Basi ntakwambia wewe.
Nlipomaliza chuo nlipata nafasi bank flani hivi nifanye kama intern huku yule manager akinipa moyo kama ntafanya vizuri basi ntaajiriwa. Nkafanya pale for three month, Sept, Oct and November. Graduation ikafika nkaenda kwenye graduu. Kurudi nakuta kuna mtu kaajiriwa, it never went well with me so nkakaa for two weeks halafu nkasema ngoja nisepe nkatafute channel Dar. Nisambaze bahasha weeee halafu niende Tanga.
Miongoni mwa ma-bank nilizokwenda moja ni NBC pale posta ya zamani. Kufika pale nkaingia front office nkawaambia jamaa pale nataka kuonana na either HR au Marketing Executive, washkaji (marika yangu kabisa) wakaniambia do you have appointment?? Nkawaambia sina but I need to meet these people, wale jamaa kwa dharau kabisa wakaniambia you can't meet them.
Nkakaa kama dakika 3 hivi nafkiria cha kufanya huku nimechoka na nina hasira, nkawafuata nkawaambia mnajua wakija wakijua kwamba mmenikatalia kuwaona bila sababu itawaletea tabu?? Wakaniambia for sure hawa watu bila appointment ni ngumu ila kama una maagizo tuachie tutawapa. Nkawaambia ok, mwambieni Marketing executive yule jamaa mwenye zile 300 accounts kaja.
Jamaa kuskia vile nafkiri head of front office akaniambia ok subiri. Straight away akapiga simu, mara akaniita nkaongee na simu pale pale, kufika nkachkua simu, hallo, yes hello! Wewe ni nani na nimeambiwa unazo 300 accounts, nkamwambia yeah ninazo but I wont give them to you until I get my cut. Akaniambia mpe simu huyo mtu, wakaongea ghafla yule jamaa ananipa visitors card ananifahamisha mensa kwenye lift mpaka ghorofa ya saba Marketing executive anakusubiri. Nkapanda lift, kufika ghorofa ya 7 ule mlango wa lift kufunguka tu, hammadi mwanadada kisuuuu. Are you Relief?? Yeah I am, come to my office. Kufika ofisini kilichotokea, next episode