliponibariki kazi yangu ya kwanza ambapo nilifanikiwa kuhama mtaa na chuo na kuanza maisha mapya, nikiwa nimetengwa na ndugu, jamnaa na marafiki isipokuwa rafiki yangu alitenivumilia nilipoanguka!
Mtu ukiyafikiria haya yote utagundua kuwa kujitambua peke yake hakutoshi bila kuwa na ujasiri na a hand to hold you on maana it is not easy at all. Mchana utatembea kichwa juu macho miita mia kujifanya u strong but usiku hulali kwa kulia na wengine kujiingiza kwenye ulevi kama si kunusuriwa na mauti.
unapoisoma hii post ninakuomba wewe mwanamke utafakari, ujiweke kwenye nafasi ya huyu MwJ1 (wa enzi hizo). Fikiria mazingira yote yanayoukuzunguka kuanzia thamani yake (kwa jinsi unavyoidefine wewe, wazazi wako na jamii inayokuzunguka)
2. Ukikumbuka kuwa decision making at household inatawaliwa na baba, mama anawezakuumia sana juu ya maumivu yako lakini kumbuka uamuzi wa mwisho unatolewa na mzazi wako wa kiume (wangapi ambao wazazi wao wa kiume wanasymphasize nao achilia mbali wale ambao hawana wazazi wa kiume au wana wazazi ambao si wazazi wa kumzaa)
3. Fikiria nafasi ya mwanamke mwenzioa ambaye hana kazi nzuri ya kumsustain yeye na wanae kama ataamua kuondoka kimoja; na mazingira yote yanayomzunguka..wanawake wengine hawana elimu, hawajui haki zao n.k
So ninawaomba ndugu zangu kabla ya kufanya "Victim blaming' ninawaomba tuwaangalie hawa wanawake wanaokuwa abused kutoka katika mazingira halisi wanayoishi. Am telling you wanawake ambao wana ujasiri wa kusimama na kuamua 'enough is enogh' wabebe misalaba yao na majukumu ya watoto wao ni 3 kati ya kumi.
Karibuni